Jaribio la kunidhuru limeshindikana ashukuriwe Mungu

Wakuu,

Bado sijarejea rasmi hapa jamvini ila nipende tu kuwataarifu kuwa nipo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku.

Siku kadhaa zilizopita ndipo nilipokutana na msukosuko wa aina yake.

Ilikua siku ya jumapili nikiwa najiandaa kwenda ibadani, nikaona nipitie kwenye moja ya mgahawa maarufu hapa mjini ambao kwa kweli pale mimi huwa ni regular customer na huwa nina wahudumu wawili ambao hao ndio tumezoeana sana.

Sasa siku hiyo ya tukio akanipokea mhudumu kama kawaida yake kwa tabasamu pana na salamu.

Nikaagiza kifungua kinywa.

Wakati natafuna nimeze lahaula nasikia vitu vikivunjikia mdomoni, nikaona niteme looh natoa mdomoni vipande vya chupa na ili kuhakiki kama kile kilikuwa chupa nikaona nikiminye nikaishia kukatwa mkono wangu.

Kuangalia ndani ya chakula looh, vyupa vimejaa.

Tangu siku hiyo ya tukio nikiwa mjini nakunywa maji tu. Mambo mengine yote nyumbani.

Wakuu kuweni makini sana na mii mgahawa na hakikisheni hamuwi wateja wa kudumu mahali.

Asanteni. Weekend njema.
Poleee asee kamanda stroke
 
Mimi huwa siwaamini walokole kwani kila siku watesi wao hutaka kuwaangamiza, ona sasa mlokole huyu amekuja na hadithi ileile.
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Pole Sana Mkuu
 
Mimi huyo juzi,, nilivamiwa usiku
IMG-20211005-WA0026.jpeg
 
Nilikunywa juise ya Nana's kwenye kitoroli kariakoo tumbo lilianza kureact palepele kwa kupiga ngurumo kama za radi na ziliendelea kwa siku hiyo Hadi kesho yake, nahisi lilikuwa jaribio Kali sana la kuniondoa kabisa
 
Ni kweli, nishakutana na paper clip kwenye kitumbua na mara nyengine tena kwenye kitumbua nakutana na shanga daah!, mwenyeezi mungu ni mkubwa.
Vitumbua huwa vinapikwa uchi na kanga moja so possible
 
Thread ifungwe! Umemaliza kila kitu, hana adui ali serious kumuua. Muuaji hawezi kutumia mbinu mbovu hivyo huyu jamaa kungekua na mtu anataka uhai wake saiv title yake ingesoma R.I.P na tungepitisha rambirambi humu, binadamu wabaya sana.

Pole yake lakini kwa huo mkasa.
So jamaa anataka uhai wake sema Mungu,hakuna mtu yeyeto mwenye kuweza kuua mtu pasipo ruhusa ya Mungu.Lisu case study
 
Hii ni tofauti mkuu, vyupa vinatoka wapi kwenye supu, ingekuwa kinywaji hapo sawa useme labda chupa imevunjika bahati mbaya wakati wa kufungua, hiyo ilikusudiwa.

Ni kuongeza umakini. hali si hali binadamu hawaaminiki tena.
Pole mkuu! Kazi za watu wasiojulikana hizo!
 
Wakuu,

Bado sijarejea rasmi hapa jamvini ila nipende tu kuwataarifu kuwa nipo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku.

Siku kadhaa zilizopita ndipo nilipokutana na msukosuko wa aina yake.

Ilikua siku ya jumapili nikiwa najiandaa kwenda ibadani, nikaona nipitie kwenye moja ya mgahawa maarufu hapa mjini ambao kwa kweli pale mimi huwa ni regular customer na huwa nina wahudumu wawili ambao hao ndio tumezoeana sana.

Sasa siku hiyo ya tukio akanipokea mhudumu kama kawaida yake kwa tabasamu pana na salamu.

Nikaagiza kifungua kinywa.

Wakati natafuna nimeze lahaula nasikia vitu vikivunjikia mdomoni, nikaona niteme looh natoa mdomoni vipande vya chupa na ili kuhakiki kama kile kilikuwa chupa nikaona nikiminye nikaishia kukatwa mkono wangu.

Kuangalia ndani ya chakula looh, vyupa vimejaa.

Tangu siku hiyo ya tukio nikiwa mjini nakunywa maji tu. Mambo mengine yote nyumbani.

Wakuu kuweni makini sana na mii mgahawa na hakikisheni hamuwi wateja wa kudumu mahali.

Asanteni. Weekend njema.
Tutaiaminije story yako, ulimdhulumu mhudumu huyo, au unafikiri msukosuko ulitokana na Nini, auhuishi vizuri na watu au, tupe ufafanuzi tafadhali angalao uwafunze na wengine.
 
Pole bwana stroke sisi tukajua huo ugonjwa Kwenye I'd Yako umekupiga mpaka unashindwa zama humu
Ni kweli Muda kidogo nilikua sijaona I'd Yako ikitoa michango kumbe ulipatwa makubwa
Daaa Makinika Sana mkuu maadui hawatoki mbali Aisee
Ninesikitika Sana!
Ushauri kama anaishi na jamii vibaya abadilike.
 
Pole Sana na ukatoe sadaka kumshukuru Mungu ulivyookoka na hatari
 
Back
Top Bottom