Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?


Mafunzo ya Paulo yalileta mzozano na ubishi mkubwa tangu pale mwanzo katika historia ya Kanisa baina ya kikundi chake cha Wakristo waliomfuata kutoka upagani, na wale Wakristo wa asili ya Kiyahudi.

Wao walipinga moja kwa moja ile shauri ya kwenda kupelekewa mafunzo ya Ukristo mataifa waliokuwa hawakutahiriwa, wala hawaikubali sharia ya Taurati. Baadhi ya wanafunzi wa Yesu walikuwa hawakubali hata kula nao wale "wasiotahiriwa".

Wao walikuwa wanajua vyema kuwa Yesu aliwakataza wasiende kuwahubiria mataifa mengine isipokuwa Mayahudi tu, kwani ni wao ndio walikuwa wanaamini Mungu Mmoja na wao ndio wakiifuata sharia ya Mungu.

Mwishowe ulifanywa mkutano na yakawapo baadhi ya masikilizano kuwa yafaa kuhubiriwa Ukristo kwa mataifa yasiokuwa ya Kiyahudi, na wao wasilazimishwe kubeba mizigo mizito katika dini kama vile wenye asli ya Kiyahudi.

Walitumwa Paulo na Barnaba kuwaendea hao mataifa, nao ni Wazungu wa Kirumi na Kigiriki, na wakachukua barua iliomalizikia maneno haya muhimu:

Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa na uasherati. Mkijizuia na hayo mtafanya vema. Wasalamu.

Matendo 15.28-29

Nyama zilizosongolewa, yaani nyama za kunyonga, zisiochinjwa. Yazingatieni haya si maamrisho ya Yesu, lakini ni masikilizano baina akina Paulo na wanafunzi wake Yesu, (kwa ridhaa ya Roho Mtakatifu) baada ya kuwa Yesu mwenyewe hayupo tena. Ikiwa hayo ndiyo waliokubaliana ilikuwaje Paulo tena kuwaandikia Wakorintho:

"Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni bila ya kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri" (?)

Lakini Paulo ni Paulo.

Mtakatifu Paulo anadai kuwa yeye aliteuliwa mahsusi kuwa ni mtume wa Yesu katika ufunuo (Wahyi), na kuwa bado yeye anaendelea kupata amri moja kwa moja kutokana na mwenyewe Bwana Yesu, ijapokuwa amri hizo na mafunzo hayo yanapingana kabisa na yale waliyoyapata wale wanafunzi wake Yesu waliokuwa naye mwenyewe alipokuwa hai.

Yeye Paulo hakupata kuonana na Yesu, bali yeye alikuwa ni mpinzani mkubwa wa Ukristo na akawa ni sababu ya kuteswa na kuuwawa Wakristo kadhaa wa kadhaa, mmoja wao ni Mtakatifu Stefano, shahidi wa mwanzo katika Wakristo.

Paulo alikuwa na asli ya Kiyahudi, na dini yake rasmi ilikuwa ya Kiyahudi.

Kwa kuwa alizaliwa nje ya Palastina katika mamlaka ya Kirumi alikuwa na uraia kamili wa Kirumi, na huko alipata fursa ya kusoma ilimu na falsafa za Kiyunani.

Mazingara yake yote ya Kigiriki na Kirumi yalikuwa ya kikafiri, kipagani.

Kwani Magiriki na Warumi walikuwa washirikina wenye kuamini chungu ya miungu, kama ilivyokuwa ada ya karibu mataifa yote ya wakati ule isipokuwa Mayahudi.

Yalipozuka mafunzo ya Yesu Kristo, ambayo kwa asli yake hayakuwa ila ni kuendeleza ile ile imani ya Kiyahudi ya Mungu Mmoja na kufuata sharia ya Taurati na kuongeza uchamngu, na ikawa mafunzo hayo yanaendelea juu ya kupingwa,

Paulo aliona anaweza kuipa nguvu hiyo dini au kwa hakika madhehebu mpya kwa kuwatia wale Warumi na Magiriki kwa kuchanganya imani zao na falsafa zao pamoja na imani ya Kiyahudi. Mayahudi wanaamini Mungu Mmoja, ndio.
Ukristo unaamini Mungu Mmoja.

Magiriki na Warumi wanaamini miungu mingi, si chini ya watatu, ndio na Ukristo nao unaamini hivyo.

Jee, si pana mgongano hapo?

La, katika Ukristo imani ni ya Mungu Mmoja katika Utatu Mtakatifu: Mungu Mmoja, mwenye nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.

Mapagani wa Kigiriki na Kirumi wakiamini mungu aliyekufa, akafufuka na akapaa mbinguni.

Hilo si kitu wanaweza kuendelea na imani hiyo katika Ukristo.

Wazungu magovi hawataki kutahiriwa.

Hapana kitu, kutahiriwa si kitu wala kutotahiriwa.

Hoja ipatikane tahara ya roho.

Wazungu wamezoea kula kila kitu, nguruwe, damu, kilichochinjwa na kisichochinjwa. Hilo si tatizo, mtaendelea vivyo hivyo, kwani dhambi ni kitokacho mdomoni, sio kiingiacho.

Kuleni kila kiuzwacho sokoni.

Hapana halali wala haramu.

Huo ndio Ukristo mpya wa Paulo, na hiyo ndio Thiolojia yake ambayo, inasikitisha Wakristo wameifuata, wakayaacha mafunzo mepesi na yaliyonyooka ya mwenyewe Yesu Kristo.
 
Thanks for this
P
 
uki follows the links unakutana na ujumbe huu
" Kumradhi! Kuna changamoto kidogo"
"You do not have permission to view this page or perform this action".

P
 


Tatizo kubwa la Quran na history yake it is very hard to prove authentic ya hizo Hadithi historically na pia watafsiri wa Quran they tried so much kufanya Biblia ambayo was already there 2000 years before Quran ionekane ni uongo at the end they have to go back to Bible kupata certain references au parallel to their teachings.

Mfano Jina la Yesu, Waislam wamehangaika sana kutafsiri neno Iēso and at the end they Used Isa na wakatunga mtu mpya kabisa

Jesus (/ˈdʒiːzəs/) is a masculine given name derived from Iēsous (Ἰησοῦς; Iesus in Classical Latin)
 
Hayo unayosema hayana ukweli wowote, kama u mkweli weka nukuu japo ya Qur'an ilipoingilia kisa chochote cha Biblia. Usifate watafsiri au washereheshaji kwani una uhakika gani kuwa wote ni Waislam?

Unataka kufananisha mkusanyiko wa vitabu vilivyotiwa mikono ya watu na kitabu kimoja kisochokuwa na mfano wake diuniani?

Isome Qur'an kijana ipo kwa ajili yako pia.

Mfano mzuri ni mimi nakwambia hakuna hata jina Sarah kwenye Qur'an, prove me wrong, uweke nukuu ya Qur'an yenye Sarah.
 
Unapoongea kuhusu biblia unakusudia biblia ipi ? KJV, QJV, RSV, AV Mormon Bible au maelfu ya Biblia tofauti?
 
King James or anything ni translation. But all of the Bibles are older than Quran

Mimi sijakuuliza ipi older , nilikuuliza hiyo Quran inachukuwa reference kutoka biblia ipi ??

ya Mormon , KJV, QJV, AV , Mormon Bible au maelfu ya biblia tofauti ??

Kwa kukuongezea kama unaelewa kiengereza msikilize huyu anayefantya kazi sehemu ya kuhifadhia hizo bible za zamani anasema nini



Your browser is not able to display this video.
 
Kinacho ni shangaza ni kuona watoto 12 wa Yakobo(Israel)wametokana na wanawake wanne na sheria hizo hizo za kiyahudi zinawatukuza.Ila pia kumbuka Ibrahim aliishi miaka mingi sana kabla ya kuwepo uyahudi.
 
Kinacho ni shangaza ni kuona watoto 12 wa Yakobo(Israel)wametokana na wanawake wanne na sheria hizo hizo za kiyahudi zinawatukuza.Ila pia kumbuka Ibrahim aliishi miaka mingi sana kabla ya kuwepo uyahudi.
 
Kinacho ni shangaza ni kuona watoto 12 wa Yakobo(Israel)wametokana na wanawake wanne na sheria hizo hizo za kiyahudi(kiebrania)zinawatukuza.Ila pia kumbuka Ibrahim aliishi miaka mingi sana kabla ya kuwepo kwa sheria za kiyahudi.
 
Ujuwe tu kuwa Quran ina miaka 1400 wakati Bibilia ina miaka zaidi ya 2000. Hapo utagundua ni nani kakopi kwa nani?

Halafu kuna watu wanadanganywa eti Mtume wao aliteremshiwa kitabu. Uwongo mtupu
Biblia ina edition ngapi??? Mpaka sasa Qur'an kuna edition ngapi mpaka sasa???
 

Ili swali ajibu Che mittoga
 
Hekima ya Mungu haichunguziki. Hata upumbavu wake ni mwema kuliko hekima yetu binadamu. Tumaini Leo, kesho tutajua zaidi kama yeye atujuliavyo zaidi. Hiyo ni ahadi tuliyopewa.
 
Asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…