Japokuwa Madini ya Zinc huhitajika kwa kiasi kidogo mwilini yana faida kubwa sana kiafya

Japokuwa Madini ya Zinc huhitajika kwa kiasi kidogo mwilini yana faida kubwa sana kiafya

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Madini ya zinc huhitajika kwa kiasi kidogo mwilini lakini huwa na faida kubwa sana kwa afya.
Kwa mujibu wa National Institutes of Health, wanawake wenye umri wa miaka 19 na kuendelea huhitaji kiasi cha 8 mg kila siku huku wanaume wakihitaji kiasi cha 11 mg.

Wakati wa ujauzito na unyonyeshaji kiasi hiki huongezeka kufikia 11 mg na 12 mg mtawalia.

Madini haya hupatikana kutoka vyanzo mbalimbali vya asili hasa kutoka kwenye maharage, samaki, nyama, vyakula jamii ya karanga, maziwa, mayai, uyoga na mchele wa kahawia.

Tumefafanua faida za madini ya zinc kwenye afya yako
Twende pamoja.

1. Vidonda
Upungufu wa madini ya zinc huhusishwa na kukawia kupona kwa vidonda.
Tafiti za tangu miaka ya 1970 zinathibitisha hoja hii. Madini ya zinc huhusika kwenye kila hatua za uponaji wa vidonda kuanzia kwenye kurekebisha ngozi iliyoharibika, kuondoa uvimbe joto hadi kuzuia maambukizi. Hii inafaa kwa aina zote za vidonda, viwe vya ajali, moto au upasuaji.

2. Magonjwa sugu
Mkazo wa seli huwa ni chanzo kikubwa cha kutokea kwa magonjwa sugu mwilini hasa saratani, shinikizo kubwa la damu na kisukari. Huongeza uwezo wa mwili kwenye kudhibiti ongezeko kubwa la sukari, pamoja na kuongeza msisimko wa vimeng’enya vya insulin katika kulinda kiwango cha kawaida cha sukari mwilini.
Aidha, huboresha afya ya mishipa ya damu, huongeza kiasi cha madini ya sodium yanayotolewa mwilini kupitia mkojo pamoja na kupunguza shinikizo la damu.

Magonjwa haya ni hatari kwa afya.

3. Kuhara
Kwa mujibu wa WHO, kuhara ni kisababishi cha pili duniani kinachoongoza kwa kuua watoto wengi wenye umri chini ya miaka 5. Wastani wa watoto 525,000 duniani hufariki kila mwaka kutokana na ugonjwa huu.
Virutubisho vya zinc husaidia kutibu tatizo hili haraka. Hupunguza vifo vitokanavyo na kuhara kwa asilimia 23. Ni muhimi kama watoto watapatiwa kiasi cha kutosha cha madini haya kwani huwa na faida kubwa sana kwao.

Watu wazima pia hufaa kwao.

4. Kinga mwili
Madini ya zinc huathiri utendaji kazi wa mfumo wa kinga wa asili ambao mtu huzaliwa nao pamoja na ule anaopata kutokana na chanjo au kuugua magonjwa mbalimbali kwenye kipindi cha uhai wake. Huongeza uwezo wa aina mbalimbali za chembechembe nyeupe za damu kwenye kupambana na vimelea vya magonjwa, uvimbe joto pamoja na kuongoza mfumo wa vinasaba kwenye kutengeneza kopi mpya, kurithisha taarifa pamoja na kugawanyika kwa seli za mwili.

Virutubisho hivi hufaa sana kwa wazee ambao uwezo wa kupambana na magonjwa hupungua kutokana na umri kuwa mkubwa.

Pasipo kujali umri wako, jitahidi kutumia virutubisho hivi ili uongeze kinga mwili yako kwa kuwa huhitajika kwa kila mtu.

Upungufu wa madini haya hupunguza uwezo wa mwili kwenye kupambana na maradhi, pia hukaribisha maambukizi ya mara kwa mara.

5. Uzazi
Zinc husaidia kuboresha afya ya uzazi kwa wanawake na wanaume hasa pale inapotumika kwa pamoja na folate.

Huwa na nafasi kubwa katika kufanikisha kukomaa kwa mbegu za kiume, uzalishwaji wa vichocheo vya kiume pamoja na kuboresha mzunguko wa hedhi za wanawake.

6. Chunusi
Chunusi ni tatizo linalo athiri walau asilimia 9.4 ya watu wote duniani.

Tafiti zinathibitisha kuwa utumiaji wa madini ya zinc, iwe kwa kumeza au kupaka kwenye ngozi hupunguza uvimbe joto pamoja na kuthibiti ukuaji wa bakteria wanaosababisha tatizo hili.

Aidha, uchunguzi unaonesha kuwa watu wengi wanaosumbuliwa na tatizo la chunusi huwa na kiwango kidogo cha zinc mwilini hivyo matumizi ya madini haya yanaweza kusaidia kwenye tiba.

7. Magonjwa ya uzee
Wazee hukabiliwa na changamoto nyingi za kiafya, baadhi yake ni kupungua kwa uwezo wa kuona, maambukizi ya mara kwa mara ya magonjwa na nimonia.

Kwa mujibu wa National Insititutes of Health, matumizi ya zinc huboresha afya ya macho kwa wazee pamoja na kuwapunguzia hatari ya kupatwa na upofu.

Huwakinga na changamoto ya kupatwa na ugonjwa wa nimonia.
Ni muhimu kama wazee watapatiwa virutubisho hivi ili kuwaepushia magonjwa na changamoto mbalimbali zinazoweza kutokea kwenye umri huu.

8. Mafua
Utafiti mdogo wa mwaka 2011 uliofanywa na Harri Hemila ( Zinc lozengers may shorten the duration of Colds: A systematic Review) unaonesha kuwa zinc husaidia kutibu tatizo la mafua.

Hata hivyo, bado hakuna tafiti nyingi zenye kuthibitisha madai haya.

Muhtasari
Madini haya huathiri uwezo wa utambuzi wa ladha mbalimbali za vyakula pamoja na harufu.
Kama unakabiliwa na tatizo hilo pengine mwili wako umepungukiwa na madini ya zinc, jitahidi uongeze matumizi ili kurejesha hali yako ya kawaida.

Pamoja na ukweli kuwa madini haya huhitajika kwa kiasi kidogo mwilini, nguvu yake kwenye kuongoza kazi na mifumo mingi ya mwili ni kubwa sana.

Huongoza utendaji kazi wa zaidi ya vimeng’enya 200 kwenye mwili wako.

Chanzo: Afyainfo
 
Kama hujasema yanaongeza NGUVU ZA KIUME basi wewe ni mkweli, na hata ungesema zinc unayo chumbani ningekuja nunua 😂
 
Back
Top Bottom