Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Mama yake Ismael alikuwa mkewe Ibrahim?
Ilikuwaje akaondoka hadi kupewa na Mungu chemchem ya zamzam?

Walitengana?
Story full ikoje?

Hajiri hajawahi kuwa Mke wa Ibrahim
Alikuwa kijakazi wa Sarah mkewe Ibrahim.

Aliyemfukuza Hajiri ni Boss wake ambaye ni Sarah.

Hiyo simulizi unaijua vizuri?
 
Kwa mujibu wa Quran na Biblia
Ismail wa kwanza
Vizuri,..Biblia inaonyesha wakati amri ya kuchinjwa kwa mtoto inatoka....Mtoto aliyekusudiwa kuchinjwa alikua na umri wa kuweza kuongea na kutembea umbali wa zaidi ya km 300....

Je, Kati ya Ismail na Isihaka nani umri wake unaendana na sifa za matendo ya kiumri ambazo Biblia imezitoa hapo?

NB:- Kwa mujibu wa Biblia amri ya mtoto kuchinjwa wakati inatoka,..mtoto pekee wa Ibrahim ambae alikua ana umri wa kuelewa mambo ni Ismail ( Umri wa miaka 14).
 

Toa hiyo Aya inayoeleza hivyo.
 

Baada ya Isaka kuzaliwa ilipita miaka mingi ndipo jaribio la kutaka kutolewa kafara likatolewa
 
Ukitaja Biblia tayari umeshamtaja Isaka kama kijana aliyetaka kutolewa kafara.

Tukio linaelezwa baada ya Ishmael na Mamaake kufukuzwa.
Nadhani umegoma kabisa kuchukulia umri wa watoto husika kama kigezo cha msingi cha kujua nani hasa alikusudiwa kuchinjwa....

Hoja yangu Mimi ilikua hapo,... ahsante.
 
Watoto wa Bilha na Zilpa wanahesabiwa kwenye uzao wa Leah na Rahel. Ila pamoja na hayo yote Kun haki msingi hawakuzipata. Reuben alipotenda dhambi atanyang'anywahaki ya uzaliwa wa kwanza haikwenda Kwa mtoto wa Zilpa au Bilha, ilienda Kwa Yusuphu mzaliwa wa kwanza wa Rahel. Mpaka uwe kwenye ndoa ndio unakua na haki ya kurithi.
 
Nadhani umegoma kabisa kuchukulia umri wa watoto husika kama kigezo cha msingi cha kujua nani hasa alikusudiwa kuchinjwa....

Hoja yangu Mimi ilikua hapo,... ahsante.
Tumia Quran kutetea hoja yako. Usitumie Biblia. Mnasema kimeongezwa Kwa hiyo sio sahihi kwenu.
 
Toa hiyo Aya inayoeleza hivyo.
DR Mambo Jambo ....ameelezea kwa kina hapa kuhusu hizo Aya unaweza ukarudi kwenye posts zake zilizopita.....

Nikinukuu points za msingi alionyesha:-
Umri wa Ibrahim wakati anazaliwa Ismail,..Kisha akataja umri wa Ibrahim wakati! anazaliwa Ishaka......ambapo inaonyesha kulikua na utofauti wa kiumri wa miaka 14 Kati ya Ismail na Isihaka.


Rudi kwenye posts zilizopita naamini uliziona.
 
Nadhani umegoma kabisa kuchukulia umri wa watoto husika kama kigezo cha msingi cha kujua nani hasa alikusudiwa kuchinjwa....

Hoja yangu Mimi ilikua hapo,... ahsante.

Nikupe reference?
Hiko kisa kwenye Biblia kimeelezewa kwa mtiririko mzuri tuu.
Mwanzo 22
Mwa 22
SUV

MWA 22​

1 Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu, akamwambia, Ee Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. 2Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

Utajiuliza mambo gani hayo. Utarudi Aya ya 21
ambapo inaelezea mambo makuu matatu
1. Kuzaliwa kwa Isaka
2. Kufukuzwa kwa Hajiri na Ishmael
3. Kuwekeana agano baina ya Ibrahim na Abimelek.

kisha Aya hii inaelezea
mwanzo 21
34Ibrahimu akakaa hali ya ugeni katika nchi ya Wafilisti siku nyingi.

Hizo siku nyingi hazitajwi ni siku ngapi au miaka mingapi lakini sura ya 22 inatupa picha kuwa ni siku nyingi ambazo Isaka alikuwa kijana ambaye angeweza kutembea na kupewa kitu akabeba.

Mwanzo 22
6. Basi Ibrahimu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.
 
Kitabu hapo cha kuaminiwa ni Toraut ya wayahudi,kurwani ni kopi na paste ya uongo kutoka kwa mudi ili kupoteza hitoria ya kweli.



View: https://www.youtube.com/watch?v=idnql9Ro7bU&t=28s&pp=ygU2bmFuaSBhbGl5ZXRha2l3YSBrdWNoaW5qd2EgaXMtaGFrYSBhdSBpc21haWxpLCBtYXppbmdl
 

Ibrahim wakati anamzaa Isaka alikuwa na miaka 100.
Ishmael 14.
Lakini Biblia haijasema kuwa alipewa jaribio hilo akiwa na miaka 100

Ndio maana nikasema Aya zitolewe.
Tukio au kisa hiko kipo kwenye mwanzo 21 na 22
 
Sawa.. naomba niulize swali.....Wakati amri ya mtoto kuchinjwa inatoka, Isihaka alikua na umri wa miaka mingapi,, kwa mujibu wa Biblia?
 
Biblia inamtaja mwana wa pekee kuwa ni Isaka bila kupepesa macho

Kwa kuwa muda huo Ismail alikuwa kashaondoka na mama yake muda mrefuu kwenda jangwani wakapewa zamzam water hii mnayoikuta mkienda Hijja
 
Sawa.. naomba niulize swali.....Wakati amri ya mtoto kuchinjwa inatoka, Isihaka alikua na umri wa miaka mingapi,, kwa mujibu wa Biblia?

Haijaeleza umri wa Isaka wala umri wa Ibrahim.
Ila siku nyingi zilipita ambazo Isaka alikua kwa kiasi cha kuweza kubeba kuni.
Muda huo Ishmael nduguye alikuwa amefukuzwa miaka mingi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…