Jaribio la kumteka Deogratius Tarimo (Deo Bonge) huko Kiluvya, na Maswali tata

Raia hao wamejionea ni walevi tu wanaotokea bar wameshalewa.

Wakanunuwe ugomvi wa watu wanaotoka bar?
Wewe muislamu shetani, shetani wewe. Unawadhalilisha waislamu wenzako.You should not be that hopeless! One can say that we are all "hopeless" to some extent, but not to the extreme hopelessness as you are!
 
Screenshot_20241113-083737.jpg
 
Mimi siku hizi silaumu issue za hivo baada ya jamaa yetu kitaa kupekekwa galilaya kumbe jamaa alikua anajishughulisha na ugaidi..na alikua anazugia kwenye maduka ya simu..Sasa jamaa sijui walimjuaje Yani hapo ndio huwa nachoka maana ata hafananiiii na izo mbanga
Unasafari ndefu sana, alithibitishwa au ulivyoambiwa na wewe ukapokea kama ilivyo?
 
HIVI mgambo hawezi kukamata mtu.
Mgambo ni Msaidizi wa Police (Auxiliary Police )anaweza kukukamata ila destination yake ni kukupeleka kituo cha Polisi ,hata wewe unaweza kukamata mhalifu kwa mujibu wa Sheria ya mwenendo wa Makosa ya Jinai kifungu cha 16 (Arrest by Private Persons) ikiwa kuna mtu ametenda kosa la Jinai mbele yako, na hatma yake ni akupeleke Polisi ,sio akuchukue kukupeleka anapotaka. Na asijifanye ni Polisi ,na anapaswa akwambie kosa lako .
 
Tukio la kusikitisha sana limetokea Kiluvya Madukani -Dar ,katika Hotel ya Rovvenpec tar.11/Nov/2024. Ikionesha watu wakimteka Ndg. Deogratius Tarimo(Deo Bonge) na kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Taarifa ya Polisi. Tanzania waliyoitoa leo tar. 13/Nov./2024 wanakiri kupokea taarifa ya tukio hili kutoka kwa Deo Bonge tar. 11 ambapo alienda kulalamika kituo cha Polisi Gogoni-Kiluvya,Wilaya ya Ubungo. Polisi wanakiri hawawatambui watu hao ila watawakamata.

Maswali ya kujiuliza.

1. Hao watu wenye Ujasiri wa kukamata (kumteka) mtu kwa nguvu Mchana kweupe wakiwa na pingu kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi.Ni watu gani hawa?

2. Kwanini wakati wanamkamata (kumteka) walikuwa wanatamka "Twende Gogoni" ambapo Gogoni ni kituo cha Polisi Kilichopo Kiluvya, Wilaya ya Ubungo- Dar kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi. Ni watu gani hawa?

3. Kwanini wakati wanamkamata (Kumteka) watamke kwa nguvu kwamba sisi ni Askari, sisi ni Askari? Ikiwa Polisi kupitia taarifa yao wamewakana kwamba hawawajui. Ni watu gani hawa wana Ujasiri kujitambulisha kama wao ni Polisi ikiwa sio Polisi?

4. Ikiwa ukamataji ulikuwa na nia njema kama sio Kumteka,kwanini baada ya kuzidiwa nguvu waliamua kumuacha na pingu mkononi na kukimbia huku wakisema tutakukafuata. Kwanini wakimbie? Kama sio Polisi. Ni watu gani hawa?

Kuongezeka kwa vyombo vya ukamataji tofauti na vyombo 3 kisheria ni sababu kubwa ya haya matukio kutokokea. Vyombo 3 kwa mujibu wa Sheria vyenye mamlaka ya kukamata, kupekua na kupeleleza ni POLISI, TAKUKURU na UHAMIAJI. Na ambapo ukikamatwa na Polisi unapelekwa kituo cha Polisi, ukikamatwa na Uhamiaji unapelekwa uhamiaji, Ukikamatwa na TAKUKURU unapelekwa TAKUKURU.

Mwaka 2023 kulifanyika marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ambapo kifungu cha 4(3) kikaruhusu Afisa wa Usalama wa Taifa kukamata mtu. Na haijulikani wapi anakupeleka. Sheria hii imeongeza mwanya wa matukio ya utekaji, inawezekana aidha kifungu cha Sheria hii kinatumika vibaya au kuna kikundi cha wahuni kinatumia mwanya wa Sheria hii kwa maslahi binafsi.

Pia Polisi kutofuata Sheria na taratibu za ukamataji, kumeongeza mwanya wa matukio haya Sababu imekuwa ni ngumu kujua nani ni Polisi nani sio Polisi. Police wameamua kupuuza utawala wa Sheria (Rule Of Law ) kupitia Sheria zinazowaongoza katika majukumu Yao ya kila siku kama, Police Force and Auxiliary Service Act, Cap 322 R.E 2002, Criminal Procedure Act, Penal Code na Police General Order. Sheria zote hizi kama Police wangekuwa wanaziheshimu na kuzifuata zingetofautisha Polisi na watu wengine. Wahuni wengine wasinge kuwa na uwezo wa kujitambulisha kama ni Polisi ikiwa sio Polisi.

View attachment 3150874View attachment 3150875
View attachment 3150876
sisi wenyewe tuanze msako kuanzia na huyu jamaa anayonekana vizuri kabisa tumuue kufukisha ujumbe
 
Raia wakiona pingu kwao inatasha kuwatambua watekaji kama ni polisi, kumbe pingu hata bunduki zipo za kukodi.

Hata huyo bonge atakuwa anawafahamu watekaji, ila jamii ya kiluvya nayo duu, utulivu ni F, yaani mtu anapiga kelele, majirani nisaidieni wanaenda kuniua hawamsaidii tena watekaji baada ya jaribio kushindikana wanaahidi kurudi lakini jamii ya kiluvya iko kimyaaa😤
Sio mtaa wa kuishi inabidi aludi kwao kwa wazee nyumban alipozaliwa kwanza at list mpaka mwakan kule hawatamfata kamwe
 
Tukio la kusikitisha sana limetokea Kiluvya Madukani -Dar ,katika Hotel ya Rovvenpec tar.11/Nov/2024. Ikionesha watu wakimteka Ndg. Deogratius Tarimo(Deo Bonge) na kumlazimisha kuingia kwenye gari.

Taarifa ya Polisi. Tanzania waliyoitoa leo tar. 13/Nov./2024 wanakiri kupokea taarifa ya tukio hili kutoka kwa Deo Bonge tar. 11 ambapo alienda kulalamika kituo cha Polisi Gogoni-Kiluvya,Wilaya ya Ubungo. Polisi wanakiri hawawatambui watu hao ila watawakamata.

Maswali ya kujiuliza.

1. Hao watu wenye Ujasiri wa kukamata (kumteka) mtu kwa nguvu Mchana kweupe wakiwa na pingu kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi.Ni watu gani hawa?

2. Kwanini wakati wanamkamata (kumteka) walikuwa wanatamka "Twende Gogoni" ambapo Gogoni ni kituo cha Polisi Kilichopo Kiluvya, Wilaya ya Ubungo- Dar kama sio Polisi na kama hawana uhusiano na Polisi. Ni watu gani hawa?

3. Kwanini wakati wanamkamata (Kumteka) watamke kwa nguvu kwamba sisi ni Askari, sisi ni Askari? Ikiwa Polisi kupitia taarifa yao wamewakana kwamba hawawajui. Ni watu gani hawa wana Ujasiri kujitambulisha kama wao ni Polisi ikiwa sio Polisi?

4. Ikiwa ukamataji ulikuwa na nia njema kama sio Kumteka,kwanini baada ya kuzidiwa nguvu waliamua kumuacha na pingu mkononi na kukimbia huku wakisema tutakukafuata. Kwanini wakimbie? Kama sio Polisi. Ni watu gani hawa?

Kuongezeka kwa vyombo vya ukamataji tofauti na vyombo 3 kisheria ni sababu kubwa ya haya matukio kutokokea. Vyombo 3 kwa mujibu wa Sheria vyenye mamlaka ya kukamata, kupekua na kupeleleza ni POLISI, TAKUKURU na UHAMIAJI. Na ambapo ukikamatwa na Polisi unapelekwa kituo cha Polisi, ukikamatwa na Uhamiaji unapelekwa uhamiaji, Ukikamatwa na TAKUKURU unapelekwa TAKUKURU.

Mwaka 2023 kulifanyika marekebisho ya Sheria ya Usalama wa Taifa ambapo kifungu cha 4(3) kikaruhusu Afisa wa Usalama wa Taifa kukamata mtu. Na haijulikani wapi anakupeleka. Sheria hii imeongeza mwanya wa matukio ya utekaji, inawezekana aidha kifungu cha Sheria hii kinatumika vibaya au kuna kikundi cha wahuni kinatumia mwanya wa Sheria hii kwa maslahi binafsi.

Pia Polisi kutofuata Sheria na taratibu za ukamataji, kumeongeza mwanya wa matukio haya Sababu imekuwa ni ngumu kujua nani ni Polisi nani sio Polisi. Police wameamua kupuuza utawala wa Sheria (Rule Of Law ) kupitia Sheria zinazowaongoza katika majukumu Yao ya kila siku kama, Police Force and Auxiliary Service Act, Cap 322 R.E 2002, Criminal Procedure Act, Penal Code na Police General Order. Sheria zote hizi kama Police wangekuwa wanaziheshimu na kuzifuata zingetofautisha Polisi na watu wengine. Wahuni wengine wasinge kuwa na uwezo wa kujitambulisha kama ni Polisi ikiwa sio Polisi.

View attachment 3150874View attachment 3150875
View attachment 3150876
Hii nchi inavuja...
 
Kama hawa ni, TISS, basi, hii, nchi ipo uchi kabisa, watu wanna, wanashindwa ku kidnap mtu mmoja! Hapo, ilibidi awekewe kitambaa cha dawa ya usingizi puani,apoteze fahamu!
Hakuna weredi kabisa,
Hz mbinu zinatumika sana hata kule Kenya, Ila jamaa wanakuja wamefunika nyuso.
Umeamua kuwapa kabisa elimu ya utekaji ...
 
Jamaa hataki kuingilia kabisa yasiyo muhusu
Screenshot_20241113-090225_1.jpg
 
Hakuna Mtanzania asiyeigopa serikali.
Awe mwana masumbwi, awe tajiri, awe maskini au tajiri.
Hakuna Mtanzania wa kumpiga pingu Mtanzania mwenzake mchana mbele ya watu kama si wakala wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Tusipepese macho wale watekaji ni government agents. Kama si government agents basi ndani ya masaa 12 tu baada ya video kuvuja tayari nisikie wako selo wananyea ndoo.
Swali langu: Kwanini walimwacha baada ya kuona mambo si mambo?
Je, serikali inaweza kumshindwa raia mhalifu?
Askari anaruhusiwa kutumia silaha kupunguza nguvu ya mtuhumiwa endapo mtuhumiwa atakuwa mkaidi au kupambana na askari , je, kwanini hawakutumia silaha?
 
Back
Top Bottom