Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Jaribio la kutaka kuiangusha serikali ya Nyerere 1982/1983

Charles Kizigha anapaswa aandike kitabu, mimi nilimsoma nikiwa chuo cha journalism TSJ, aliripoti kutekwa kwa ndege ya ATC, ndie mwandishi wa kwanza na labda wa pekee nchini Tanzania niliyemfahamu mimi, kumiliki gari brand new kutoka show room, alimiliki gari ya Musso new brand kutoka dukani!, waandishi wengine wote gari zetu ni used, ila sijui kwa waandishi wadada, maana wenzetu hawachelewi kununuliwa magari na ma source!.
P
Nilisikia pia kwamba Kizigha aliokota na kuvikusanya vikaratasi kadhaa vya propaganda ya Oscar Kambona uwanja wa taifa na alishughulikiwa na Usalama wa Taifa. Lakini sikuwahi kumuuliza kuhusu jambo hilo.

Halihusu kesi ya uhaini au alichofanya au hakufanya uwanja wa taifa lakini Kizigha pia alikuwa rafiki wa karibu sana na Abdallah Ngororo na Harold Nsekela tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini. Nilifahamiana sana na hao wote. Mara nyingi walikuwa katika gari la Ngororo, Peugeot 404 nyeupe, mwaka 1972 na baada ya hapo. Miake ile, Harold Nsekela alikuwa anafundisha sheria chuo kikuu, UDSM; Kizigha na Ngororo walikuwa waandishi wa habari pamoja, Daily News.
 
Ndugu Pascal,

Sijui kwa nini mpaka sasa Kizigha hajaandika kitabu. Anajua mambo mengi sana tangu enzi ya Mwalimu Nyerere. Najua huo ndiyo ukweli kwa sababu yeye si mgeni kwangu na mimi siyo mgeni kwake. Tumetoka mbali sana pamoja. Tumefahamiana zaidi ya miaka arobaini na tano - itakuwa miaka hamsini hivi karibuni - pamoja na Makwaia wa Kuhenga na wengineo. Ila sijui kama nitafanikiwa kumshawishi Kizigha aandike kitabu. Labda wewe na wengine mjaribu kufanya hivyo.

Pia jaribuni kuwashawishi wengine - Jenerali ulimwengu, Kassim Mpenda, Ulli Mwambulukutu, Makwaia wa Kuhenga na wengineo - wafanye hivyo. Nimefahamiana nao kwa miaka mingi sana. Wanajua mengi na wana uwezo mkubwa sana wa kuandika. Mwingine ni Karl Lyimo ingawa sifahamiani naye. Lakini ni mwandishi mwenye uwezo mkubwa sana na ametoka mbali sana na taifa letu kuliko waandishi wengi sana nchini mwetu.
 
unajua kitu cha kwanza ambacho academics wetu wangepigania ni kufunguliwa kwa classified materials ambazo zilikuwa zinazuiwa hadi ipite miaka 30. Karibu nyaraka zote za kati ya 1961 hadi sasa zimeshapita huo muda na zinatakiwa kisheria ziwekwe huru kwa wasomi kupitia. Nyaraka zote kuhusiana na uhuru, mapinduzi, muungano, n.k .. vinatakiwa viwe kwenye public domain sasa. But.. I said our academics.. sijui kama bado wapo...
Nadhani umesahau kuwa wizara ya mambo ya ndani iliteketea kwa moto siku za mwisho mwisho za awamu ya kwanza. Halikadhalika BOT.
 
Ndugu Pascal,

Sijui kwa nini mpaka sasa Kizigha hajaandika kitabu. Anajua mambo mengi sana tangu enzi ya Mwalimu Nyerere. Najua huo ndiyo ukweli kwa sababu yeye si mgeni kwangu na mimi siyo mgeni kwake. Tumetoka mbali sana pamoja. Ila sijui kama nitafanikiwa kumshawishi aandike kitabu. Labda wewe na wengine mjaribu kufanya hivyo.
Loh !! hilo wazo mimi nilikuwa nalo wakati akina Mama wanasherehekea sherehe zao za miaka 50.

Kifupi nilitaka nimwambe Pascal aandike kitabu kinachhlhusu akina mama Wenye Mchango mkubwa hapa TZ bila Kujali vyama au mapungufu yao kama binadamu
Ila nilikuwa sijui nitampelekeaje ujumbe.

Mimi sio mwandishi..

Mfano.

Bibi Titi
Anna Makinda
T. Siwale
Anna Abdallah
Tibaijuka
K.Kamba
Sophia Kawawa
N.k

Akina mama wapo walio chomoza na kufanya makubwa tu.
Inaelekea pamoja na kukwepa hivi vitabu vinahitaji mchango wa P kwa namna moja au nyingine.
 
Mkuu Wakurochi, japo wanahabari wote tunaitwa waandishi wa habari, lakini ndani ya waandishi kuna specialization, wengine ni waandishi maripota wa habari, wengine ni wachambuzi wa habari, wengine ni watangazaji, wengine ni wapiga picha, kuna ma producers etc. Kazi ya kuandika biography ni specialized sio kila mtu anaweza, mimi nimejikita kwenye utangazaji na digital production, Kutengeneza vipindi, hivyo kwa upande wangu natakiwa ku document kwa kufanya nao mahojiano nitayarishe vipindi. The right person wa kufanya haya ni mwana JF Mkuu Maalim Mohammed Said, ila sijui kama Maalim atakubali kuandika history ya watu fulani fulani aombwe tuu akatae mwenyewe.

Kaka yngu umeanza vzuri mwisho umekosea kwa nn unasema Mzee Mohamed Said awezi kkubari kuandika khs watu fulani fulani bila shaka umelenga upande wa pili ila umesahau Mzee Mohamed Said ameandika mara nyingi khs Mzee John Rupia Khs Chief Makwahiya wa Sia Nk sie ndugu kaka yngu Yule Mama alie kuwa mwenye nyumba yko pale Ilala Pamoja na kuwa upande wa pili lkn alikuwa Mama yetu mwenzetu kwa hali zote kumbuka msiba kijana wake na Mzee pia sie Swahili au upande pili tulikuwa wengi na pamoja nae km mwenzetu...
 
Nilisikia pia kwamba Kizigha aliokota na kuvikusanya vikaratasi kadhaa vya propaganda ya Oscar Kambona uwanja wa taifa na alishughulikiwa na Usalama wa Taifa. Lakini sikuwahi kumuuliza kuhusu jambo hilo.

Halihusu kesi ya uhaini au alichofanya au hakufanya uwanja wa taifa lakini Kizigha pia alikuwa rafiki wa karibu sana na Abdallah Ngororo na Harold Nsekela tangu mwanzoni mwa miaka ya sabini. Nilifahamiana sana na hao wote. Mara nyingi walikuwa katika gari la Ngororo, Peugeot 404 nyeupe, mwaka 1972 na baada ya hapo. Miake ile, Harold Nsekela alikuwa anafundisha sheria chuo kikuu, UDSM; Kizigha na Ngororo walikuwa waandishi wa habari pamoja, Daily News.
Umenikumbusha Abdalah Ngororo alikuwa Mkurugenzi wangu RTD, nilijiunga enzi za David Wakati (RIP), enzi hizo hali ulikuwa ngumu sana kwa Watangazaji, akaja Nkwabi Ngwanakilala (RIP), akafanya transformation kubwa kwa mazingira ya kazi, watu wakaanza kulipwa overtime na allowances nene nene, TBC ikaanzisha FM, watangazaji vijana tukawa tunalipiwa decent housing, kabla ya hapo Watangazaji walipanga vyumba nyumba za kupanga uswazi, tukapangiwa flats Ilala Shariff Shamba (Ostabei ya Ilala). Mkwabi alitambua vipaji na utalipwa kutokana na jasho lako, uwezo wako na kipaji chako, watangazaji vijana tukaanza kuvuta pesa ndefu.

Alipokuja Ngororo, this is a man of principles akairudisha ile RTD ya David Wakati, wafanyakazi wote wawe treated equally hakuna cha wenye vipaji wala wafanyakazi wa kuvuta allowances ndefu, hapo ndipo kukatokea mass exodus ya watangazaji zaidi ya 15 kutimka kwa mpigo akiwamo Mikidadi Mahmood, Charles Hillary, Uncle J, Julius Nyaisangah, Betty Mkwasa, Ahmed Kipozi, Aboubakar Liongo, John Mdolwa, Abdallah Majura, Vicky Msina, Flora Nducha na wengine.

Sikumbuki hata alidumu kwa muda gani pale.

P
 
Kaka yngu umeanza vzuri mwisho umekosea kwa nn unasema Mzee Mohamed Said awezi kkubari kuandika khs watu fulani fulani bila shaka umelenga upande wa pili ila umesahau Mzee Mohamed Said ameandika mara nyingi khs Mzee John Rupia Khs Chief Makwahiya wa Sia Nk sie ndugu kaka yngu Yule Mama alie kuwa mwenye nyumba yko pale Ilala Pamoja na kuwa upande wa pili lkn alikuwa Mama yetu mwenzetu kwa hali zote kumbuka msiba kijana wake na Mzee pia sie Swahili au upande pili tulikuwa wengi na pamoja nae km mwenzetu...
Mkuu Rubawa, usichanganye kuwataja na kuandika, sijui labda kama ni mimi tuu ndio namsoma kwa jicho tenge, concentration yake mchango wa Baba na Babu zake wa upande ule, lakini kwenye shida na raha tunashirikiana vizuri tuu. Naomba reference ya andiko lake kuhusu mchango wa yeyote wa upande wa pili.
P
 
Mkuu Wakurochi, japo wanahabari wote tunaitwa waandishi wa habari, lakini ndani ya waandishi kuna specialization, wengine ni waandishi maripota wa habari, wengine ni wachambuzi wa habari, wengine ni watangazaji, wengine ni wapiga picha, kuna ma producers etc. Kazi ya kuandika biography ni specialized sio kila mtu anaweza, mimi nimejikita kwenye utangazaji na digital production, Kutengeneza vipindi, hivyo kwa upande wangu natakiwa ku document kwa kufanya nao mahojiano nitayarishe vipindi. The right person wa kufanya haya ni mwana JF Mkuu Maalim Mohammed Said, ila sijui kama Maalim atakubali kuandika history ya watu fulani fulani aombwe tuu akatae mwenyewe.
P
OK, Asante kwa kunielewesha. Ila M. Said
Kwenye mizani imekataa ingawa habari zake si haba humu
Unajua hata wapishi wakipakua wanaweka chumvi kiasi ila wanaleta kichupa kia mtu aongeze kiasi chake.
Huyu M. Said yeye kama mpishi anaweka chumvi kolea kwa kipimo chake yeye.

Lakini niishie hapa hii sio mahali pake
 
Kwa Pascal unamaanisha huyu Pascal Mayalla ? Huyu ndiye aandike kitabu?

Usitake ncheke. Ataanzia wapi kuandika kuhusu watu hao?

Nnakuhakikishia huyo hana uwezo huo. Tunamuona anavyoandika humu. Huyo ni mwandishi wa vi "article" uchwara vyenye ufataani usio na mithili.
 
OK, Asante kwa kunielewesha. Ila M. Said
Kwenye mizani imekataa ingawa habari zake si haba humu
Unajua hata wapishi wakipakua wanaweka chumvi kiasi ila wanaleta kichupa kia mtu aongeze kiasi chake.
Huyu M. Said yeye kama mpishi anaweka chumvi kolea kwa kipimo chake yeye.

Lakini niishie hapa hii sio mahali pake
Weka ushahidi wa uliyoandika kuhusu Allama Mohamed Said maana huwezi isifia chumvi kama hujaionja. Tuoneshe hiyo chumvi aliyoizidisha iko wapi?

Ukishindwa basi wewe ni muongo.
 
Mkuu Rubawa, usichanganye kuwataja na kuandika, sijui labda kama ni mimi tuu ndio namsoma kwa jicho tenge, concentration yake mchango wa Baba na Babu zake wa upande ule, lakini kwenye shida na raha tunashirikiana vizuri tuu. Naomba reference ya andiko lake kuhusu mchango wa yeyote wa upande wa pili.
P
"Upande wa pili" ndiyo upi?
 
Labda Ngororo alidumu RTD muda mfupi kuliko gazetini, Daily News, ambako alikuwa news editor baada ya muda mfupi tu kutoka UDSM ambako nadhani alisomea literature, kama nilivyowahi kusikia. Pia nilisikia kwamba Mwalimu Nyerere alimpenda sana Abdallah Ngororo. Hazikuwa porojo. Niliowasikia wakisema hivyo walikuwa karibu na viongozi kadhaa serikalini. Hawakuwa wananchi wa kawaida kama mimi. Mwalimu alimwamini ingawa bado alikuwa kijana. Baadaye nilisikia pia hivyo kuhusu Jenerali Ulimwengu.

Inasemekana pia kwamba Mwalimu Nyerere alimpenda sana Salim Ahmed Salim tangu alipokuwa kijana. Alitaka hata awe raisi baada ya yeye kung'atuka.

Lakini si hao tu. Kuna wengine, pia wengi. Muhimu ni sifa, uwezo, na uzalendo. Kwa mfano, ndiyo maana umesema kuhusu Ngororo: “Alipokuja Ngororo, this is a man of principles akairudisha ile RTD ya David Wakati, wafanyakazi wote wawe treated equally.”

Mfano mwingine ni Salim Ahmed Salim. Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi tangu alipokuwa kijana, kuanzia ubalozi, wakati vijana wengi wenye umri wake walikuwa bado shuleni. Mwalimu Nyerere hakukosea.

Kuna senior diplomat mmoja ninayemfahamu sana na ambaye alikuwa anafanya kazi na Salim Ahmed Salim ubalozi wetu Umoja wa Mataifa. Tulikuwa ni sisi wawili tu, tunazungumza. Alimzidi Salim umri na elimu lakini alisema ingawa Salim hana elimu ya juu, wakati ule, kama wenzake anaofanya kazi nao ubalozi wetu, “He is an excellent ambassador.” Hayo ndiyo maneno yake.

Aliendelea kumsifu sana na kusema Salim ni kiongozi mwenye uwezo mkubwa sana. Nilikutana pia na Salim wakati ule. Alikuwa na umri wa miaka thelathini tu lakini alikuwa anaheshimiwa sana Umoja wa Mataifa na katika nchi mbalimbali.

Pia balozi mmoja wa Marekani nchini Tanzania, Richard N. Viets, alisema yafwatayo kuhusu Salim:

“I found Salim Salim...to be a very, very bright, interesting man whose revolutionary zeal had long since cooled."

Balozi mwingine wa Marekani, John W. Shirley, alisema:

“It was as intellectually stimulating to deal with him (Nyerere), as it was to deal with Prime Minister Salim Salim.”

Wasingemchafua, angekuwa raisi wetu wa kujivunia.

Mara nyingi, kuna nyakati najiuliza taifa letu linakwenda wapi ingawa tumekuwa na sifa duniani ya kutokuwa na ubaguzi kama nchi nyingi za Kiafrika.

Kuna hata Watanzania wanaojisifu na kujiona bora kuliko wananchi wenzao kwa sababu wanatoka makabila fulani au ukanda fulani. Huo ndiyo msingi wa nchi yenye umoja na amani?

Enzi ya Mwalimu Nyerere, tulikuwa hatuulizani makabila yetu, ukanda wetu, asili yetu au dini zetu. Tulijenga taifa based on individual rights, not one based on group rights or tribal and racial identities.
 
Back
Top Bottom