Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Wakuu,
Bado sijarejea rasmi hapa jamvini ila nipende tu kuwataarifu kuwa nipo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku.
Siku kadhaa zilizopita ndipo nilipokutana na msukosuko wa aina yake.
Ilikua siku ya jumapili nikiwa najiandaa kwenda ibadani, nikaona nipitie kwenye moja ya mgahawa maarufu hapa mjini ambao kwa kweli pale mimi huwa ni regular customer na huwa nina wahudumu wawili ambao hao ndio tumezoeana sana.
Sasa siku hiyo ya tukio akanipokea mhudumu kama kawaida yake kwa tabasamu pana na salamu.
Nikaagiza kifungua kinywa.
Wakati natafuna nimeze lahaula nasikia vitu vikivunjikia mdomoni, nikaona niteme looh natoa mdomoni vipande vya chupa na ili kuhakiki kama kile kilikuwa chupa nikaona nikiminye nikaishia kukatwa mkono wangu.
Kuangalia ndani ya chakula looh, vyupa vimejaa.
Tangu siku hiyo ya tukio nikiwa mjini nakunywa maji tu. Mambo mengine yote nyumbani.
Wakuu kuweni makini sana na mii mgahawa na hakikisheni hamuwi wateja wa kudumu mahali.
Asanteni. Weekend njema.