Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Hilo andiko Ni Moja kwenye Bible nzima na Ukiangalia Original yake in hebrew halisemi wakeze linasema Wanawake wake..

So obvious hakuwa..

Kwnza kabisa harusi ilifanyika kwa ulaghai aliambia Anamuoa Rahel ila amemaliza kulala naye asubuhi anakuta sio Rahel ni lea ndo alipomfata mkwewe kulalamika..

Kwakuwa Alikuwa amekwisha Kumbikiri sheria hairuhusu Kutokumtwaa ila alimtwaa kama mtu aliyelala naye..

Na ndo maana Ukisoma mbele ya Harusi hiyo siku ya Asubuhi Yakobo anasema anataka Mke wake 😅😅
Soma hii Aya yote Kijana..

Labani hakumpa Lea Yakobo awe Mkewe ila Alimpa Rahel Yakobo awe mkewe.. Soma aya ya 28
 


 

Ndio maana nikakuambia kuwa ukisoma Biblia usiishie kwenye aya moja.

Soma
Mwanzo 21:10,12-13
[10]Kwa hiyo akamwambia Ibrahimu, Mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi pamoja na mwanangu, Isaka.

[12]Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambialo Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka uzao wako utaitwa.

[13]Naye mwana wa mjakazi nitamfanya kuwa taifa, maana huyu naye ni uzao wako.


Hapo Mungu mwenyewe anamtambua Hajiri kama mke au mjakazi?
 
Kumbuka, sitetei hoja haoa, haoa nauweka ukweli kwa kutumia "tafsil" siyo "tafsiri".

Unajuwa tofauti ya tafsil na tafsir?
Jana ulisema unataka ushahidi wa Aya kutoka kwenye Qur'an ikionyesha kwamba Ismail ni mtoto wa Ibrahim,...Nikakuweka aya husika uliiona?
 
Hujajibu swali nililouliza.....

Katika watoto hao wote,..yupi amewahi kuwa mtoto wa pekee wa Ibrahim?

Namaanisha Mtoto yupi aliishi kipindi ambacho Ibrahim hakua na mtoto mwingine isipokua yeye?
Upekee aliousema Mungu hauhusiana na kuwa peke yake. Ndio maana huielewi Biblia maana unasoma kama kitabu kwingine. Ni sababu nimekwambia ubishi uishie hapa. Neno la Mungu halihitaji kubishaniwa. Labda Roho wa Mungu akuguse tofauti maana hata niongeeje bado utaona maandishi ya kitabu na sio Neno la Mungu lililo hai.
 

Na andiko linaloonyesha Hajiri alifanywa mke wa Ibrahim kwa kulala naye ni moja


Tena ànayesimulia hapo Ni Musa.

Mungu anamtambua Hajiri kama Nani?,
Biblia inaonyesha mara kadhaa Mungu alimtaja Hajiri kama Kijakazi kwa nini wewe umwite Mke?

Msimuliaji ambaye ni Musa ukisoma hiyo simulizi anavyosimulia haionyeshi kama hajiri alikuwa mke ila Sarah alimuamuru alale na Ibrahim kama mke ili wapate uzao.

Kupata mbegu au uzao hakumfanyi mtu awe mke au mume. Tukio hilo limejitokeza mara kadhaa kwenye biblia
Hata kwa vijakazi wa Yakobo ilikuwa hivyo.
Na biblia haiwataji kama Wake wa Yakobo.

Kuna kisa kingine cha yule aliyeambiwa amuingilie mke wa kakaake ili apate uzao. Baada ya kaka yake kufa. Akamwagia nje.
Haikumaanisha kitendo hicho ni kuoa.
 
Lakini pia unapozungumzia baraka,... mbona inaonyesha Ismail na Isihaka wote wamepewa baraka nyingi tu... hii imekaaje
Ismael amepewa Baraka na Mungu lakini hakupewa zikapitia kwa Baba yake. Isaka amepewa Baraka na Mungu lakini zimepitia kwanza kwa Mama na Baba yake, hakupewa yeye kama yeye. Ndo maana tunasema Baraka ya Ismael ni kama agano la Mlima Horebu lakini Baraka za Isaka ni za Mlima Sayuni.
Kuna tofauti ya wewe kurithi Baraka za baba yako na wewe kupewa Baraka zako. Na pia warithi hawawi wengi na ndio maana hata Mzee akifa mnachagua kiongozi wa familia. Kuna vitu kwenye ulimwengu huu havikaliwi na watu wawili bali mtu mmoja.
 
Wewe ni Maalim eitha kwa siri au unajidhihirisha. Kwani ukweli ushaujua. Niweke sawa. Mungu wa wakristo ni yesu. Si yule Mungu wa Ibrahim.

Na Mungu wa waislam ni yule Mungu wa yesu. Eloi au Allah

Kwa hiyo rekebisha kwanza utangulizi kabla ya kujenga msingi huo kwenye mada.

Kwani ukianza kwa makosa utaishia kupata majibu yenye makosa
 
Ndo maana nasema aliyetakiwa kuchinjwa ni wa ahadi na sio wa mwili. Ndio ni mke lakini walipokorofishana na mke wa ndoa bado alimfukuza. Kwa utajiri aliokua nao bado alimpa chakula kidogo sana Cha njiani. Kuna swali hapo la ukiwa wa hiyo ndoa.
 
Lea Hakuwa Mke wa Yakobo hahahah🤣🤣 ndo maana Watoto wa Leah hawakurithi kitu..
Nimekuibia siri hiyo
Lea alikaa kwenye kiti Cha mke upande wa Rohoni. Lawi mzaliwa wake ndio alikua badala ya mzaliwa wa kwanza wa Israel mbele za Mungu. Yuda mzaliwa wake wa nne ndio aliyepewa kiti Cha ukombozi wa Dunia. Kwa jinsi ya mwili hakuwa mke lakini usiku ule alipopewa Yakobo akaingia kwake walifunga agano la ndoa kwenye ulimwengu wa Roho. Yakobo alilipa mahari, alimkuta mke ni bikra lakini siye aliyempenda.
Ilibidi atumike miaka mingine 7 ili apate alichokipenda. Na bado Yusuphu baada ya kupewa haki ya uzaliwa wa kwanza bado Taifa lake lilikuja kuparanganyika. Wale wayahudi waliopo Leo Wana tafuta asili yako kutoka Yuda. Hawaitafuti kutoka Manase, Reubeni au Benjamini. Wanaitafutia Kwa Yuda mzaliwa wa Leah mke halali wa kwanza wa Yakobo ambae hakuwahi kupendwa.
 
Samahani sana kwa Swali Hili Dada angu?
No offence but!...

Unajua kweli Kiarabu na Unafahamu hata Grammar النحو (an-nahw)?

Mwalimu aliyekufundisha alikosa kukufahamisha kitu cha Muhimu sana Kuhusu Tofauti ya Nomino (الأسماء ...(al-asma)) na Kitenzi (الأفعال" (al-afʻāl))..
Kama alikufundisha basi utakuwa Umesahau kidogo..

Aya ya mwanzo aya Ya 102 sura hiyo Ya ass'Affat
Neno liliotumika lilikuwa ni "أَنِّي أَذْبَحُكَ فَانظُرْ. " annī adhbaḥuka fa-unẓur

Umeshindwa kujua Kama Matumizi ya Neno adhbahuka ni Kama kitenzi kuwa Nakuchinja..

Na matumizi ya Neno Dhibh kwenye aya ya 107 ni "Kichinjo" kama Nomino?

وَفَدَيْنَاهُ بِذِبْحٍ عَظِيمٍ

"Wa fadaynāhu bi-dhbḥin ʿaẓīm."

Umenisikitishi kutokujua Kinachotamkwa hapo Ni kuwa Tukampa Kichinjo (Kichinjwacho) Kitukufu..

Kwa hiyo kwa maana yako Mungu ndyo alitahiri wa kina Ibraham?😅

Nisamehe kusema hivi ila unahitaji kusoma tena Lughatul arabiya..

Hapo Neno hilo baada ya kuwekewa Kasri limechange kutoka kuwa Kuchinja kuwa Kichinjo ambayo ni nomino..

Sasa Naomba niazime Macho unifatilie Kwa aya zingine Neno hilo hilo lilipotumika likiwa na maana Sawa ya Kuchinja..
Tusome wote Suratul Baqarah aya ya 71..


قَالَ إِنَّهُۥ يَقُولُ إِنَّهَا بَقَرَةٌۭ لَّا ذَلُولٌۭ تُثِيرُ ٱلْأَرْضَ وَلَا تَسْقِى ٱلْحَرْثَ مُسَلَّمَةٌۭ لَّا" شِيَةَ فِيهَا ۚ قَالُوا۟ ٱلْـَٰٔنَ جِئْتَ بِٱلْحَقِّ ۚ فَذَبَحُوهَا وَمَا كَادُوا۟ يَفْعَلُونَ

inasomeka namna Hii kwa wale wanaotaka kufatilia Mjadala..

"Qala innahu yaquulu innaha baqaratun la dhaluulun tuthiiru alardha wala tasqee alhartha musallamatun la shiyata fiiha qaloo alana jita bialhaqqi fadhabahooha wama kaduu yafAAluuna"

Nikianza na aya Hii ambayo Tafsiri yake ni kwamba..

"Akasema: Yeye anasema: Kuwa huyo ni ng'ombe asiye tiwa kazini kulima ardhi wala kumwagia maji mimea, mzima, hana baka. Wakasema: Sasa umeleta haki. Basi wakamchinja, na walikaribia kuwa wasifanye hayo."
nakupa na Aya ya ziada unaweza ukapitia Pia Suratul Baqara aya ya 67 pia..

Turudi sasa..
Kwenye Aya hiyo Ya Suratul Baqara nafikiri Unakumbuka Kuwa Mwenyzi Mungu aliwaamba Wana wa Israel khusu Kuchinja Ng'ombe na Musa akawa anawaambia Soma kuanzia Aya ya 67...

Sasa Unataka Kuniambia Mungu aliamrisha Kutahiri Ng'ombe 🤣🤣🤣

Na wacha hiyo Tusome neno lililotumika hapo kwenye 71 ni fadhabahooha..


hiyo dhahiri kwamba aliyechinjwa Hapo ni Ngombe Jike sasa Swali Je Ngombe Jike kwanini Walimtahiri ikiwa Wewe Adhabh ni kutahiri..
Walikata nini kwa Ng'ombe Jike 🤣🤣

Dada Yangu Faiza unatakiwa usome..
Na ukubali si kila kitu utajua
 
SO you Declare That bible is Contradictory Documents
 
Mkuu Hicho kiti cha rohoni nani Alikiweka??
Na kumbuka Ruben alikuwa Mzaliwa wa Kwanza wa Lea mpaka alipopokonywa..

Kingine Yuda Alifanya madudu na Tamari mkwewe umesahau??
 
Oya hivi vyote umesoma plus medicine?..uko poa Sana,itakua wazitumia vizuri saa 24
 


Hii ndio Safari ya Ibrahim kulingana na Jews tradition.

Kutoka Yerusalem hadi Mecca ni km 1400 sasa humu ndani kuna mtu amesema Ibrahim alimpeleka Ishmael na Hagar Mecca alafu akarudi kwa Sarah, alafu akawapa tende tu😂😂😂😂😂😂

Ukiangalia kwa makini sana Safari Ibrahim kutoka Ur hadi kaanani alipita sehemu ambazo ni Habitable yaani kuna mito na si jangwa sana, Ila Ibrahim wa Waislam alitembea na kulanda landa Jangwani KM 2800 hakuna maji wala nini.

Waislam walikataa kabisa kuunganisha logic na elimu Dunia na Quran
 
Mkuu Hicho kiti cha rohoni nani Alikiweka??
Na kumbuka Ruben alikuwa Mzaliwa wa Kwanza wa Lea mpaka alipopokonywa..

Kingine Yuda Alifanya madudu na Tamari mkwewe umesahau??
Mungu siku ameumba vinavyoonekana aliumba na visivyoonekana. Kwenye order of things aliweka viti vyenye mamlaka mbalimbali. Ushawahi kujiuliza Kwa Nini adui alipoasi alitaka kuweka kiti chake juu ya kiti cha Mungu kilichopo upande wa kaskazini wa bustani ya Edeni ya Mbinguni?
Kwa Nini asitake tu kumtoa Mungu alikitaka na Kiti alichokua amekalia Mungu? Nafasi ni viti. Viti huwa vinatoa maelekezo vinataka Nini.
Mungu alitumia dhambi za wateule wake kuonesha yeye peke yake ndio mkamilifu.
Adam alitenda kosa la kutokutii, Ibrahim na Sara walikosa subira, Yakobo aliiba haki ya uzaliwa wa kwanza. Yuda alilala na mke wa mwanae tena kama kahaba, Musa alikua na kuona hasira, Daudi alikua mwasherati kama sio mzinzi, Solomon aliabudu miungu mingine. Wote hao Mungu aliwatumia ili kuonesha yeye anaweza kutumia yeyote Kwa kazi yake.
Bado kwenye ulimwengu usioonekana Leah alipendelewa. Kwa kutopendwa na Mume wake Mungu alilifungua tumbo lake. Alizaa Wana saba wanaojulikana. Haki ya Baraka alivyopewa Ibrahim ya kuwa Baba wa Mataifa ilitimia kupitia Leah, mzaliwa wa tumbo lake alipewa kiti Cha Enzi Cha kukaa mbele za Mungu milele kama mbalamwezi. Pia alipewa ahadi ya kutokukosekana mtu wa kukikalia hicho kiti milele.
Yesu utambulisho wake rasmi ni ," Simba wa kabila la Yuda, Mwanakondoo wa Mungu aondoaye dhambi za ulimwengu, shila la Yesse, mwana wa Daudi". Leah bado alikua na mamlaka kwenye ulimwengu ule usioonekana.
Yusuphu ni mkombozi wa Taifa ila bado usitawi wa Taifa ulimtegemea Yuda na uzao wake. Kati ya makabila mawili ambayo hayakumwasi Mungu baada ya kufanya scouting ya nchi Takatifu Kuna Caleb mwana wa Yefune wa kabila la Yuda. Yoshua alikua anaambatana na Musa Kwa hiyo aliuona Utukufu wa Mungu Kwa tofauti na hao wengine.
Baraka ya uzaliwa wa kwanza alipewa mwana wa Leah. Bado huoni mahindi ni yeye?
 
SO you Declare That bible is Contradictory Documents

Hiyo ni simulizi.
Kuna msimuliaji ambaye ni Musa alafu kuna dialogue ya Wahusika humo kwenye simulizi.

Kwa hiyo Quotation unapoitoa hasa inayohusu simulizi lazima ujue nani anayezungumza.
Wakristo wengi katika jambo hili wanachanganya madesa.

Kuna sehemu Munga akasema
Kuna sehemu Ibrahim akasema au Sarah akasema,
Alafu kuna sehemu ànayesimulia ni msimulizi.

Ndio Kilekile nawaambia Watu kuhusu Injili, Zaburi na Torati na vitabu vya Hadithi.
Sio kila neno kwenye Biblia ni amri au sheria ya Mungu.

Ukisoma biblia na sio tuu biblia bali kitabu chochote lazima yapo mambo utazingatia íli usijeleta tafrani.

Mfano ni hiyo ndoto ya Ibrahim ya kumtoa Mwanaye kafara iliyopo kwenye Quran. Hiyo ni ndoto na sio tukio la kweli.

Au Yesu anapotoa mfano alafu kuna Watu wanaochukua ule mfano kama tukio la kweli ni dalili ya kutozingatia kanuni za usomaji
 
Kwenye Quran Ibrahim aliota anamtoa kafara ismail alafu kesho yake akamuuliza amtoe asimtoe 😂😂😂😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…