Shughuli za magendo na zisizotozwa kodi sasa zinachangia asilimia 11.8 ya Pato la Taifa Duniani (GDP), ikiwa ni punguzo kutoka asilimia 17.7 mwaka 2000, lakini bado zinawakilisha thamani ya kiuchumi ya matrillion ya Shilingi.
Uchumi wa kivuli (Shadow Economy) unajumuisha aina mbalimbali za miamala isiyo rasmi, kuanzia ajira zisizotambulika rasmi hadi shughuli za uhalifu wa kupanga.
Uchumi wa kivuli au unaweza kuita Uchumi haramu, unaojulikana pia kama uchumi wa chini ya ardhi (Underground Economy, uchumi usio rasmi (Informal Economy), au soko la giza (Black Market), unahusisha shughuli za kiuchumi zinazofanyika nje ya mifumo rasmi na iliyodhibitiwa na serikali. Shughuli hizi mara nyingi huepuka ushuru, huepuka udhibiti, au ufuatiliaji, na mara nyingi ufanyika sambamba au pamoja na njia za uchumi rasmi.
Sifa za Uchumi wa Kivuli (Shadow Economy):
1. Ukwepaji Kodi: Washiriki mara nyingi huepuka kulipa kodi, jambo linalovutia wale wanaotafuta faida kubwa.
2. Kukwepa Udhibiti au kukaguliwa: Shughuli hizi zinaweza kupuuza au kukwepa sheria za kazi, sheria za mazingira, au viwango vingine vya kisheria.
3. Ukosefu wa Nyaraka: Shughuli hizi nyingi hufanywa kwa pesa taslimu au kubadilishana bidhaa ili kuepuka rekodi zinazoweza kufuatiliwa na mamlaka.
4. Sifa nyinginezo: Uchumi huu unajumuisha kila kitu kutoka kwa wauzaji holela wa mtaani, biashara zisizosajiliwa, na biashara ya dawa za kulevya hadi kazi za malipo ya mezani au mikononi kutoka au kwenda kwa wataalamu.
Mifano wa 1: shughuli Halali Lakini Zisizodhibitiwa kama wauzaji wa mtaani wasio na vibali vya biashara au wasiosajiliwa au Kazi za malipo ya mkononi zisizoripotiwa au kufuatiliwa (mfano, shule za majumbani, ukarabati wa nyumba usiofuata mipango ya jiji).
Mfano wa 2. Shughuli Haramu kama biashara ya dawa za kulevya, uuzaji wa bidhaa bandia, utoroshaji madini, umiliki na uuzaji wa silaha za kivita na magendo haramu ya aina yoyote.
Athari:
1. Athari za Kiuchumi: Kupungua kwa mapato ya serikali kutokana na ukwepaji wa kodi. Na pia ushindani usio wa haki kwani biashara zisizo rasmi zinaweza kutoa bei za chini kwa kuepuka gharama kama kodi au kufuata sheria.
2. Athari za Kijamii: Ukosefu wa ulinzi kwa wafanyakazi (mfano, hakuna bima ya afya au msaada wa kisheria endapo mfanyakazi atapata shida za zinazohitaji msaada wa kisheria). Pia uwekezaji mdogo katika miundombinu na huduma za umma kutokana na kupoteza mapato ya kodi.
View attachment 3348936
Tanzania inashika nafasi ya 7 Duniani kwa kuwa na Uchumi Haramu au Uchumi Kivuli, ikiwa na zaidi ya asilimia 44.7% ya uchumi haramu au uchumi kivuli unaopotea kutoka kwenye Pato la Taifa (GDP). Ambapo ni karibia nusu ya Pato la Taifa linapotea kwenye Biashara Haramu au Uchumi Kivuli (Shadow Economy)
Sierra Leone inaongoza, ikiwa na uchumi wa kivuli unaofikia asilimia 64.5 ya GDP. Nchi hiyo ni mfano wa mwenendo mpana zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako ajira isiyo rasmi—ambayo mara nyingi hupatikana katika kilimo, biashara za mtaani, na biashara ndogo ndogo—hutumika kama sekta ya ajira ya kawaida kutokana na upatikanaji mdogo wa kazi za rasmi.
Marekani ina uchumi wa kivuli wa wastani wa asilimia 5% ya GDP. Kutokana na ukubwa wa uchumi wa Marekani, takwimu hiyo inawakilisha wastani wa dola trilioni 1.4, na kuiweka kati ya nchi zenye uchumi wa kivuli mkubwa zaidi duniani kwa viwango vya jumla. @WorldVisualized
Chanzo: Ripoti ya Uchumi wa Kivuli Duniani ya Ernst & Young 2025