Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Ile video imeniharibia siku. Nilijisikia vibaya sana moyoni. Jamaa anapiga makelele ya mtu aliyekata tamaa akiomba msaada na kuelezea hali anayokwenda kukumbana nayo.

Allah Kareem akawaangamize utawala wa kisheitwani ukiongozwa na Samia na wahuni wenzake wote wa CCM. Hawana haya wala hofu kwamba wataulizwa kaburini juu ya yale waliyotendea wengine. Kuvaa ushungi kujisitiri inafaa nini ikiwa matendo yake ni ya kishirikina na kisheitwani? Mjaa laana mkubwa!
 
Upumbavu wangu wanauelewa wanao wateka kuwa ni akili kubwa sana ..ila nyinyi wapumbavu wa chadema hamuwezi kunielewa ....mimi ni the great genius mkubwa sana ....niliwaambia watu kuwa MUISLAMU HAFAI KUWA KIONGOZI TANZANIA NA MWANAMKE HAFAI KUWA KIONGOZI TANZANIA ...kwa sasa tunaongozwa na sifa zote mbili zisizofaa yaani RAIS MUISLAMU NA MWANAMKE
Ukiweka Mkiristo Parapanda inapigwa wanapanda juu kama ilivyo leo. Katiba ifanyiwe amendments kabla ya uchaguzi wa 2025 vinginevyo hili ombwe halitaisha.
 
Mimi siku hizi silaumu issue za hivo baada ya jamaa yetu kitaa kupekekwa galilaya kumbe jamaa alikua anajishughulisha na ugaidi..na alikua anazugia kwenye maduka ya simu..Sasa jamaa sijui walimjuaje Yani hapo ndio huwa nachoka maana ata hafananiiii na izo mbanga
Tatizo ni aina ya uchukuaji. Kwanini wasije na mavazi ya kiaskari walau mmoja? Staili wanayoitumia inaacha mwanya kwa wahalifu kuitumia kwa kujifanya maafisa usalama. Ni nchi ya kishenzi sana Tanzania ni vile basi tu!
 
Tukio la kusikitisha sana limetokea Kiluvya Madukani -Dar ,katika Hotel ya Rovvenpec tar.11/Nov/2024. Ikionesha watu wakimteka Ndg. Deogratius Tarimo(Deo Bonge) na kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Taarifa ya Polisi. Tanzania waliyoitoa leo tar. 13/Nov./2024 wanakiri kupokea taarifa ya tukio hili kutoka kwa Deo Bonge tar. 11 ambapo alienda kulalamika kituo cha Polisi Gogoni-Kiluvya,Wilaya ya Ubungo. Polisi wanakiri hawawatambui watu hao ila watawakamata.

Maswali ya kujiuliza.

1. Hao watu wenye Ujasiri wa kukamata (kumteka) mtu kwa nguvu Mchana kweupe wakiwa na pingu kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi.Ni watu gani hawa?

2. Kwanini wakati wanamkamata (kumteka) walikuwa wanatamka "Twende Gogoni" ambapo Gogoni ni kituo cha Polisi Kilichopo Kiluvya, Wilaya ya Ubungo- Dar kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi. Ni watu gani hawa?

3. Kwanini wakati wanamkamata (Kumteka) watamke kwa nguvu kwamba sisi ni Askari, sisi ni Askari? Ikiwa Polisi kupitia taarifa yao wamewakana kwamba hawawajui. Ni watu gani hawa wana Ujasiri kujitambulisha kama wao ni Polisi ikiwa sio Polisi?

4. Ikiwa ukamataji ulikuwa na nia njema kama sio Kumteka,kwanini baada ya kuzidiwa nguvu waliamua kumuacha na pingu mkononi na kukimbia huku wakisema tutakukafuata. Kwanini wakimbie? Kama sio Polisi. Ni watu gani hawa?

Kuongezeka kwa vyombo vya ukamataji tofauti na vyombo 3 kisheria ni sababu kubwa ya haya matukio kutokokea. Vyombo 3 kwa mujibu wa Sheria vyenye mamlaka ya kukamata, kupekua na kupeleleza ni POLISI, TAKUKURU na UHAMIAJI. Na ambapo ukikamatwa na Polisi unapelekwa kituo cha Polisi, ukikamatwa na Uhamiaji unapelekwa uhamiaji, Ukikamatwa na TAKUKURU unapelekwa TAKUKURU.

Mwaka 2023 kulifanyika marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ambapo kifungu cha 4(3) kikaruhusu Afisa wa Usalama wa Taifa kukamata mtu. Na haijulikani wapi anakupeleka. Sheria hii imeongeza mwanya wa matukio ya utekaji, inawezekana aidha kifungu cha Sheria hii kinatumika vibaya au kuna kikundi cha wahuni kinatumia mwanya wa Sheria hii kwa maslahi binafsi.

Pia Polisi kutofuata Sheria na taratibu za ukamataji, kumeongeza mwanya wa matukio haya Sababu imekuwa ni ngumu kujua nani ni Polisi nani sio Polisi. Police wameamua kupuuza utawala wa Sheria (Rule Of Law ) kupitia Sheria zinazowaongoza katika majukumu Yao ya kila siku kama, Police Force and Auxiliary Service Act, Cap 322 R.E 2002, Criminal Procedure Act, Penal Code na Police General Order. Sheria zote hizi kama Police wangekuwa wanaziheshimu na kuzifuata zingetofautisha Polisi na watu wengine. Wahuni wengine wasinge kuwa na uwezo wa kujitambulisha kama ni Polisi ikiwa sio Polisi.

View attachment 3150874View attachment 3150875
View attachment 3150876
Aise sisi wabongo sijui huu uoga tumetoa wapi yan hao maboyo ilitakiwa wananchi wawashushie kipigo cha kufa mtu
 
Ila na pia tungependa kujuwa huyo deo bonge ni nani na anajishugulisha na nini???
Au naye mwanaharakati

Ova
 

Attachments

  • 354506.jpg
    354506.jpg
    14.5 KB · Views: 1
  • 20241113_042356.jpg
    20241113_042356.jpg
    234.1 KB · Views: 3
Tutajua tu,itoshe kuanzia sasa kama anakamatwa popote na watu waliovaa kiraia bila kujali na police basi jua ni majambazi ,nguvu ya umma itumike, na kama swala ni kufika kituo cha police ambacho inasemekana kipo karibu na eneo la tukio why kutumia nguvu nyingi kiasi hicho ,hawa hawakua na nia njema kwa uyu ndugu
 
Kila nikiangalia hii Video naijiwa na Hisia mbaya za Viongozi wetu. Imani imenitoka nawaombea baya lolote liwapate. Am real disappointed, at the end tungeambiwa KIFO NI KIFO TUUU!
Hatuna viongozi tuna watawala na wajukuu wa Hitler.
 
Siwalaumu polisi nawalaumu hao kukumaji wanaume wa dar waliokuwa wanashangaa na kushindwa kumsaidia mwenzao,oumbavu kabisa
Mtoa msaada ndie anae umia..hofu ni jamaa wakiwa na 🔫 chukulia mfano tukio la mzee Ali kibao..yaan ungejiingiza TU KUSAIDIA ni kujitoa kafara.

NB.
Ni Bora ufe ukitetea haki kuliko kukaa kimya huku uovu ukitendeka.
 
Back
Top Bottom