Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Japo Wakristo na Waislamu ni Watoto wa Baba Mmoja, Nabii Ibrahim na Mungu ni Mmoja, Kati ya Ismail na Isaka ni nani aliyetolewa Sadaka ya Kuchinja?

Naelewa Then kama Ni mpango wa Mungu kwanini Yuda ahukumiwe na Kulaaniwa kwa sababu hiyo?
Unahisi kuna Fair Treatment?

Na kwanini Mungu kama alitaka Yuda apate uzao asitafute Uzao kwa Wanawake wengine mpaka kwa Mke wa Mtoto wake?

Unafahamu Jinsi Yesse Alivyopatikana??
Ile story ya Naomi na Mama yake Mkwe mpaka kufikia kwa Daudi?

vItu vingi Ukivisoma Utasikitika Sana..
View attachment 3022321
Mungu ana namna zake za ajabu kufanya mambo yake. Mimi hata Yuda Iskariote naamini kabisa hana kosa na ameenda mbinguni The Role of Yuda Eskarioti Kwenye Ukombozi wa Dunia: Je, Yuda alaumiwe, alaaniwe au apongezwe?!
P
 
Hiyo ni simulizi.
Kuna msimuliaji ambaye ni Musa alafu kuna dialogue ya Wahusika humo kwenye simulizi.

Kwa hiyo Quotation unapoitoa hasa inayohusu simulizi lazima ujue nani anayezungumza.
Wakristo wengi katika jambo hili wanachanganya madesa.

Kuna sehemu Munga akasema
Kuna sehemu Ibrahim akasema au Sarah akasema,
Alafu kuna sehemu ànayesimulia ni msimulizi.

Ndio Kilekile nawaambia Watu kuhusu Injili, Zaburi na Torati na vitabu vya Hadithi.
Sio kila neno kwenye Biblia ni amri au sheria ya Mungu.

Ukisoma biblia na sio tuu biblia bali kitabu chochote lazima yapo mambo utazingatia íli usijeleta tafrani.

Mfano ni hiyo ndoto ya Ibrahim ya kumtoa Mwanaye kafara iliyopo kwenye Quran. Hiyo ni ndoto na sio tukio la kweli.

Au Yesu anapotoa mfano alafu kuna Watu wanaochukua ule mfano kama tukio la kweli ni dalili ya kutozingatia kanuni za usomaji
kwenye Qur'an ipo ndoto na lipo tukio la kweli baada ya ndoto, tofauti ni kuwa watafsiri wqmetafsiri neno lilitumika kama tafsida ya jando kuwa ni kuchinja mtu au mnyama.

Hapo simply Ibrahim alioteshwa akamte jando mwanae.
 
Owky, tunaomba historia ya Ibrahim. Biblia inajitosheleza hahitaji kuthibitishwa. Neno la Mungu limehakikiwa na Mungu mwenyewe. Type historia ya Ibrahim mpaka anaitwa na Mungu wenu, anatembea nae miaka yote mpaka anapata uzao then anatoa Baraka na kufa. Kidogo tutamwelewa Ibrahim wenu maana wetu alitoka Uru wa Wakaldayo ambayo ni Iraq ya Leo. Akasafiri mpaka Haran- maeneo ya Syria na Uturuki ya leo toka huko akaambiwa bado aendelee na safari. Alipofika Canaan akaambiwa nitakupa nchi hii wewe na uzao wako na sio na wazao wako. Je hiyo Ibrahim wenu atokea wapi? Mkewe ni nani? Tusije bishania watu wawili tofauti hapa.
Una uhakika Biblia umehakikiwa na kuthibitishwa na Mungu? Biblia ipi unayoisema wewe. Biblia ya Waprotestant na Walokole yenye vitabu 66? Au ya wakatoliki yenye vitabu 73? au ya Waorthordoks lenye vitabu vingi zaidi? Au ile ya wa Coptic? Ipi kati hizo ndo Biblia sahihi??

Kama ni Biblia ya vitabu 66 na vitabu 73 basi Unatakiwa kujua kwamba Biblia unayoisoma ni kazi ya mikono ya Mtakatifu padre Jerome na timu mwaka 325 na kilioawekwa ndani ya biblia ni kile walioona inafaa kuwekwa kulingana na namna ambavyo watalawa wa wakati huo walitaka Mkristo uwe. Lakini kanisa katoliki la Mashariki (The Orthordox) wana Biblia yenye vitabu vingi zaidi kulingana na wao walivyoo hii ndo inayofaa kuwa Biblia. Pia kanisa la Coptic la Ethiopia na Misri wana idadi tofauti ya vitabu vyao.

Pia Biblia uliyonayo ni nakili ya nakili ya nakili ya Biblia. Ina mapungufu mengi sana kutokana na nakili ya nakili ya nakili na pia kutokana na namna mzungu alivyotaka Biblia iwe. Ndo maana uliaminishwa kwama Yesu ni Mzungu na kaka yao na Nyetanyahu.
 
Kwa mtazamo wa haraka,waislam wanamtaja ismail.kwakuwa mama yake alitokea misri.mwenye ufahamu atajiongeza.

Ingekuwa alizaa na mwanamke tokea Italy,China.ila sio nchi yeyote y kiarabu.hapo show ingekuwa nyingine kabisa.nadhani hata ibrahimu asingekuwepo kwenye quran.
 
Nisome kitu ninachokijua?
Au unadhani stori hii naijadili na wewe kisha naenda ku-google kama wewe.

Ibrahim ni muebrania kwa taifa.
baba wa waebrania ni Eber mjukuu wa Nuhu(Nuhu ni Assyrian)
Dini yake ni Myahudi
Mungu wake ni Yehova.
Huyo ndiye Ibrahim
Wewe ni Mweupe katika mambo haya ya dini. Turudi zetu kule kwenye mapambio ya siasa. Ibrahi hawezi kuwa wa dini ya kitukuu chake kilichozaliwa baada ya miaka mingi Ibrahimu akiwa ameshakufa. Unaposema Myahudi unamaanisha Yuda ambaye ni mtoto wa nne wa Yako kupitia kwa Lea. Hadi wakati wa Daudi tunaona kulikuwa na Taifa la Wayuda na taifa la Israel. Haya yalikuwa mataifa mawili tofauti. Taratibu wazao wote wa Yakobo walikubaliana na utaratibi wa dini za wayuda then wakajiunga na ibada za Wayuda za kwenda Yesuralemu kusali kila mwaka . Pia tunaona baada ya Ufalme kugawanyika tena baada ya Sulemani kufariki, wayuda na Kabila la Benyamini walibaki kama Taifa la Wayuda na makabalila 10 yaliyobakio yaliunda tena ufalmwe wao wa Isreal na hawakuwa wakienda tena kusali Yerusalemu bali Samaria.
 
Ibrahim ndiye muanzilishi wa Dini ya Uyahudi.
Unafikiri ni kwa nini Kila Mungu alijitambulisha kwa manabii wa kiyahudi anasema yeye ni Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo?

Unajua Mungu wa Ibrahim anaitwa Yehova
 
Walikuwa Wakifanya Zamani kwenye Pesach (Passover) au Kiswahili Pasaka ila baada ya Kuvunjwa kwa Hekalu mwaka 70 AD..

Ibada ya Pasaka ikawa inafanyika Bila "Korban Pesach" (קָרְבַּן פֶּסַח) yaani Sacrificial lamb insteady sasa Hivi kipind Inalika Pasaka..

Kunakuwa na Mfupa wa Kondoo kama ukumbusho mezani ila nyama zinazolika ni za kawaida wanyama na hata kuku bata ila ziwe kosher tu..

Ila kuhusu Kuchinja..
Ndyo walikuwa Wakichinja na kunywa na kula Pasaka..

Unajua Waislam wamekopi Tamaduni karibu zote kutoka Kwa Judaism karibu 85% ya Ritual zao zote na Ibada ni Za kiyahudi mpaka Adhana...

Niliwahi kuelezea Hili humu kama sikosei mwaka jana kwenye uzi fulani
Kwahiyo wayahudi walikuwa wanachinja sababu ya Isaka kutolewa kama Sadaka Au Ismail kutolewa kama Sadaka.

Yaani wao wayahudi walifata taratibu za Ibrahim.
 
Implication ya kuweka hiyo aya hapo ni kuonyesha kwamba as long as Mtu ameamua kuamini uwepo wa Mungu Muumba na kuishi a righteous life basi Mtu huyo atawekwa miongoni mwa wema na atalipwa kadri ya wema wake ...regardless of his religious affiliation as long as moyo wake ulijitahidi kuwa na good intentions kwenye maisha yake na akaishi hivyo.......

Kuhusu Wayahudi kutokua na day of Judgement kwenye mafundisho yao,..hiyo sio concern yangu maana wao hawana mamlaka yoyote ya kuamua whether day of Judgement iwepo ama isiwepo....Wayahudi ni watu kama walivyo watu wengine. Yaani hatuwezi kusema Qiyama hakipo kwasababu Wayahudi wanasema hakipo...La!
Sio wao peke yao zipo jamii nyingine ambazo kwenye mafundisho yao hutokuta habari kuhusa Qiyama.
Yeah But Unajua Kuwa Andiko ulilotoa Linamaanisha Kama wakiamini? Yaani Mpaka uwe mwislamu?

But Unafahamu kuwa agano la kale lote haluna hizo mambo za kiama?

Ila zipo kwenye agano Jipya Why tuwalaumu??
 
Hizo zako zote ni porojo.

Dhabah au Dhibihi i;liyotumika hapo inamaanisha "incision" hiyo ni tafsida ya jando.

Nenda ukaijuwe maana ya neno Dhabah na dhabih katika Lisan Al Arab cha Ibn manzour.

Unasema kichinjwacho wakati hujakioandika hicho kichinjwacho? Hakuna.

Hapo panada ushuke inabaki kuwa ni jando ytu. Watafsiri wa Kiislam walifata matamanio yao au walikuwa na agenda zao.

Jiulize, hivi Allah kweli anahitaji kafara ya damu hata aagize mtu amchinje mwanawe? Bado hujaiona "plot" iliyotumiwa na watafsiri waliopotosha.

Hakuna mtoto wala mtu mzima aliyetaka kuchinjwa na hakuna hata jina Sarah katika Qur'an mmelitowa wapi?
Ok Then nijibu Kuhusu Aya nilizokuonyesha hapo Chini za Suratul Baqara aya ya 67 na aya ya 71 niliyokupa..

Ambayo imetaja maneno hayo lakini Wakiamrishwa kumfanyia Ngombe Jike ..

Swali langu ni jepesi tu Kwahyo Mungu alimuamuru Musa Awaambie wana wa Israeli wamtahiri Ngombe Jike???
Swali jepesi tu
 
Una uhakika Biblia umehakikiwa na kuthibitishwa na Mungu? Biblia ipi unayoisema wewe. Biblia ya Waprotestant na Walokole yenye vitabu 66? Au ya wakatoliki yenye vitabu 73? au ya Waorthordoks lenye vitabu vingi zaidi? Au ile ya wa Coptic? Ipi kati hizo ndo Biblia sahihi??

Kama ni Biblia ya vitabu 66 na vitabu 73 basi Unatakiwa kujua kwamba Biblia unayoisoma ni kazi ya mikono ya Mtakatifu padre Jerome na timu mwaka 325 na kilioawekwa ndani ya biblia ni kile walioona inafaa kuwekwa kulingana na namna ambavyo watalawa wa wakati huo walitaka Mkristo uwe. Lakini kanisa katoliki la Mashariki (The Orthordox) wana Biblia yenye vitabu vingi zaidi kulingana na wao walivyoo hii ndo inayofaa kuwa Biblia. Pia kanisa la Coptic la Ethiopia na Misri wana idadi tofauti ya vitabu vyao.

Pia Biblia uliyonayo ni nakili ya nakili ya nakili ya Biblia. Ina mapungufu mengi sana kutokana na nakili ya nakili ya nakili na pia kutokana na namna mzungu alivyotaka Biblia iwe. Ndo maana uliaminishwa kwama Yesu ni Mzungu na kaka yao na Nyetanyahu.
Kichwani kwangu sina picha ya Yesu Kwa sababu amri ya kwanza ya Mungu inasema clearly, usifanye chochote kwa mfano wangu duniani, mbinguni au kuzimu.
Ile ni picha imetengenezwa na kina
Mungu ana namna zake za ajabu kufanya mambo yake. Mimi hata Yuda Iskariote naamini kabisa hana kosa na ameenda mbinguni The Role of Yuda Eskarioti Kwenye Ukombozi wa Dunia: Je, Yuda alaumiwe, alaaniwe au apongezwe?!
P
Yuda anakosa Moja tu, hakutubu alijiua. Petro alimkana Yesu ila baada ya kufufuka kwake wito ulipotumwa kwake wakutane Galilaya aliitikia. Na kuthibitisha Yesu mwenyewe wakati anatoa hesabu Kwa Baba yake kwenye Yohane 17 anasema ," sikumooteza hata mmoja isipokuwa yule mwana wa uovu ili litimie neno". Nisamehe ila inabidi nikudisapoint hapo kwa Yuda. Ametumika kama farao wa agano jipya.
 
Nimewahi kuwa Christian tena nilikuwa Mchungaji Nimewahi kuwa Muslim na nimewahi kuwa jewz..
Hakika katika Vyote Hivyo hakuna Upendo ni chuki iliyokithiri ndiyo hufundishwa Ndani..

Chuki Ambayo watu hudanganywa Ni Upendo..Bado nawasoma hinduism na Budha ni watu wenye Upendo wa Hali ya Juu sana Pengine kuliko Wakristo na Waislamu..

Spirituality without religion ni kama personal quest for understanding and connection with something larger than oneself ambayo Ndo Emmanuel au Mungu yaani kuamini kwamba Una Mungu ndani yako, kuamini kwamba We are All connected all creature, Kuamini kwamba Hakuna Kitu chenye thamani dhidi ya kingine..

Muhubiri 3
View attachment 3022312
Yaani focuses on inner peace, harmony, na kuamini Duniani Hjaja Kwa bahati mpaka Kuwa kila kitu kinakuja On purpose na Kuamini Kila Hatua unayopiga ni funzo na Ndyo hasa Njia uliyoitwa Kuifanya Duniani...
Kuamini Kwamba Bila Upendo Sisi Ni kitu Bure..
View attachment 3022314

Kuamini kwamba Vitabu vyote Vitakatifu vyafaa kwa ajili ya Kuonya katika njia ya Haki ila Tumeharibu Ujumbe wake na tunautumia Kinyume na maana zake

Kuishi maisha ya Adabu katika kila kitu hata kula
Mwisho kutafuta maana ya Kuishi...
Spirituality bado ni Imani juu ya Mungu(concept) yule yule wa bible na QUR'AN,wahindu hawana upendo wowote,labda Kama hufuatilii yaliyo na yanayojiri india
 
Kama wayahudi wanaamini kitabu cha Daniel basi wanatakiwa waamini ipo siku ya mwisho yenye hukumu. Daniel anaelezea vision ya kuona siku kiti Cha Enzi kimewekwa mbinguni na Mzee wa Siku ameketi juu yake. Alipoletwa Mwana wa Mtu akaletwa na kuwekwa mbele ya Mzee wa Siku. Naye akapewa mamlaka ya kuhukumu. Hiyo tayari ni tafsiri kwamba kuna siku ya mwisho Kwa viumbe vyote vilivyoumbwa.
Kila mwaka Wayahudi Wana siku ya Mwisho na Siku ya Hukumu na siku Ya kusamehewa Dhambi kila mwisho wa mwaka na mwanzo wa Mwaka wao wanaziita sikukuu hizo..
Rosh Hashanah and Yom Kippur.

Ila hakuna siku maalum kwamba mwisho wa kila kitu..

Daniel Ipo na inasomwa vizuri ila haijaongea kuhsuu Mwisho wa hkumu kwa kila mmoja..
Kitabu cha Sefer Daniel au Daniel ni kitanu cha narative Na Apocaptical version..

Na kwa Judaism kipi kwenye Aina inayoitwa ketuviim..

Ni alot of Complication but Kwenye Vitu vingi Wasilam na wakristo hufanana ila sio wakristo na wayahdi
 
Nimekwambia kasome kuhusu "Locution" au "lexicon" ndiyo utanielewa. Nimekwambia hiyo hapo kwa Ibtrahim na Ishaka imetumika kama tafsida, lakini siyo mtu kuchinjwa kukatwa shingo.

Mfanoi ukiambiwa "serikali ina mikono mirefu" unaelewa nini? Au ukisikia mashabiuki wa mpira wakisema "alotaka kufunga akakatwa mtama" inamaanisha nini?

Ukiyaelewa hayo utaelewa maana ya "Lisan" (locution) ambayo imetajwa sana kwenye Qur'an.
Locution nafahamu na hata Lexicon nazifahamu I was a Pastor one najua vizuri..

Hizo terms Angesema Mkristo ningemuelewa Zaidi..
Maana Mara nyingi Wao husema Mpaka Roho Mtakatifu akufunulie Andiko lilikuwa lina maana ipi..

But in quran hakuna Lexicon words kwenye Amri yoyote..
 
Spirituality bado ni Imani juu ya Mungu(concept) yule yule wa bible na QUR'AN,wahindu hawana upendo wowote,labda Kama hufuatilii yaliyo na yanayojiri india
Hinduism has nothing to do with India..
Ni sawa na Useme Waislam wote wahuni na wanapenda Starehe si unaona Dubai ilivyo...
Thats unlogical arguments
 
kwenye Qur'an ipo ndoto na lipo tukio la kweli baada ya ndoto, tofauti ni kuwa watafsiri wqmetafsiri neno lilitumika kama tafsida ya jando kuwa ni kuchinja mtu au mnyama.

Hapo simply Ibrahim alioteshwa akamte jando mwanae.
🤣🤣🤣🤣🤣
Na Musa aliambiwa Atoe Jando kwa Ng'ombe pia Sio..
QURAN 2:67, QURAN 2:71
 
Back
Top Bottom