Jarida la World Visualized Limetoa Takwimu Za Nchi 10 zenye kuongoza kwa Uchumi Haramu (Shadow Economy), Tanzania yashika nafasi ya 7 Duniani

Jarida la World Visualized Limetoa Takwimu Za Nchi 10 zenye kuongoza kwa Uchumi Haramu (Shadow Economy), Tanzania yashika nafasi ya 7 Duniani

Mkuu hapo wanaangalia anayepoteza si anayeingiza.

Huenda Rwanda wanachukua toka DRC lakini pengine vya kwao vinasimamiwa vizuri kuhakikisha taifa linafaidika.
Asante... umemuelewesha vyema
 
Kutoa Nje na kuleta ndani ni kuongeza pato la nchi au uchumi wa Nchi... Rwanda haiwezi kuongoza kwa sababu haifanyi Magendo kupeleka pesa nje ya nchi, Pesa ya Rwanda inabaki ndani ya nchi kwenye mzunguko wa serikali....

Mbona hujiulizi hiyo DRC unayoizungumzia imetajwa hapo sambamba na Tanzania.... DRC uchumi wake hauingii kwenye mzunguko wa serikali, kule watu wanafanya biashara haramu, wanakwepa kodi, biashara za magendo, wizi, utoroshaji wa madini... viongozi wao wanapeleka pesa nje ya nchi na mambo mengi ndio maana unakuta licha ya kuwa Tajiri kwa rasimali bado ni Nchi masikini duniani....

Rwanda sheria zinafatwa, watu wanalipa kodi, biashara zimesajiliwa, magendo hayatoki ndani kwenda nje, Kagame kaweka mifumo rafiki kwa wafanya biashara na makampuni... japo kama nchi haiwezi kuwa bora kila nyanja, lazima Shadow Economy iwepo ila haiwezi kulingana na DRC
Huu ufafanuzi wako ni mzuri.
 
Wewe na kichwa lako ni mgumu kulewa..., mimi hapo nazungumzia shadow economy, sizungumzii nani ana biashara gani au nani ana Milioni 4.... mbona nimefafanua hapo maana ya shadow economy zikiwemo Biashara Haramu, wakwepa Kodi, biashara za magendo na kadharika...

Wewe unataka mpaka nikuwekee kiwango cha mtu anayetakiwa kuanza kulipa kodi kwenye Biashara, hiyo sio kazi yangu... Nenda TRA ukapewe Elimu ya kodi... sijaweka icho kiwango kwa sababu kila nchi ina sheria zake na viwango vyake...

Mimi nazungumzia Shadow Economy kwa ujumla, ambayo pia kwa sheria zilizowekwa Tanzania mtu akizivunja anaonekana kama anafanya Shadow Economy

- “unahusisha shughuli za kiuchumi zinazofanyika nje ya mifumo rasmi na iliyodhibitiwa na serikali”

- “Uchumi wa kivuli (Shadow Economy) unajumuisha aina mbalimbali za miamala isiyo rasmi, kuanzia ajira zisizotambulika rasmi”

- “uchumi usio rasmi (Informal Economy), au soko la giza (Black Market), unahusisha shughuli za kiuchumi zinazofanyika nje ya mifumo rasmi na iliyodhibitiwa na serikali.”

Kwa maelezo yako hapo juu, Muuza maembe , wabeba zege kwahiyo hawapo humo kwenye mnachoita mifumo isiyo rasmi (Shadow economy)?
 
Uenda wanamiliki madawa ila hawakwepi kodi na wanafuata sheria za nchi ambazo mwisho wa siku zinaficha udhaifu wa uchumi na pesa inabaki nchini au kwenye mzunguko wa serikali yani serikali inakuwa na pesa... hizo nchi ulizotaja kama Brazili ni nchi Tajiri kwenye Pato la Nchi na Pato la mtu mmoja, na hazipo kwenye orodha ya nchi masikini

Afrika japo hakujashamili madawa ya kulevya, ila biashara za magendo, uhujumu uchumi, wizi wa madini, Ujangili na mambo mengine ndio nyumbani kwake... ukiangalia Top 10 ya nchi maskini Duniani nyingi zinatoka Afrika, huku Afrika watu wachache wanapiga pesa kisha pesa hizo zinasafirishwa nje ya nchi, watu wanafanya biashara wanakwepa kodi na ndio maana mwisho wa siku serikali unakuta haina pesa za kuleta maendeleo... na hiyo ndio Shadow Economy
ok
 
Shughuli za magendo na zisizotozwa kodi sasa zinachangia asilimia 11.8 ya Pato la Taifa Duniani (GDP), ikiwa ni punguzo kutoka asilimia 17.7 mwaka 2000, lakini bado zinawakilisha thamani ya kiuchumi ya matrillion ya Shilingi.

Uchumi wa kivuli (Shadow Economy) unajumuisha aina mbalimbali za miamala isiyo rasmi, kuanzia ajira zisizotambulika rasmi hadi shughuli za uhalifu wa kupanga.

Uchumi wa kivuli au unaweza kuita Uchumi haramu, unaojulikana pia kama uchumi wa chini ya ardhi (Underground Economy, uchumi usio rasmi (Informal Economy), au soko la giza (Black Market), unahusisha shughuli za kiuchumi zinazofanyika nje ya mifumo rasmi na iliyodhibitiwa na serikali. Shughuli hizi mara nyingi huepuka ushuru, huepuka udhibiti, au ufuatiliaji, na mara nyingi ufanyika sambamba au pamoja na njia za uchumi rasmi.

Sifa za Uchumi wa Kivuli (Shadow Economy):

1. Ukwepaji Kodi: Washiriki mara nyingi huepuka kulipa kodi, jambo linalovutia wale wanaotafuta faida kubwa.

2. Kukwepa Udhibiti au kukaguliwa: Shughuli hizi zinaweza kupuuza au kukwepa sheria za kazi, sheria za mazingira, au viwango vingine vya kisheria.

3. Ukosefu wa Nyaraka: Shughuli hizi nyingi hufanywa kwa pesa taslimu au kubadilishana bidhaa ili kuepuka rekodi zinazoweza kufuatiliwa na mamlaka.

4. Sifa nyinginezo: Uchumi huu unajumuisha kila kitu kutoka kwa wauzaji holela wa mtaani, biashara zisizosajiliwa, na biashara ya dawa za kulevya hadi kazi za malipo ya mezani au mikononi kutoka au kwenda kwa wataalamu.

Mifano wa 1: shughuli Halali Lakini Zisizodhibitiwa kama wauzaji wa mtaani wasio na vibali vya biashara au wasiosajiliwa au Kazi za malipo ya mkononi zisizoripotiwa au kufuatiliwa (mfano, shule za majumbani, ukarabati wa nyumba usiofuata mipango ya jiji).

Mfano wa 2. Shughuli Haramu kama biashara ya dawa za kulevya, uuzaji wa bidhaa bandia, utoroshaji madini, umiliki na uuzaji wa silaha za kivita na magendo haramu ya aina yoyote.


Athari:

1. Athari za Kiuchumi: Kupungua kwa mapato ya serikali kutokana na ukwepaji wa kodi. Na pia ushindani usio wa haki kwani biashara zisizo rasmi zinaweza kutoa bei za chini kwa kuepuka gharama kama kodi au kufuata sheria.


2. Athari za Kijamii: Ukosefu wa ulinzi kwa wafanyakazi (mfano, hakuna bima ya afya au msaada wa kisheria endapo mfanyakazi atapata shida za zinazohitaji msaada wa kisheria). Pia uwekezaji mdogo katika miundombinu na huduma za umma kutokana na kupoteza mapato ya kodi.

View attachment 3348936

Tanzania inashika nafasi ya 7 Duniani kwa kuwa na Uchumi Haramu au Uchumi Kivuli, ikiwa na zaidi ya asilimia 44.7% ya uchumi haramu au uchumi kivuli unaopotea kutoka kwenye Pato la Taifa (GDP). Ambapo ni karibia nusu ya Pato la Taifa linapotea kwenye Biashara Haramu au Uchumi Kivuli (Shadow Economy)

Sierra Leone inaongoza, ikiwa na uchumi wa kivuli unaofikia asilimia 64.5 ya GDP. Nchi hiyo ni mfano wa mwenendo mpana zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako ajira isiyo rasmi—ambayo mara nyingi hupatikana katika kilimo, biashara za mtaani, na biashara ndogo ndogo—hutumika kama sekta ya ajira ya kawaida kutokana na upatikanaji mdogo wa kazi za rasmi.

Marekani ina uchumi wa kivuli wa wastani wa asilimia 5% ya GDP. Kutokana na ukubwa wa uchumi wa Marekani, takwimu hiyo inawakilisha wastani wa dola trilioni 1.4, na kuiweka kati ya nchi zenye uchumi wa kivuli mkubwa zaidi duniani kwa viwango vya jumla. @WorldVisualized


Chanzo: Ripoti ya Uchumi wa Kivuli Duniani ya Ernst & Young 2025
Uchumi haramu chama dola tajiri.
 
Tanzania kuna informal sector kubwa sana mfano wamachinga, bodaboda, mama Ntilie hawa wote wanaoperate kwenye shadow economy

Angalia watu ambao wana bank account hawafiki hata million 5 hili ni tatizo kubwa sana, wanaolipa direct income tax wamepungua zaidi ya million alisema Philip mpango

Mimi nikiwa Rais ntahakikisha formal sector inakuwa dominant zaidi ya informal sector kwa sababu mbinu ninazo
Mkuu Share Hizo Mbinu Itakuwa Unyama Sana..
 
Tanzania kuna informal sector kubwa sana mfano wamachinga, bodaboda, mama Ntilie hawa wote wanaoperate kwenye shadow economy

Angalia watu ambao wana bank account hawafiki hata million 5 hili ni tatizo kubwa sana, wanaolipa direct income tax wamepungua zaidi ya million alisema Philip mpango

Mimi nikiwa Rais ntahakikisha formal sector inakuwa dominant zaidi ya informal sector kwa sababu mbinu ninazo
Wewe mwenyewe ulijitangaza winga! Vipi umesajiliwa? Unalipa kodi?
 
Back
Top Bottom