Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

NOTE: ... MWANZO 22:2
Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.

Hapo mbona ipo wazi kabisa kwamba ni Isaka ndiye alitakiwa kutolewa sadaka ya kuchinjwa kuonyesha utii kwa Mungu!.
Hilo jina Isaka hapo limepachikwa Kwa kulazimishwa
Isaka hajawahi kuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim Kwa sababu yeye ni mtoto wa pili

Ila Ishmael ndio aliwahi kuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim

Wakati Isaka hajazaliwa Ishmael ndio alikuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim

Nyinyi wagalatia mmedanganywa sana na Wazungu
 
hakuna kitu kama hicho labda unalazimisha ili ukubaliwe na jamii mkristo ni tofauti na muislamu na hawajawahi kuwa watoto wa baba mmjoja kamwe na haijawahi kuwa na haitakaa iwe na miungu yao ni tofaoti pia wala hailingani maana kila mmoja ameagizwa tofauti hivyo hawawezi kuwa na baba mmoja
Sikulaumu kwasababu wengi hawajui kuwa Wakristo na Waislamu ni watoto wa Baba mmoja Ibrahim, hivyo Mungu wetu pia ni mmoja.
P
 
Waislamu wapo sahihi. Ukitakakujua ukweli ni kufahamu nani alikuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim kwani wakati anataka kumchinja andiko linasema mtptp pekee hii ina maana ilikuwa kabla Ibrahim hajapata mtoto wa pili
 
Ndoa ya Ibrahim hakuwahi kuoa Ndoa za Mitala.
Mke wake alikuwa ni Sarah. Kisha alipokufa akamwoa Ketura.
Ni kweli Ibrahim hakuwa na mitala, ila mke anakuwa huru kumtoa kijakazi wake kwa mumewe ili kumzalisha, huyo kijakazi anageuka suria, ana hadhi ya mke, ila watoto wa suria, wanakuwa ni wa bosi wake, yaani mama mwenye nyumba, hivyo baada ya Sarah kumtoa kijakazi wake, yule kijakazi akageuka suria, mtoto akawa ni wa Sarah, hivyo hakuna ubishi wowote kuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail.
Hajiri hajawahi kuwa Mke wa Ibrahim. Alikuwa ni kijakazi wa Sarah.
Kwa sheria za zamani kijakazi huweza kumzalia Bwana wa Boss wake(Sarah) kama ataruhusiwa.
Hajiri alikuwa suria, ni sawa na mke, kijakazi akiisha geuka suria, hawi kijakazi tena, anakuwa mke mdogo, kazi yake ni kumhudumia baba.
Isaka ndiye anayetambulika kama mtoto wa familia ya Ibrahim na sio Ishmael.
Sii kweli, mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail na aliyekuwa mtoto wa pekee ni Ismail watoto wa wajakazi ni watoto kamili, ushahidi ni watoto 12 wa Yakobo, waliozaa makabila 12 ya Israel, watoto wa lea ni 5, watoto wa Recho ni wawili, watoto 5 ni wa wajakazi wa Lea na Recho
Wahusika wakuu katika kisa cha Ibrahim ni Ibrahim mwenyewe na Sarah kisha kwenye episode zilizofuata wahusika wakuu wakawa Isaka na Raheli.

Ishmael na Hajiri ni wahusika wadogo sana ambao hata ukiwaondoa kwenye simulizi hiyo stori haitapata dosari kubwa. Ni sawa utoe kijiko cha maji kwenye bahari hakuna tofauti itakayoonekana
Yes it's true, Kikristo Ismail is not a big deal, Kiislamu it's a very big deal, Iddi ya kuchinja inatokana na Isamal ambaye ndio uzao wa Uislam.
P
 
Ni kweli Ibrahim hakuwa na mitala, ila mke anakuwa huru kumtoa kijakazi wake kwa mumewe ili kumzalisha, huyo kijakazi anageuka suria, ana hadhi ya mke, ila watoto wa suria, wanakuwa ni wa bosi wake, yaani mama mwenye nyumba, hivyo baada ya Sarah kumtoa kijakazi wake, yule kijakazi akageuka suria, mtoto akawa ni wa Sarah, hivyo hakuna ubishi wowote kuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail.

Hajiri alikuwa suria, ni sawa na mke, kijakazi akiisha geuka suria, hawi kijakazi tena, anakuwa mke mdogo, kazi yake ni kumhudumia baba.

Sii kweli, mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail na aliyekuwa mtoto wa pekee ni Ismail watoto wa wajakazi ni watoto kamili, ushahidi ni watoto 12 wa Yakobo, waliozaa makabila 12 ya Israel, watoto wa lea ni 5, watoto wa Recho ni wawili, watoto 5 ni wa wajakazi wa Lea na Recho
Yes it's true, Kikristo Ismail is not a big deal, Kiislamu it's a very big deal, Iddi ya kuchinja inatokana na Isamal ambaye ndio uzao wa Uislam.
P
kwa maelezo haya Brother Robert Heriel Mtibeli hawezi kuwa na comeback 🤝🏼
 
Wanabodi,
Leo ni sikukuu ya Eid El Haji, Iddi ya Kuchinja.

Leo ni siku ya Sikukuu ya Idd El Haj, ni iddi ya kuchinja, asubuhi nilikuwa naangalia matangazo ya mubashara ya Baraza la Iddi kupitia TBC, kutoka Msikiti wa Mfalme Mohammed VI wa Morroco, Bwakwata, Kinondoni jijini Dar es Salaam, kumbe Msikiti Mkuu wa Bakwata, sasa umebadilishwa jina!, na kupewa jina la Mfalme wa Morroco!.

Mgeni rasmi kwenye Baraza la Iddi ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, ambaye ameandamana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ambaye amesilimishwa na kupewa jina la Aboubakar Chalamila!, na mawaziri akiwemo Waziri Mhe. Mohamed Mchengerwa. Baadhi ya watu maarufu niliowaona ni pamoja na Alhaj Sheikh Ali Nguruko, Alhaj Chande, Idda Azan, Shaweji Abdalah, Salum Mwalimu, Juma Simba Gadafi, Salum Abladaha "TRY Again", Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Mruma, Kadhi wa Dar es Salaam, Shamin Khan, mwenyekiti wa JUAKITA, pia kulikuwa na mabalozi wa Balozi wa Moroko, na wa Comoro.

Katika salam zake, Sheikh Aboubakar Chalamila alisema utulivu wa jiji la Dar es Salaam, unawategemea sana viongozi wa Dini.

Salaam za Waislamu, zimetolewa na Alhaj Sheikh Nuru Mruma, Katibu Mkuu wa Bakwata ambaye amewasisitiza Waislamu kudumisha amani na kuilinda amani. Wazazi watakiwa kulea watoto wao kwa tabia njema, kujenga taifa la kizazi cha watu wema ambao hawatapokea rushwa wala kufanya ufisadi.

Amesema kupanda miti na utunzaji wa mazingira ni ibada muhimu kwa Waismamu wote.

Pia amewataka Waislamu kujitokeza kwa wingi, kujiandikisha kwenye uboreshaji daftari la kudumu la wapiga kura.
na wametakiwa kujitokeza kwa wingi kutumia haki yao ya kidemokrasia kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.

Salaam za Mufti, zimetolewa na Kaimu Mufti Sheikh Ali Muhidin Mporogore, Mjumbe wa Baraza la Maulamaa wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania, Bwakwata. Aamezungumzia Watanzania tutafakari, sadaka ya kuchinja siku ya Iddi El Haj, ni iddi ya kuchinja. Zamani ilikuwa sio kuchinja tuu wanyama, bali walichinja hata binadamu ana akatolea mfano Sadaka ya Nabii Ibrahim kutaka kumtoa mwanae Ismail, kwa sadaka ya kuchinja.

Hakuna ubishi kuhusu Wakristo na Waislamu, kuwa ni watoto wa Baba mmoja, Nabii Ibrahim hivyo huu ni uthibitisho wa Mungu wa Wakristo na Waislamu ni Mungu Mmoja, ila kuna watu wanafundishwa ukweli na kuna watu wanadanganywa!.

Hakuna ubishi kuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail aliyezaa na mjakazi wa Kimisri, Hagir, na Isaka ni mtoto wa pili wa Ibrahim, aliyemzaa na mkewe Sarah.

Hakuna ubishi Ibrahim alitaka kumtoa mtoto wake Sadaka ya kuchinja.

Waislamu na Kitabu chao Kitukufu cha Quran Tukufu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Ismail.
Wakristo na Kitabu chao Kitakatifu cha Biblia Takatifu, kinamtaja mtoto huyo aliyetaka kutolewa sadaka ya kuchinja ni Isaka.

Jee ukweli halisi ni upi?.
Hii maana yake, kuna watu wanadanganywa, haiwezi huku awe huyu na kule awe yule!.
Umuhimu wa kuujua ukweli huu, unakupa fursa ya kujua ukweli ni upi, hivyo ufuate mafundisho yapi ndio ya kweli?..

Nawatakia Waislamu wote,
Iddi Mubarak.

Paskal
jibu ni jepesi sana. Ukristo umekuwepo miaka karibia 500 ndio uislam ukaja. na Uyahudi umekuwepo miaka kama 3000 ndio uislam ukaja. maana yake, miaka 3000 historia iliwekwa kwa Ibrahim kumtoa Isaka mtoto wake, baadaye sana mood kazaliwa, akasema aliyetolewa hakuwa Isaka, alikuwa Ismail. hapo kuna mmoja ni mwongo, na mwongo ni yule wa juzi ambaye amewakuta wenzake wakicelebrate mambo hayo kwa maelfu ya miaka, yeye asiyejua kusoma wala kuandika, akaibuka tu na kusema walikosea, na hatoi sababu ipi inayotufanya tuamini kwamba anachokisema yeye mtoto wa juzi ndio cha kweli, ila anasema tu, na watu wanamwamini. mood mwongo sana. kajitahidi sana kubadilisha Biblia kama alivyokuwa ametumwa na shetani lakin njia ya mwongo siku zote ni fupi, huwa anakamatika tu.
 
Mtoto aliyezaliwa na kuwa Mwana wa Pekee wa Ibrahim ni Ismail, wakati Isaka anazaliwa, Ismail alikuwa ameisha zaliwa, hivyo Isaka hakuwa mwana wa pekee wa Ibrahim!.
Encyclopedia Britanica Inasema "after Ishmael and Hagar were banished, they settled in Mecca, near which they had found relief and water at the Well of Zamzam. Later, in nearby Minā, Abraham attempted to sacrifice Ishmael (rather than Isaac, as stated in the Old Testament), an event commemorated on Eid al-Adha and in the rituals of the hajj (pilgrimage)"
P
King James Version:
.2And he said, Take now thy son, thine only son Isaac, whom thou lovest, and get thee into the land of Moriah; and offer him there for a burnt offering upon one of the mountains which I will tell thee of.

Paskali usilete hadithi za rafiki zako, leta how it's written not thinking au encyclopedia, hayo ni maandiko tu ambayo yanahaririwa kila wakati kutokana na utashi wa watu hata wewe unaweza.

Kwani biblia inajisemeaje wkt wa Ibrahim kimtoa huyo kijana?.

Tukienda nje ya it's written utawin hata kwa hao wajomba wanaopinga andiko la biblia.
 
Ni kweli Ibrahim hakuwa na mitala, ila mke anakuwa huru kumtoa kijakazi wake kwa mumewe ili kumzalisha, huyo kijakazi anageuka suria, ana hadhi ya mke, ila watoto wa suria, wanakuwa ni wa bosi wake, yaani mama mwenye nyumba, hivyo baada ya Sarah kumtoa kijakazi wake, yule kijakazi akageuka suria, mtoto akawa ni wa Sarah, hivyo hakuna ubishi wowote kuwa mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail.

Hajiri alikuwa suria, ni sawa na mke, kijakazi akiisha geuka suria, hawi kijakazi tena, anakuwa mke mdogo, kazi yake ni kumhudumia baba.

Sii kweli, mtoto wa kwanza wa Ibrahim ni Ismail na aliyekuwa mtoto wa pekee ni Ismail watoto wa wajakazi ni watoto kamili, ushahidi ni watoto 12 wa Yakobo, waliozaa makabila 12 ya Israel, watoto wa lea ni 5, watoto wa Recho ni wawili, watoto 5 ni wa wajakazi wa Lea na Recho
Yes it's true, Kikristo Ismail is not a big deal, Kiislamu it's a very big deal, Iddi ya kuchinja inatokana na Isamal ambaye ndio uzao wa Uislam.
P

Suria upo wa aina mbili katika mazingira ya zamani.
1. Suria aliyechaguliwa ña Mke halali
Sarah alimchagua Hajiri.
Lea ma Rahel wakachagua vijakazi wao kuwa masuria.
2. Suria aliyechaguliwa na Mume.
Suleiman anaingia katika kundi hili.

Suria anabaki kuwa Suria na hawezi kuwa kwenye hadhi sawa ya Mke.
Biblia inaposema Suleiman alikuwa na Wake mia saba na masuria Miatatu inamaana kubwa kisheria.

Mke yupo kisheri na anapatikana kisheria kulingana na mila na tamaduni za Kale kama vile Kutoa mahari n.k.
Suria au hawara hatambuliki kisheria za kizamani,

Torati ambayo ni sheria ya Kiyahudi haitambui kitu kitu kinaitwa Suria
Inatambua Mke.

Tukija kwenye m/Watoto.

Mtoto wa kwanza kisheria za dini ni yule aliyezaliwa ndani ya ndoa. Kwa mke halali.

Kidini hasa za Ibrahim au kimila hata hapa Afrika mtoto wa kwanza ni yule ambaye umezaa ndani ya ndoa.
Bahati nzuri sheria za kiislamu zinaeleza hilo.

Tukirudi kwenye mfano uliotoa kuwa mbona Watoto wa masuria wa Yakobo walihesabika na kupewa urithi

Walihesabika kwa sababu walijua kula na kipofu.
Waliwaheshimu Wake wa Yakobo ambao ndio waliowateua kuwa masuria.

Hii ni tofauti na Hajiri ambaye alileta ujeuri na kiburi akataka ligi na mke halali wa ndoa akasahau mke huyo ndiye aliyechagua amsaidie baadhi ya majukumu na ndiye mwenye mamlaka ya kumfukuza.

Ibrahim akamwambia Mkewe Sarah kuwa huyo kijakazi wake yupo chini yake(wala sio chini ya Ibrahim) hivyo yeye ndiye mwenye maamuzi ya kumfukuza au kumbakiza.

Pascal Mayalla uliona wapi Suria mwenye hadhi sawa na mke mamlaka ya kumfukuza ikawa kwa mke mkubwa?

Tuzingatie, vijakazi wote zamani walikuwa wanakuja na Wanawake wanaoolewa tokea huko kwao au wanatafuta wenyewe na sio kAzi y mume kutafuta kijakazi wa kumsaidia mke.

Tena Baba Mkwe wa mwanamke ndiye humsaidia binti yake kumtafutia kijakazi binti yake.

Tukija kwenye urithi, baba anahaki ya kutoa urithi kwa watoto kulingana na vile awaonavyo.
Ni ngumu Mwanamke uliyetalakiana naye au kugombana naye ukatoa urithi kwa watoto wake ingawaje ni wako pia. Unaweza ukawapa lakini hawawezi kufikia donge nono kwa watoto ambao mama yao alikuwa anakufurahisha.

Tumeona Kwa Ibrahim jambo hilo lilifanyika. Kwa Yakobo tumeona Yusuphu na Yuda wakipendelewa.

Kwa Daudi tumeona Suleiman akipendelewa ilhali kuna Wakubwa zake.

Na kwa zama za leo tumeona Kesi ya Tajiri marehemu Mengi.
Pia tumeona Wake wadogo wakipendelewa au watoto wa mke mdogo wakipendelewa hii yote ni kutokana na uhusiano wa mume na wake zake.

Sio mume na masuria. Nop.
 
Hilo jina Isaka hapo limepachikwa Kwa kulazimishwa
Isaka hajawahi kuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim Kwa sababu yeye ni mtoto wa pili

Ila Ishmael ndio aliwahi kuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim

Wakati Isaka hajazaliwa Ishmael ndio alikuwa mtoto wa pekee Kwa Ibrahim

Nyinyi wagalatia mmedanganywa sana na Wazungu
Nadhani kwa sababu ukweli upo na kuna wengine wanadanganywa hebu (ukweli uwekwe hapa kimaandiko) tuache porojo za fulani au encyclopedia kasema, kaandika.

Ukweli upo ki_evidence siyo kifikra.
 
Ibrahim ni Muebrania kiasili lakini dini yake ni Myahudi na ndie muanzilishi wa dini ya wayahudi.

Mungu wa Ibrahim, isaka ma Yakobo ambaye ni Yahwe ndiye alimchagua Ibrahim kuanzisha dini ya Kiyahudi
Acha kulazimisha mambo. Uyaudi ulianzishwa na isaka kama ulivyotabkliwa kuwa uzao wake utaiwa Israeli

Waandiahi wa bibilia walikuwa makanjanja. Kasome maisha ya Ibrahim na alitokea wapi mpaka akafika nchi ya palestina ville vile kasoma maisha ya mama yake yesu alipotokea na wazazi wake walikuwa akina nani
 
Múngu wa wayahudi ndiye Mungu wa Ibrahim
Ibrahim ndiye founder Dini ya Kiyahudi
 
Jee ukweli halisi ni upi?.
Hii maana yake, kuna watu wanadanganywa, haiwezi huku awe huyu na kule awe yule!.
Umuhimu wa kuujua ukweli huu, unakupa fursa ya kujua ukweli ni upi, hivyo ufuate mafundisho yapi ndio ya kweli?..
Kitabu cha kweli ndio chenye ukweli. Endapo, vyote havina ukweli, basi ukweli haupo.
 
Back
Top Bottom