Yericko Nyerere,
..ur of the mark katika madai yako kwenye post # 4.
..mfano: Hans Pope hakuwahi kuwa Maj Gen. Pia alipatikana na hatia ya makosa ya uhaini na kufungwa jela.
..pia komandoo aliyeuawa alijulikana kwa jina la mohamed tamim, lakini hakuuawa ktk mapambano toka airport mpaka kinondoni.
..kumbukumbu zako ni sawa na zako kuhusu idadi ya majaribio kuwa ni matatu. jaribio la kwanza, na serious kupita yote kwa mtizamo wangu, ni la 1964. jaribio la pili ni la miaka ya 1970 ambalo lilihusisha wanajeshi, wanasiasa kama Kamaliza,Chipaka, etc inasemekana hawa walijaribu kuhusisha wapiganaji wa vyama za ukombozi. Inasemekana jaribio hili la pili lilikuwa na mkono wa Oscar Kambona. jaribio # 3, liliwahusisha wakina Lugangira,Hatibu Gandhi, Zacharia Hans Pope, etc etc.
@Mzee Mwanakijiji,
..serikali ya Mwalimu Nyerere ilichelewa ktk utekelezaji wa zoezi la Africanization kwa upande wa jeshi.
..hiyo ilipelekea askari wa ngazi za NCO kuanza vurugu za kuwakataa maofisa wa Kizungu waliokuwa wakiongoza jeshi.
..kiongozi wa maasi hayo alikuwa Sgt.Hingo Ilogi. sasa kuna wakati Sgt.Hingo Ilogi na wenzake walikwenda mpaka Ikulu kwa nia ya "kuonana" na Mwalimu Nyerere.
..inasemekana walipofika[Hingo Ilogi & Co] ikulu walikutana na aliyekuwa mkuu wa usalama wa taifa, Emilius Mzena, ambaye alitumia ujanja na kuwadanganya kwamba Mwalimu alikuwa hayuko Ikulu. kuna wanaodai kitendo cha Mzena ndiyo kilimuokoa Mwalimu kwasababu maana baada ya hapo alipelekwa mafichoni.
..kwa mtizamo wangu, askari toka Uingereza ndiyo waliookoa jahazi, vinginevyo tungekuwa tunaongea habari nyingine kabisa hapa.
NB:
..kuna mwana JF anaitwa
Shwari, huyu huwa ni msaada mkubwa sana ktk masuala ya kihistoria kama haya.