Jagina
JF-Expert Member
- Jan 29, 2019
- 8,428
- 4,022
Yesu anathibitisha umuhimu mkubwa wa kutekeleza mapenzi ya Mungu kama yalivyorekodiwa kwenye torati na manabii (yaani, vitabu 5 vya Agano la Kale na sehemu zingine za Maandiko).
Biblia inasema Yesu hakuja kuitangua torati bali kuitimiliza—ikiwa na maana kwamba aliyapa Maandiko maana yake kamili zaidi.
Alikuja kuonesha namna bora ya kufuata mapenzi ya Baba Yake.
Katika Mathayo 5, kwa mfano, Yesu anabainisha vipengele kadhaa vinavyoonesha undani hasa wa torati. Anasema, kumchukia mtu ni sawa na uuaji (Mat 5:21-26), kutamani ni kuzini (Mat 5:27-30; Mat 19), talaka haramu ni zinaa (Mat 19:8-9); anawasisitiza wanafunzi Wake kusema ukweli, kuepuka kisasi na kuwapenda maadui wao (Mat 5:33-48).
Katika kila mmoja ya mafundisho hayo hapo juu, Yesu anasema mmesikia kwamba imenenwa au mmesikia watu wa kale walivyoambiwa; kisha anasema bali Mimi nawaambieni.
Hii ndiyo kusema kwamba Kristu alionesha undani wa torati, namna ilivyoeleweka awali na namna anavyoifafanua sasa.
Kwa waandishi na Mafarisayo, Marabi na walimu wa sheria, ni bayana Yesu alikuwa ameivunja torati.
Ndiyo maana walimchukia sana na kujaribu mara nyingi kumpiga mawe.
Sababu ya mwitikio huo mkali dhidi ya Yesu ni kwa vile viongozi wa dini walikuwa makini sana katika kufuata sheria zote.
Walikuwa na masharti magumu na yenye uzingativu mkubwa katika masuala ya dini yao.
Jibu pekee la Yesu ambalo lingeweza kuwafikirisha viongozi hao wa dini waliokuwa na uhakika wa mwenendo wao katika torati ni pale alipowaambia, nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, Nataka rehema, wala si kujitoa mhanga (Mathayo 9:13)!
Yesu alikuwa akiwatafakarisha waichunguze mioyo yao zaidi kuliko kuishia tu kutazama matendo yao ya nje na kujisifu kwa namna walivyotekeleza vipengele vya dini.
Hii hutuambia kwamba Yesu alidai kwao wawe na mwenendo wa kina zaidi kuliko kushika vipengele ama masharti tu ya nje.
Alienda mbali zaidi hadi kwenye kiini ama msingi kabisa wa nia ya moyo. Nia, mawazo, matendo, vyote vinahusika katika kutekeleza mapenzi ya Mungu.
Kwa mujibu wa Kristo, kinachofanyika moyoni ndicho kinachoibua matendo ya nje. Ndiyo maana alisema chuki ni sawa na uuaji, kutamani ni sawa na kutenda zinaa, nk.
Matendo yao ya nje yalikuwa na maana tu pale ambapo yangeambatana na utauwa au tohara ya moyo.
Hayo imewapasa kuyafanya, wala yale mengine msiyaache (Mathayo 23:23)! Haki yenu isipozidi hiyo haki ya Mafarisayo!
Yesu aliwafundisha mambo ambayo kwao yalionekana kuwa mageni na yanayopingana na torati, kadiri uelewa wao ulivyohusika.
Hata hivyo, mafundisho Yake yalipatana kikamilifu na mafunuo ya Mungu.
Je, Paulo alipingana na mafundisho ya Kristu?
Ni katika mantiki kama hiyo ya Yesu ndipo tunaweza kumwelewa vyema Mtume Paulo.
Alifundisha mambo ambayo watu wasio makini hudhani aliipinga torati au aliibatilisha sheria ya Mungu, kama ambavyo Yesu alidhaniwa anafundisha kinyume na torati.
Katika muktadha huo, tahadhari ya Petro ni muhimu sana:
^Katika nyaraka hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuelewa nayo; na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wayapotoavyo na maandiko mengine, kwa uvunjifu wao wenyewe.^ (2 Petro 3:16).
Kabla ya kuangalia baadhi ya mafundisho ya Paulo, hebu tuone yeye alikuwa ni mtu wa namna gani kabla hajakutana na Yesu na kuitwa kuwa mtume.
Wafilipi 3:3-4
^3 Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.
4 Walakini mimi ningeweza kuutumainia mwili. Mtu yeyote akijiona kuwa anayo sababu ya kuutumainia mwili, mimi zaidi.
5 Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli, wa kabila ya Benjamini, Mwebrania wa Waebrania, kwa habari ya kuishika torati, ni Farisayo, 6 kwa habari ya juhudi, mwenye kuliudhi Kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na hatia.
7 Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.^
Mtume Paulo alikuwa Farisayo wa Mafarisayo! Paulo alijua namna ya kuishika sheria au torati, lakini kama Yesu asemavyo, lazima haki yake izidi ile ya waandishi na Mafarisayo ili aurithi ufalme.
Si ajabu Paulo anasema, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili ya uzuri usio na kiasi wa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu; ambaye kwa ajili yake nimepata hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nimpate Kristo; tena nionekane katika Yeye, nisiwe na haki yangu mwenyewe ipatikanayo kwa sheria, bali ile ipatikanayo kwa imani iliyo katika Kristo, haki ile itokayo kwa Mungu, kwa imani (Wafilipi 3:8, 9).
ESV 1 Cor. 10:25
Eat whatever is sold in the meat market without raising any question on the ground of conscience.
Muktadha wa 1Kor 10:14-33 ni namna ya kuikabili ibada ya kipagani hasa kuhusu vyakula au nyama zilizotolewa sadaka kwa sanamu.
Hivi ni vyakula vya matambiko kwa miungu, ibada ya sanamu na ushirikina.
Paulo anaeleza namna 4 za kukabiliana na changamoto hiyo:
a) Ni kosa kwa mfuasi wa Kristu kwenda kwenye mahekalu ya wapagani na sehemu zao za matambiko ili kushiriki vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu. Kufanya hivyo ni sawa na kujihusisha na ushirikina na ibada ya mashetani (1Kor 10:18-21).
b) Iwapo chakula kinauzwa sokoni ama sehemu za umma, ni halali kula bila kuuliza maswali ili kujua iwapo au la kilitokana na matambiko (1Kor 10:25-26).
Paulo anasema si haramu kula chakula kilichonunuliwa mahali sahihi ambapo hakuna matambiko wala ibada za kipagani na iwapo mtu husika hafahamu kwamba chakula hicho kilitolewa sadaka kwa sanamu (kilitambikiwa).
c) Kufuatia mwaliko wa mtu asiyeamini—ni halali kula chakula chake bila kuuliza iwapo au la kilitambikiwa (1Kor 10:27).
d) Hupaswi kula chakula hicho iwapo umeambiwa kilitambikiwa. Paulo anabainisha sababu husika kwamba hilo hufanyika kwa faida ya mtu huyo asiyeamini (1Kor 10:27-28, 32-33).
Hitimisho: Paulo hazungumzii kula tu kitu chochote bila kubagua vyakula najisi na visivyo najisi, bali anaongelea vyakula—vitu ambavyo vimeainishwa kwamba vinapaswa kuliwa kwa mujibu wa Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14.
Kama ilivyoelezwa awali, tatizo hapa lilikuwa vyakula vilivyotolewa sadaka kwa sanamu au kufanyiwa matambiko.
Kamwe, tatizo haukuwa mgogoro wa vyakula gani viliwe na vipi visiliwe. Ni vyema kuzingatia muktadha ili kuepuka upotoshaji.
^Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu,^ ndivyo Mtume Paulo anavyohitimisha kipengele hiki.
Paulo anafundisha vyema kwamba mtu anayefanya tohara kwa kusudi tu la kuhesabiwa haki, huyo ni sawasawa amejifunga nira ya utumwa, ametengwa na Kristu, ameanguka mbali na neema!
Ni wazi kwamba Paulo hajivunii tohara yake kama sifa ya kumpatia haki kwa Mungu.
Anadai tohara ya kweli ni kumwabudu Mungu kwa Roho na kujivunia Kristu (Wafilipi 3:3, 4).
Hivyo ndivyo hasa alivyofundisha Bwana aliposema lazima haki ya wanafunzi Wake na waumini wa kweli izidi ile ya waandishi na Mafarisayo, ambao japo walikuwa wamefanya tohara ya mwili, mioyo yao haikuwa imefanyiwa tohara—hawakuwa na uongofu halisi wala badiliko kamili la moyo.
Ni wazi Paulo anaonesha tofauti kati ya tohara, ambayo si sharti lenye mamlaka tena katika Agano Jipya, na sheria zingine za Mungu ambazo zenyewe hudumu milele.
Anasema, ^Kwa maana kutahiriwa kwafaa kama ukiwa mtendaji wa sheria, lakini ukiwa mvunjaji wa sheria kutahiriwa kwako kumekuwa kutokutahiriwa.
Basi ikiwa yeye asiyetahiriwa huyashika maagizo ya torati, hivi kutokutahiriwa kwake hakutahesabiwa kuwa kutahiriwa?^ (Warumi 2:25, 26).
Izingatiwe hapa kwamba kuhesabiwa haki, ambako hufanyika kwa neema kupitia imani katika Kristu (Waefeso 2:8-10) ni tofauti na mchakato wa utakaso, ambao wenyewe hufanyika kwa kuishi kwa hiyo neema—yaani, kuzitii amri.
Ndiyo maana Paulo anasema linapokuja suala la kuhesabiwa haki, basi imani yetu katika neema ya Kristu iokoayo ndiyo hasa inahusika, kisha matendo ya utii wa sheria hujaa kama matokeo ya kuishi kwa imani hiyo.
Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. (Warumi 3:28).
Tunatii sheria kwa sababu tumeokolewa kwa neema kwa njia ya imani; hatuitii ili tuokolewe.
Yakobo anafafanua jambo hili zaidi anaposema: imani bila matendo imekufa (Yakobo 2:17).
Imani yetu katika Kristu itaoneshwa kwa matendo ya kuitii sheria, yaani kuyafanya mapenzi ya Mungu.
Je, Paulo anasema sheria haina mamlaka tena kwa sababu ya neema ya Kristu? Hapana.
Sheria ni takatifu, ya haki na njema. Sheria ni kama kioo kinachotusaidia kuitambua dhambi (Warumi 7:7, 12); bila sheria, mdhambi hawezi kuona kasoro yake na hivyo hawezi kumhitaji Kristu na neema Yake.
Kamwe Paulo haioni torati kuwa ni laana!!! Paulo anasema Mkristu muumini hahukumiwi na sheria kwa sababu kupitia Kristu hatekelezi tena tamaa za dhambi ziletazo mauti (Warumi 7:5).
Paulo anasema nini? Kwa upande mmoja anaonekana kuitetea torati, kwa upande mwingine anaonekana kuibatilisha.
Ndiyo maana Mtume Petro akatupatia onyo kuhusu kuwa makini tunapojaribu kuuelewa ujumbe thabiti ambao Paulo anauwasilisha katika kanisa la Kristu.
Je, Mkristu analazimika kutoa dhabihu ya wanyama, wanakondoo, mbuzi, nk. madhabahuni kama zamani?
Vipi kuhusu sikukuu au miandamo ya mwezi, sherehe zingine walizoagizwa Waisraeli wazidhimishe?
Habari gani juu ya makuhani na wakuu wa makuhani katika huduma za hekaluni?
Haya mambo yalikuwa vielelezo ama ishara ya Kristu ambaye angekuja na kufa Msalabani.
Alipotamka Imekwisha, pazia la hekalu likachanika vipande viwili juu hata chini, ndiyo kusema kwamba huduma hizo nazo zikafikia utimizo wao.
Paulo anasisitiza: ^Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato; mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.^ (Wakolosai 2).
Mwanadamu anapomwamini na kumpokea Kristu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yake, akaacha maisha yake ya zamani ya anasa za dhambi, anakuwa kiumbe kipya.
Hapo anahesabika kwamba ameifia torati. Na ndiyo mantiki nzima ya kielelezo cha ubatizo wa kuzamishwa kwenye maji mengi kama ishara ya kuamini mauti na ufufuo wa Yesu Kristu (Warumi 6:4).
Mwamini huyo anahesabika ameifia torati kwa sababu torati haiwezi kumhukumu tena mtu aliye milki ya Kristu.
Umiliki wake umehama kutoka kwenye dhambi na kuwa kwa Yesu na Mwokozi wa maisha yake.
Kama ambavyo mwanamke yuko huru na wala hafungwi na sheria ya ndoa baada ya mumewe kufariki (1 Wakorintho 7:1-3), kadhalika Mkristu hahukumiwi na torati anapokuwa kwenye himaya ya wokovu katika Kristu.
^Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda.^ (Warumi 7:4)
Paulo anaendelea kusema kwamba wakati tukiishi nje ya Kristu, tuliiasi torati, tulitenda dhambi na hivyo torati ikatuhukumia kifo (aya ya 5).
Lakini tulipompokea Yesu, tulifunguliwa katika torati. Maana yake ni kwamba torati haituhesabu tena kama waasi bali viumbe wapya katika Kristu.
Anasema, tumeifia hali ile iliyotupinga, yaani utawala wa zamani wa dhambi na mauti juu yetu tukingali waovu.
Baada ya Mtume Paulo kuzungumzia badiliko hilo ambalo limemtokea mdhambi aliyempokea Kristu kuwa Bwana na Mwokozi wake, sasa anazungumzia matokeo husika ama lengo tarajiwa la ^kufunguliwa katika torati^ na ^kuifia hali ile iliyotupinga.^
Anaandika jawabu hilo: ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko. (aya ya 6).
Huku ni kumtumikia Mungu chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, ambaye hutusaidia kuzaa matunda ya Roho (Wagalatia 5:22).
Kabla ya kuhitimisha kwa kufafanua anachomaanisha Paulo anaposema hali ya zamani, ya andiko, ni vyema kukariri kwa mara nyingine tena kuhusu udaima wa sheria, torati au amri za Mungu.
Hizi bado zina mamlaka na wala hazikubatilika msalabani (Mathayo 5:17).
^Basi, hivi twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria.^ (Warumi 3:31).
Ili kuelewa vilivyo maana ya hali ya zamani, ya andiko, hebu tujiulize ni sehemu ipi ya torati ambayo imefikia tamati kwa kifo cha Kristu msalabani?
Bila shaka hayo ni maagizo ya torati yaliyohusu taratibu za kiibada (ceremonial laws) kama vile tohara, kafara au dhabihu za wanyama, sikukuu mbalimbali, miandamo ya mwezi, nk. (Walawi 23).
Mambo haya, ambayo ni hali ya zamani ya andiko, yalilenga wakati ujao kwenye kazi na kafara ya Kristu, nayo yalikoma alipokufa msalabani.
Inavutia kuona kwamba Paulo aliyekuwa akijivunia ufarisayo wake na tohara ya nje tu, sasa baada ya uongofu wake na kuwa kiumbe kipya anamshangilia Bwana Yesu Kristu.
Anasema, 14 Lakini mimi, hasha, nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba wa Bwana wetu Yesu Kristo, ambao kwa huo ulimwengu umesulibishwa kwangu, na mimi kwa ulimwengu.
15 Kwa sababu kutahiriwa si kitu, wala kutokutahiriwa, bali kiumbe kipya. 16 Na wote watakaoenenda kwa kanuni hiyo, amani na iwe kwao na rehema, naam, kwa Israeli wa Mungu.^ (Warumi 6:14-16)
Mafunzo ya Paulo yalileta mzozano na ubishi mkubwa tangu pale mwanzo katika historia ya Kanisa baina ya kikundi chake cha Wakristo waliomfuata kutoka upagani, na wale Wakristo wa asili ya Kiyahudi.
Wao walipinga moja kwa moja ile shauri ya kwenda kupelekewa mafunzo ya Ukristo mataifa waliokuwa hawakutahiriwa, wala hawaikubali sharia ya Taurati. Baadhi ya wanafunzi wa Yesu walikuwa hawakubali hata kula nao wale "wasiotahiriwa".
Wao walikuwa wanajua vyema kuwa Yesu aliwakataza wasiende kuwahubiria mataifa mengine isipokuwa Mayahudi tu, kwani ni wao ndio walikuwa wanaamini Mungu Mmoja na wao ndio wakiifuata sharia ya Mungu.
Mwishowe ulifanywa mkutano na yakawapo baadhi ya masikilizano kuwa yafaa kuhubiriwa Ukristo kwa mataifa yasiokuwa ya Kiyahudi, na wao wasilazimishwe kubeba mizigo mizito katika dini kama vile wenye asli ya Kiyahudi.
Walitumwa Paulo na Barnaba kuwaendea hao mataifa, nao ni Wazungu wa Kirumi na Kigiriki, na wakachukua barua iliomalizikia maneno haya muhimu:
Kwa maana ilimpendeza Roho Mtakatifu na sisi, tusiwatwike mzigo ila hayo yaliyo lazima, yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa na uasherati. Mkijizuia na hayo mtafanya vema. Wasalamu.
Matendo 15.28-29
Nyama zilizosongolewa, yaani nyama za kunyonga, zisiochinjwa. Yazingatieni haya si maamrisho ya Yesu, lakini ni masikilizano baina akina Paulo na wanafunzi wake Yesu, (kwa ridhaa ya Roho Mtakatifu) baada ya kuwa Yesu mwenyewe hayupo tena. Ikiwa hayo ndiyo waliokubaliana ilikuwaje Paulo tena kuwaandikia Wakorintho:
"Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni bila ya kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri" (?)
Lakini Paulo ni Paulo.
Mtakatifu Paulo anadai kuwa yeye aliteuliwa mahsusi kuwa ni mtume wa Yesu katika ufunuo (Wahyi), na kuwa bado yeye anaendelea kupata amri moja kwa moja kutokana na mwenyewe Bwana Yesu, ijapokuwa amri hizo na mafunzo hayo yanapingana kabisa na yale waliyoyapata wale wanafunzi wake Yesu waliokuwa naye mwenyewe alipokuwa hai.
Yeye Paulo hakupata kuonana na Yesu, bali yeye alikuwa ni mpinzani mkubwa wa Ukristo na akawa ni sababu ya kuteswa na kuuwawa Wakristo kadhaa wa kadhaa, mmoja wao ni Mtakatifu Stefano, shahidi wa mwanzo katika Wakristo.
Paulo alikuwa na asli ya Kiyahudi, na dini yake rasmi ilikuwa ya Kiyahudi.
Kwa kuwa alizaliwa nje ya Palastina katika mamlaka ya Kirumi alikuwa na uraia kamili wa Kirumi, na huko alipata fursa ya kusoma ilimu na falsafa za Kiyunani.
Mazingara yake yote ya Kigiriki na Kirumi yalikuwa ya kikafiri, kipagani.
Kwani Magiriki na Warumi walikuwa washirikina wenye kuamini chungu ya miungu, kama ilivyokuwa ada ya karibu mataifa yote ya wakati ule isipokuwa Mayahudi.
Yalipozuka mafunzo ya Yesu Kristo, ambayo kwa asli yake hayakuwa ila ni kuendeleza ile ile imani ya Kiyahudi ya Mungu Mmoja na kufuata sharia ya Taurati na kuongeza uchamngu, na ikawa mafunzo hayo yanaendelea juu ya kupingwa,
Paulo aliona anaweza kuipa nguvu hiyo dini au kwa hakika madhehebu mpya kwa kuwatia wale Warumi na Magiriki kwa kuchanganya imani zao na falsafa zao pamoja na imani ya Kiyahudi. Mayahudi wanaamini Mungu Mmoja, ndio.
Ukristo unaamini Mungu Mmoja.
Magiriki na Warumi wanaamini miungu mingi, si chini ya watatu, ndio na Ukristo nao unaamini hivyo.
Jee, si pana mgongano hapo?
La, katika Ukristo imani ni ya Mungu Mmoja katika Utatu Mtakatifu: Mungu Mmoja, mwenye nafsi tatu, Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.
Mapagani wa Kigiriki na Kirumi wakiamini mungu aliyekufa, akafufuka na akapaa mbinguni.
Hilo si kitu wanaweza kuendelea na imani hiyo katika Ukristo.
Wazungu magovi hawataki kutahiriwa.
Hapana kitu, kutahiriwa si kitu wala kutotahiriwa.
Hoja ipatikane tahara ya roho.
Wazungu wamezoea kula kila kitu, nguruwe, damu, kilichochinjwa na kisichochinjwa. Hilo si tatizo, mtaendelea vivyo hivyo, kwani dhambi ni kitokacho mdomoni, sio kiingiacho.
Kuleni kila kiuzwacho sokoni.
Hapana halali wala haramu.
Huo ndio Ukristo mpya wa Paulo, na hiyo ndio Thiolojia yake ambayo, inasikitisha Wakristo wameifuata, wakayaacha mafunzo mepesi na yaliyonyooka ya mwenyewe Yesu Kristo.