CHIEF NZELLAH
Member
- Jan 7, 2014
- 31
- 16
Mkuu hakuna kitu kama hicho mkiristu anaweza kufanya kama wewe, kwamba kusherehekea kukombolewa kwa huyo jamaa, inshort haina ishara kwa mkristo maana huyo jamaa hakuwa na ishara iliyotolewa na mwenyeezi Mungu kwamba apewe nafasi yoyote kwa ukumbusho.Waislamu mpaka leo hii wanaadhimisha kukombolewa kwa huyu mtoto wa Ibrahim alietakiwa kuchinjwa, maadhimisho haya hufanywa kwa kuchinja mnyama kama alivyokombolewa yule mtoto. Pia Maadhimisho haya yanafanywa baada ya kukamilisha ibada ya Hija ambayo kimsingi hufanyika katika mji wa Makka mji wenye nyumba tukufu ya Al-Qaaba, according to Islam Al-Qaaba ilijengwa tena upya na Ibrahim na mwanawe Ismail.
Yani yote hayo juu yanahusishwa Ibrahim na Ismail lakini bado mnataka kulazimisha kuwa huyo mtoto alitakiwa kutolewa sadaka alikuwa ni Isaak? Hili ni jambo kubwa sana lakini mbona hatulioni kuadhimishwa kukombolewa kwa huyu mtoto kwenye ukristo wala uyahudi ispokuwa tunaliona kwenye uislamu tu?
Mtoto wa HARAMU ni mtoto wa HARAMU tu.Wanabodi,
Leo ni sikukuu ya Eid El Haji, Iddi ya Kuchinja.
Leo ni siku ya Sikukuu ya Idd El Haj, ni iddi ya kuchinja, asubuhi nilikuwa naangalia matangazo ya mubashara ya Baraza la Iddi kupitia TBC, kutoka Msikiti wa Mfalme Mohammed VI wa Morroco, Bwakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, kumbe Msikiti Mkuu wa Bakwata, sasa umebadilishwa jina!, na kupewa jina la Mfalme wa Morroco!.
Mgeni rasmi kwenye Baraza la Iddi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, ambaye ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambaye amesilimishwa na kupewa jina la Aboubakar Chalamila!, na mawaziri akiwemo Waziri Mhe. Mohamed Mchengerwa. Baadhi ya watu maarufu niliowaona ni pamoja na Alhaj Sheikh Ali Nguruko, Alhaj Chande, Idda Azan, Shaweji Abdalah, Salum Mwalimu, Juma Simba Gadafi, Salum Abladaha "TRY Again", Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mruma, Kadhi wa Dar es Salaam, Shamin Khan, mwenyekiti wa JUAKITA, pia kulikuwa na mabalozi wa Balozi wa Moroko, na wa Comoro.
Katika salam zake, Sheikh Aboubakar Chalamila alisema utulivu wa jiji la Dar es Salaam, unawategemea sana viongozi wa Dini.
Salaam za Waislamu, zimetolewa na Alhaj Sheikh Nuru Mruma, Katibu Mkuu wa Bakwata ambaye amewasisitiza Waislamu kudumisha amani na kuilinda amani. Wazazi watakiwa kulea watoto wao kwa tabia njema, kujenga taifa la kizazi cha watu wema ambao hawatapokea rushwa wala kufanya ufisadi.
Amesema kupanda miti na utunzaji wa mazingira ni ibada muhimu kwa Waismamu wote.
Pia amewataka Waislamu kujitokeza kwa wingi, kujiandikisha kwenye uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.
na wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kidemokrasia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Salaam za Mufti, zimetolewa na Kaimu Mufti Sheikh Ali Muhidin Mporogore, Mjumbe wa Baraza la Maulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Bwakwata. Aamezungumzia Watanzania tutafakari, sadaka ya kuchinja siku ya Iddi El Haj, ni iddi ya kuchinja. Zamani ilikuwa sio kuchinja tuu wanyama, bali walichinja hata binadamu ana akatolea mfano Sadaka ya Nabii Ibrahim kutaka kumtoa mwanae Ismail, kwa sadaka ya kuchinja.
Hakuna ubishi kuhusu Wakristo na Waislamu, kuwa ni watoto wa Baba mmoja, Nabii Ibrahim hivyo huu ni uthibitisho wa Mungu wa Wakristo na Waislamu ni Mungu Mmoja, ila kuna watu wanafundishwa ukweli na kuna watu wanadanganywa!.
Hakuna ubishi kuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail aliyezaa na mjakazi wa Kimisri, Hagir, na Isaka ni mtoto wa pili wa Ibrahim, aliyemzaa na mkewe Sarah.
Hakuna ubishi Ibrahim alitaka kumtoa mtoto wake Sadaka ya kuchinja.
Waislamu na Kitabu chao Kitukufu cha Quran Tukufu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Ismail.
Wakristo na Kitabu chao Kitakatifu cha Biblia Takatifu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Isaka.
Jee ukweli halisi ni upi?.
Hii maana yake
Kama tukio la Ibrahim kutaka kumchinja mwanae kumtoa sadaka ni tukio moja, then
1. Hii maana yake ni kuna watu wanadanganywa, haiwezekani kwa Waislamu mtoto huyo awe ni Ismail na kwa Wakristu mtoto huyo awe ni Isaka, hii maana yake kuna kitabu hapo kinasema kweli na kuna kitabu kinasema uongo!, jee ukweli ni upi?.
Umuhimu wa kuujua ukweli huu, unakupa fursa ya kujua ukweli ni upi, hivyo ufuate mafundisho yapi ambayo ndio mafundisho ya kweli!.
Bandiko hili linakutaka kwanza uwe open minded, kama wewe ni mfia dini, unaamini dini yako ni ya ukweli mtupu, bandiko hili halikufai.
Pili unatakiwa uwe na ngozi ngumu ya kuukubali ukweli halisi hata uwe mchungu vipi!, ikitokea ni dini yako unayoiamini kuwa ni dini ya kweli, kumbe ni dini ya uongo, uwe na uwezo wa kustahimili maana...
Nawatakia Waislamu wote,
Iddi Mubarak njema ya kuchinja.
Paskal
Mwanzo 16:3Mtoto wa HARAMU ni mtoto wa HARAMU tu.
Ibrahim mwarabu wa Iraq toka mji wa ur,180km kaskazini mwa saudia
Unahangaika na nini wewe,vitu muhimu vyote kwenye QUR'AN vipo,ibada,sheria,mahusiano ya kijani,tawhiid...haihangaiki na birthday za watu
"What is the meaning of the word "Hebrew"? A definition" What Does The Word "Hebrew" Mean?Ibrahim ni Hebrew sio muarabu.
Únawajua waebrania?
Unajua lugha ya kiebrania?
Iraq hawakai waarabu tangu zamani
Assyrians únawajua?
Wewe Biblia huijui lakini unataka kubishana na wataalam wa Biblia. Nimesema kitabu cha Matendo ya Mitume. Sasa Yesu anatoka wapi kwenye hicho kitabu? Read to understandWapi yesu aliwahi kula nguruwe hata kwa bahati mbaya? Zaidi tunasoma aliyakemea mapepo yakakimbilia kwenye nguruwe na kutumbukia baharini
Sawa,..kwanza naomba tuweke biasness pembeni ili tupate jibu sahihi la mtoto yupi hasa aliyetaka kuchinjwa au kutolewa dhabihu kama ulivyosema........
Kwa nilivyofuatilia huu mjadala kuna hoja moja ambayo nadhani ndiyo ya wazi kabisa ameigusia DR Mambo Jambo ..... hoja ya umri wa wahusika pindi amri ya kuchinjwa ilivyotoka.....DR ameweka verses za Biblia ambazo zinaonyesha wazi kwamba wakati amri inatoka Ismail ndiyo mtoto pekee wa Ibrahim ambaye alikua ana :-
1. Uwezo wa kuongea (kama ilivyoonyeshwa kwenye biblia akijadiliana na Baba yake)
2. Uwezo wa kutembea zaidi ya Km 300,..kuelekea eneo ambalo tukio la kuchinjwa ilikua lifanyike.
NB: kwa mujibu wa hoja nilizopitia humu Ismail alikua na umri wa miaka 14,.wakati amri ya kuchinjwa inatoka........vipi kuhusu Ndugu yake alikua na umri gani? huenda alikua hajazaliwa au alizaliwa miezi michache baada ya tukio hilo.
So,. kimsingi kwenye hoja ya umri wa watoto husika... dadisi zinaonyesha Ismail ndiyo muhusika kwenye ishu ya kuchinjwa..endapo tukiondoa ushabiki nadhani tunaweza kukubaliana juu ya hili.
"What is the meaning of the word "Hebrew"? A definition" What Does The Word "Hebrew" Mean?
Muebrania/Hebrew ni muhamaji,ukihama ukonga ujaenda tandika wewe ni muebrania,Ibrahim aliitwa muebrania kwa kuwa alikua mhamiaji Tena wa kuvuka moto,bila shaka Euphrates na Tigris
Ndo maana nikasema Baraka za Isaka ni tofauti. Hakuambiwa kokote nitakubariki akiwa mwenyewe. Yeye karithi agano la baba yake. Ishmael ni tofauti, yeye alibarikiwa yeye kama yeye na Mungu lakini hakuingia kwenye agano. Agano lilifungwa Kwa Ibrahim na mzao wake.Lakini watoto ambao wametajwa Kubarikiwa kwenye Biblia na kutajwa kwa majina ni wawili tu sikusikia Median akibarikiwa zaidi ya Mbeleni huko kupewa lawama
Hapana Mkuu Waebrania sio Tafsiri hiyo.."What is the meaning of the word "Hebrew"? A definition" What Does The Word "Hebrew" Mean?
Muebrania/Hebrew ni muhamaji,ukihama ukonga ujaenda tandika wewe ni muebrania,Ibrahim aliitwa muebrania kwa kuwa alikua mhamiaji Tena wa kuvuka moto,bila shaka Euphrates na Tigris
Hawajui races zikizo wahi ishi duniani. Waarabu wapo Saudia hata watu wa Jordan sio waarabu. Ni w hashimite. Waturuki wenyewe sio waarabu. Hata wairan ambao ni wapersia sio waarabu. Watu wanapinga Biblia kwa kutumia BibliaIbrahim ni Hebrew sio muarabu.
Únawajua waebrania?
Unajua lugha ya kiebrania?
Iraq hawakai waarabu tangu zamani
Assyrians únawajua?
Agano lilifungwa Kipindi Ambacho Isaka hajazaliwa sasa sjui unazungumzia Agano lipi..Ndo maana nikasema Baraka za Isaka ni tofauti. Hakuambiwa kokote nitakubariki akiwa mwenyewe. Yeye karithi agano la baba yake. Ishmael ni tofauti, yeye alibarikiwa yeye kama yeye na Mungu lakini hakuingia kwenye agano. Agano lilifungwa Kwa Ibrahim na mzao wake.
Naamini wewe ni mwanaume, je sasa hivi ukizaa mtoto mkubwa wa kiume ukiwa na ndoa halafu mkeo akaja kuzaa mtoto je yupi ana haki ya kurithi Baraka zako? Wa nje ya ndoa au wa ndoa? Na Kwa Nini?
Hawajui races zikizo wahi ishi duniani. Waarabu wapo Saudia hata watu wa Jordan sio waarabu. Ni w hashimite. Waturuki wenyewe sio waarabu. Hata wairan ambao ni wapersia sio waarabu. Watu wanapinga Biblia kwa kutumia Biblia
Japo arabunj ilikuwepo ila Arabuni ya sasa sio arabuni ya Zaman..Hawajui races zikizo wahi ishi duniani. Waarabu wapo Saudia hata watu wa Jordan sio waarabu. Ni w hashimite. Waturuki wenyewe sio waarabu. Hata wairan ambao ni wapersia sio waarabu. Watu wanapinga Biblia kwa kutumia Biblia