Nikupe reference?
Hiko kisa kwenye Biblia kimeelezewa kwa mtiririko mzuri tuu.
Mwanzo 22
Mwa 22
SUV
MWA 22
1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. 2Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.
Utajiuliza mambo gani hayo. Utarudi Aya ya 21
ambapo inaelezea mambo makuu matatu
1. Kuzaliwa kwa Isaka
2. Kufukuzwa kwa Hajiri na Ishmael
3. Kuwekeana agano baina ya Ibrahim na Abimelek.
kisha Aya hii inaelezea
mwanzo 21
34Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.
Hizo siku nyingi hazitajwi ni siku ngapi au miaka mingapi lakini sura ya 22 inatupa picha kuwa ni siku nyingi ambazo Isaka alikuwa kijana ambaye angeweza kutembea na kupewa kitu akabeba.
Mwanzo 22
6. Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.