Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Haiitwi Uhuru wa wakaldayo inaitwa Uru wa wakaldayo au Ur of Chaldeans..
Hilo la kwanza..
unahisi Ishamael hakuwa na Nchi aliyopewa?
Ishmael aliishi Parani akiwinda Huko..
Hizo ahadi zote ulizotaja Ni ahadi sawa na alizoahidiwa Ishmael
Haya tusome mwanzo 17:20
View attachment 3021508
kwa lugha ya Anko charles Pale Uk
Mwanzo 17:20
"And as for Ishmael, I have heard thee: Behold, I have blessed him, and will make him fruitful, and will multiply him exceedingly; twelve princes shall he beget, and I will make him a great nation."
Kwanza Mungu amesema
- Amembariki (Blessed Him)
- Amemzidisha (Make Him fruitful)
- Atamzidisha Uzao wake (Multiply Him Exceddingly)
- Atazaa watawala 12 (12 Prince)
- Naye atamfanya Awe Taifa kuu..
Hoja zako Nchi ya Kanaani
Isaka Alipewa kanaani ila Ishamael alipewa Beersheba, na Parani
We unahisi kwanini Watoto wengine wa Ibrahimu Hawatajwi sana au hawatajwi kabisa Kwa sababu waliobarikiwa Na kupewa Urithi ni wawili tu..
Ketura MKEWE MWINGINE WA IBRAHIMU ALIKUWA NA WATOTO 6 Ila sijaona mkiwajadili wengine wala hawajawahi kujadiliwa kabisa..
Kingine kuhusu Kwamba Isaka ni maarufu kuliko Ishmael...
kwa mfano nikikupa nafasi uandike Historia Ya ukoo wenu Je Utaweza kuniandikia Historia ya Kaka Yake na Babu yako?
waandishi wa Biblia wote ni Waebrani ana Wayahudi wote wametoka kwenye Uzao wa Watoto 12 wa Yakobo mtoto wa Isaka na ndo maana Hata Historia ya Esau (Edomu) pia huwezi kuipata..
Mkuu kwanza kwenye biblia au hata Quran sijawahi kusoma kuwa Ishmael alipewa nchi ya Harani. Sijawahi kwa kweli.
Umesema vizuri
Moja ya ishara kuwa aliyetimiza ahadi ni Isaka ni hilo la taifa lao kuwa mpaka hivi leo.
Mimi na wewe na hata jamii zingine nyingi hazijui Historia zao.
Huyo Muhammad mwenyewe hajui ni kwakivipi ametoka kwa Ibrahim.
Hao waarabu wanaojinasibisha na Ibrahim wenyewe hawaelewi na ushahidi uliowazi kuwa Baba yao ni Ibrahim.
Hata ikiulizwa uzao au taifa la waishmael ni lipi sasa hivi hakuna majibu.