Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Mimi nawalaumu raia wote wapo kimya tunaishi kama wanyamapori kwanini hawakuchukua hatua hata ya kuhoji kuwa ni akina nani na vitambulisho vyao akuna mjumbe wala mwenyekiti.

HUYO DEO BONGE NI NANI KWANINI AKAMATWE NA NAMNA ILE NA KUSIWE NA MSAADA WOWOTE. ANAJISHUGHULISHA NA NINI??
Raia wakiona pingu kwao inatasha kuwatambua watekaji kama ni polisi, kumbe pingu hata bunduki zipo za kukodi.

Hata huyo bonge atakuwa anawafahamu watekaji, ila jamii ya kiluvya nayo duu, utulivu ni F, yaani mtu anapiga kelele, majirani nisaidieni wanaenda kuniua hawamsaidii tena watekaji baada ya jaribio kushindikana wanaahidi kurudi lakini jamii ya kiluvya iko kimyaaa😤
 
Mkuu

Huyo Fike Wilson alishawahi kuwa bingwa wa Kickboxing Tanzania enzi hizo, baadaye akahamia kwenye masumbwi (boxing) kabla hajafungua gym pale Sinza na Kinondoni...ndio huyo hapo kwenye mlango wa gari.

Upelekezi unapaswa kuanzia kwake.
Kumbe watu wanawajua WATU.
 
Picha zinaonekana vzuri kabisa. Ingekuwa halali yao kutangulizwa akhera hata usiku haujaingi
Umeshaambiwa;
Yule anaitwa Fike Wilson, a former Tanzania Kick Boxing Champion alitaka kumteka Deo Bonge.
Those two men who attempted to abduct the guy, their faces are clearly seen, and therefore it is easy to trace them after a wide publication of their faces on social
 
Maswali ya upande wa pili nayo muhimu
Ni shughuli/mawasiliano zi/yapi afanyazo/yo Ndugu Tarimo ambazo/yo zi/yana ukakasi katika jamii?
Plate number ya gari ?
Mtaani siku hizi watu hawatoi msaada kabsaa.
 
Nadhani tuna sehemu nzuri ya kuanzia hili lazima lifike mwisho, kwanza siamini kama hawa ni polisi maana kama ni kweli polisi na wako kisheria wasingemuacha najuwa kuna watu wanasema walikuwa wanasema sisi polisi hiyo yoyote anaweza kusema pili toka lini polisi wakatumia gari kama ile lakini yote ni lazima polisi wawakamate hawa jamaa wawe polisi au sio polisi. Bonge yupo ahojiwe hili tukio na kwanini yeye? nini nyuma yake aligombana na mtu au anashuku nini kosa. yako maswali mengi polisi lazima wajibu maana sehemu ya kuanzia ipo na wafanye haraka sana. Kuna haja ya sheria kubadilshwa haraka sana kuwe na taratibu za arrest mtu ziko serikali za mitaa wako wajumbe lazima wahusishwe katika utambulisho.
NAKAZIA "yako maswali mengi polisi lazima wajibu maana sehemu ya kuanzia ipo na wafanye haraka sana"
 
Tukio la kusikitisha sana limetokea Kiluvya Madukani -Dar ,katika Hotel ya Rovvenpec tar.11/Nov/2024. Ikionesha watu wakimteka Ndg. Deogratius Tarimo(Deo Bonge) na kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Taarifa ya Polisi. Tanzania waliyoitoa leo tar. 13/Nov./2024 wanakiri kupokea taarifa ya tukio hili kutoka kwa Deo Bonge tar. 11 ambapo alienda kulalamika kituo cha Polisi Gogoni-Kiluvya,Wilaya ya Ubungo. Polisi wanakiri hawawatambui watu hao ila watawakamata.

Maswali ya kujiuliza.

1. Hao watu wenye Ujasiri wa kukamata (kumteka) mtu kwa nguvu Mchana kweupe wakiwa na pingu kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi.Ni watu gani hawa?

2. Kwanini wakati wanamkamata (kumteka) walikuwa wanatamka "Twende Gogoni" ambapo Gogoni ni kituo cha Polisi Kilichopo Kiluvya, Wilaya ya Ubungo- Dar kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi. Ni watu gani hawa?

3. Kwanini wakati wanamkamata (Kumteka) watamke kwa nguvu kwamba sisi ni Askari, sisi ni Askari? Ikiwa Polisi kupitia taarifa yao wamewakana kwamba hawawajui. Ni watu gani hawa wana Ujasiri kujitambulisha kama wao ni Polisi ikiwa sio Polisi?

4. Ikiwa ukamataji ulikuwa na nia njema kama sio Kumteka,kwanini baada ya kuzidiwa nguvu waliamua kumuacha na pingu mkononi na kukimbia huku wakisema tutakukafuata. Kwanini wakimbie? Kama sio Polisi. Ni watu gani hawa?

Kuongezeka kwa vyombo vya ukamataji tofauti na vyombo 3 kisheria ni sababu kubwa ya haya matukio kutokokea. Vyombo 3 kwa mujibu wa Sheria vyenye mamlaka ya kukamata, kupekua na kupeleleza ni POLISI, TAKUKURU na UHAMIAJI. Na ambapo ukikamatwa na Polisi unapelekwa kituo cha Polisi, ukikamatwa na Uhamiaji unapelekwa uhamiaji, Ukikamatwa na TAKUKURU unapelekwa TAKUKURU.

Mwaka 2023 kulifanyika marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ambapo kifungu cha 4(3) kikaruhusu Afisa wa Usalama wa Taifa kukamata mtu. Na haijulikani wapi anakupeleka. Sheria hii imeongeza mwanya wa matukio ya utekaji, inawezekana aidha kifungu cha Sheria hii kinatumika vibaya au kuna kikundi cha wahuni kinatumia mwanya wa Sheria hii kwa maslahi binafsi.

Pia Polisi kutofuata Sheria na taratibu za ukamataji, kumeongeza mwanya wa matukio haya Sababu imekuwa ni ngumu kujua nani ni Polisi nani sio Polisi. Police wameamua kupuuza utawala wa Sheria (Rule Of Law ) kupitia Sheria zinazowaongoza katika majukumu Yao ya kila siku kama, Police Force and Auxiliary Service Act, Cap 322 R.E 2002, Criminal Procedure Act, Penal Code na Police General Order. Sheria zote hizi kama Police wangekuwa wanaziheshimu na kuzifuata zingetofautisha Polisi na watu wengine. Wahuni wengine wasinge kuwa na uwezo wa kujitambulisha kama ni Polisi ikiwa sio Polisi.

View attachment 3150874View attachment 3150875
View attachment 3150876
Ahoo kwani kabla ya 2023 utekaji haukuwepo acha kutumia rejea kengefu hoja ni ukiuwani wa Utawala wa sheria
 
Uroho wa Madaraka ili kumiliki bandari utatuletea shida kubwa mbeleni
 
TISS hawawezi kumkamata mtu kizembe namna ile,dar sasa hivi kuna wale polisi jamii(shirikishi),mitaani wanasaidia kimtindo kuzima uhalifu,ila baadhi yao mambo wanayofanya wanalichafua jeshi la polisi
Are you sure?

Mkwere alirahisisha ajira ndo tukawapata akina Mafwere ambao wakahamishiwa polisi kwa ajili ya utekelezaji
 
Kila nikiangalia hii Video naijiwa na Hisia mbaya za Viongozi wetu. Imani imenitoka nawaombea baya lolote liwapate. Am real disappointed, at the end tungeambiwa KIFO NI KIFO TUUU!
Kiongozi wako yupi na kafanya nini?

Msisisikilize upande mmoja tu, biashara ipi ya kwenda kufanyia bar?

Picha si ziko na polisi wamesema watawashika tu? Tusubiri. Na Deo mwenyewe afunguke, biashara ipi ya bar?
 
We ni mpuuzi, ndivyo mlivyo nyie watu wa jihad.
Wewe usiye mpuuzi, Deo
We ni mpuuzi, ndivyo mlivyo nyie watu wa jihad.
kishajulikana, na alioshindana nao mmoja kishajulikana, au hujaupigtia uzi vizuri. Nenda kalipize, haki itendeke.

Unaogopa nini na kujifanya unahjuwa kuliko polisi? Kuwa 'vigilante' tu. Hata sifahamu kama unaijuwa maana yake.
 
Duh kama ndy tiss ndy hao basi hamna kitu watu wa ovyo kabisa
Ona wanavyo operate kama walevi wanaogombea wanawake

Ova
Ndo maana wamewekewa kinga dhidi ya jinai.

Hawaogopi wala kustushwa na kelele zetu
 
Back
Top Bottom