Janja weed
JF-Expert Member
- Nov 20, 2020
- 3,527
- 6,306
ndiomana alipokonywa mke na diblo akakimbilia mahakamani kuvunja ndoa , kimsingi bado ana msongo wa mawazo wazee wanajilia mkewe sasa kihalali.😆😆😆😆
ndiomana alipokonywa mke na diblo akakimbilia mahakamani kuvunja ndoa , kimsingi bado ana msongo wa mawazo wazee wanajilia mkewe sasa kihalali.😆😆😆😆
Swali ni rahisi, na nimeeleza toka awali, bibi aliechuma maembe yake shambani, anatembeza apate elfu 2 ya kula, anafanya biashara haramu?Nikujibu mara ngapi sasa... Biashara Haramu hapo itategemea Mtaji alionao na anaenda kuuza kwa njia gani... mtu anachuma embe 5 anaenda kuuza Tsh 100... anapata faida ya Tsh 500 huyo ni Mjasiriamali mdogo au mfanyabiashara mdogo sana hata kodi atakiwi kuombwa labda alipie ushuru tu, lakini kama ana Hekali 50 za maembe na anauza magunia kwa magunia na kupata faida maradufu ya mfanyabiashara mdogo labda mamilioni ya pesa, huyo anapaswa kulipa kodi na hasipolipa kodi anakuwa anafanya Biashara Haramu au ya magendo na ni ukwepaji Kodi, ambacho ni sawa na kesi ya kuhujumu Uchumi....
Kasome sheria za mlipaji kodi hili ujue ni kundi gani la wafanyabiashara au wafanyakazi wanapaswa kulipa kodi na ni kundi gani la wafanyabiashara wanatakiwa kulipa ushuru tu (Levy au Fees)... na ni kundi gani wao kodi au Ushuru hauwahusu kabisa kulingana na mazingira waliyopo... hili ujue ni yupi kwenye kundi lipi akiyumba kidogo anaitwa ukwepaji kodi
Ndio hilo Swali nililouliza toka awali, bibi aliyechuma maembe shambani kwake, na anatembeza ili apate pesa ya kula siku hiyo, anafanya biashara haramu?Haijasajiliwa ila ilitakiwa isajiliwe, sio Haijasajiliwa sababu ni ndogo. Sheria Za Nchi zinaruhusu biashara zote ambazo hazifiki Milioni 4 kwa mwaka kutosajiliwa, ina maana kama Bibi yako hauzi majembe ya milioni 4 asiposajili hio sio shadow economy, ila kama anauza majembe Ya milioni 40 na has ajili biashara basi yeye ndio anaesemwa hapa.
Hafanyi sababu mtaji/pato lake halifiki milioni 4Ndio hilo Swali nililouliza toka awali, bibi aliyechuma maembe shambani kwake, na anatembeza ili apate pesa ya kula siku hiyo, anafanya biashara haramu?
Kwenye uzi alioweka jamaa nionyeshe alipoweka hicho kigezo cha milioni 4, maana tunajadili bandiko lake.., na amejumuisha wote kuwa ni haramu, bila kusema kwamba kiwango ni kiasi gani.., yeye kawaita wote haramu!Hafanyi sababu mtaji/pato lake halifiki milioni 4
Wewe hauko serious... yani marekani ina 5% ya shadow economy na Tanzania ina 44.7% ya shadow economy... alafu unasema eti kwa sababu zote zinashadow Economy haina shida, huna tofauti na kulinganisha mtu aliyetapeliwa 1,000 Tsh (Buku) alafu na mtu aliyetapeliwa Million 100.. eti kwa sababu wote wametapeliwa unaona ni Haina shida, sisi ni kama huyo mwenye ametapeliwa Milliona 100, uwezi kujilinganisha na Marekani aliyetapeliwa Buku tukama mpaka marekani ipo basi hiyo haina shida tuko sawa tu tofauti ni hizo asilimia kwahiyo haina shida
Kwa maigizo tuliyonayo sishangai.Shughuli za magendo na zisizotozwa kodi sasa zinachangia asilimia 11.8 ya Pato la Taifa Duniani (GDP), ikiwa ni punguzo kutoka asilimia 17.7 mwaka 2000, lakini bado zinawakilisha thamani ya kiuchumi ya matrillion ya Shilingi.
Uchumi wa kivuli (Shadow Economy) unajumuisha aina mbalimbali za miamala isiyo rasmi, kuanzia ajira zisizotambulika rasmi hadi shughuli za uhalifu wa kupanga.
Uchumi wa kivuli au unaweza kuita Uchumi haramu, unaojulikana pia kama uchumi wa chini ya ardhi (Underground Economy, uchumi usio rasmi (Informal Economy), au soko la giza (Black Market), unahusisha shughuli za kiuchumi zinazofanyika nje ya mifumo rasmi na iliyodhibitiwa na serikali. Shughuli hizi mara nyingi huepuka ushuru, huepuka udhibiti, au ufuatiliaji, na mara nyingi ufanyika sambamba au pamoja na njia za uchumi rasmi.
Sifa za Uchumi wa Kivuli (Shadow Economy):
1. Ukwepaji Kodi: Washiriki mara nyingi huepuka kulipa kodi, jambo linalovutia wale wanaotafuta faida kubwa.
2. Kukwepa Udhibiti au kukaguliwa: Shughuli hizi zinaweza kupuuza au kukwepa sheria za kazi, sheria za mazingira, au viwango vingine vya kisheria.
3. Ukosefu wa Nyaraka: Shughuli hizi nyingi hufanywa kwa pesa taslimu au kubadilishana bidhaa ili kuepuka rekodi zinazoweza kufuatiliwa na mamlaka.
4. Sifa nyinginezo: Uchumi huu unajumuisha kila kitu kutoka kwa wauzaji holela wa mtaani, biashara zisizosajiliwa, na biashara ya dawa za kulevya hadi kazi za malipo ya mezani au mikononi kutoka au kwenda kwa wataalamu.
Mifano wa 1: shughuli Halali Lakini Zisizodhibitiwa kama wauzaji wa mtaani wasio na vibali vya biashara au wasiosajiliwa au Kazi za malipo ya mkononi zisizoripotiwa au kufuatiliwa (mfano, shule za majumbani, ukarabati wa nyumba usiofuata mipango ya jiji).
Mfano wa 2. Shughuli Haramu kama biashara ya dawa za kulevya, uuzaji wa bidhaa bandia, utoroshaji madini, umiliki na uuzaji wa silaha za kivita na magendo haramu ya aina yoyote.
Athari:
1. Athari za Kiuchumi: Kupungua kwa mapato ya serikali kutokana na ukwepaji wa kodi. Na pia ushindani usio wa haki kwani biashara zisizo rasmi zinaweza kutoa bei za chini kwa kuepuka gharama kama kodi au kufuata sheria.
2. Athari za Kijamii: Ukosefu wa ulinzi kwa wafanyakazi (mfano, hakuna bima ya afya au msaada wa kisheria endapo mfanyakazi atapata shida za zinazohitaji msaada wa kisheria). Pia uwekezaji mdogo katika miundombinu na huduma za umma kutokana na kupoteza mapato ya kodi.
View attachment 3348936
Tanzania inashika nafasi ya 7 Duniani kwa kuwa na Uchumi Haramu au Uchumi Kivuli, ikiwa na zaidi ya asilimia 44.7% ya uchumi haramu au uchumi kivuli unaopotea kutoka kwenye Pato la Taifa (GDP). Ambapo ni karibia nusu ya Pato la Taifa linapotea kwenye Biashara Haramu au Uchumi Kivuli (Shadow Economy)
Sierra Leone inaongoza, ikiwa na uchumi wa kivuli unaofikia asilimia 64.5 ya GDP. Nchi hiyo ni mfano wa mwenendo mpana zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako ajira isiyo rasmi—ambayo mara nyingi hupatikana katika kilimo, biashara za mtaani, na biashara ndogo ndogo—hutumika kama sekta ya ajira ya kawaida kutokana na upatikanaji mdogo wa kazi za rasmi.
Marekani ina uchumi wa kivuli wa wastani wa asilimia 5% ya GDP. Kutokana na ukubwa wa uchumi wa Marekani, takwimu hiyo inawakilisha wastani wa dola trilioni 1.4, na kuiweka kati ya nchi zenye uchumi wa kivuli mkubwa zaidi duniani kwa viwango vya jumla. @WorldVisualized
Chanzo: Ripoti ya Uchumi wa Kivuli Duniani ya Ernst & Young 2025
Kwenye uzi alioweka jamaa nionyeshe alipoweka hicho kigezo cha milioni 4, maana tunajadili bandiko lake.., na amejumuisha wote kuwa ni haramu, bila kusema kwamba kiwango ni kiasi gani.., yeye kawaita wote
Na hizo ndio zinafanya kuwa na kiwango kikubwa cha Shadow Economy, kwamza Mabosi wengi hawataki wataki wafanya kazi wao kuwa formal kwa sababu ya ukwepaji Kodi na kukwepa sheria za ajira zenye kumlinda mfanyakazi... Boss anatakiwa Amsajilie NSSF au PSSF mwajiriwa wake na kisha kumpatia Bima ya Afya... Mabosi wengi hapa ndipo wanakwepa, ukijumuisha na Kodi nyingine za ukubwa wa kampuni na idadi ya wafanyakazi... shadow economy ndio inaanzia hapa, Mabosi wanataka kuwanyonya RaiaWatanzania wengi wanafanya kazi kwenye informal sector.
Shughuli za magendo na zisizotozwa kodi sasa zinachangia asilimia 11.8 ya Pato la Taifa Duniani (GDP), ikiwa ni punguzo kutoka asilimia 17.7 mwaka 2000, lakini bado zinawakilisha thamani ya kiuchumi ya matrillion ya Shilingi.
Uchumi wa kivuli (Shadow Economy) unajumuisha aina mbalimbali za miamala isiyo rasmi, kuanzia ajira zisizotambulika rasmi hadi shughuli za uhalifu wa kupanga.
Uchumi wa kivuli au unaweza kuita Uchumi haramu, unaojulikana pia kama uchumi wa chini ya ardhi (Underground Economy, uchumi usio rasmi (Informal Economy), au soko la giza (Black Market), unahusisha shughuli za kiuchumi zinazofanyika nje ya mifumo rasmi na iliyodhibitiwa na serikali. Shughuli hizi mara nyingi huepuka ushuru, huepuka udhibiti, au ufuatiliaji, na mara nyingi ufanyika sambamba au pamoja na njia za uchumi rasmi.
Sifa za Uchumi wa Kivuli (Shadow Economy):
1. Ukwepaji Kodi: Washiriki mara nyingi huepuka kulipa kodi, jambo linalovutia wale wanaotafuta faida kubwa.
2. Kukwepa Udhibiti au kukaguliwa: Shughuli hizi zinaweza kupuuza au kukwepa sheria za kazi, sheria za mazingira, au viwango vingine vya kisheria.
3. Ukosefu wa Nyaraka: Shughuli hizi nyingi hufanywa kwa pesa taslimu au kubadilishana bidhaa ili kuepuka rekodi zinazoweza kufuatiliwa na mamlaka.
4. Sifa nyinginezo: Uchumi huu unajumuisha kila kitu kutoka kwa wauzaji holela wa mtaani, biashara zisizosajiliwa, na biashara ya dawa za kulevya hadi kazi za malipo ya mezani au mikononi kutoka au kwenda kwa wataalamu.
Mifano wa 1: shughuli Halali Lakini Zisizodhibitiwa kama wauzaji wa mtaani wasio na vibali vya biashara au wasiosajiliwa au Kazi za malipo ya mkononi zisizoripotiwa au kufuatiliwa (mfano, shule za majumbani, ukarabati wa nyumba usiofuata mipango ya jiji).
Mfano wa 2. Shughuli Haramu kama biashara ya dawa za kulevya, uuzaji wa bidhaa bandia, utoroshaji madini, umiliki na uuzaji wa silaha za kivita na magendo haramu ya aina yoyote.
Athari:
1. Athari za Kiuchumi: Kupungua kwa mapato ya serikali kutokana na ukwepaji wa kodi. Na pia ushindani usio wa haki kwani biashara zisizo rasmi zinaweza kutoa bei za chini kwa kuepuka gharama kama kodi au kufuata sheria.
2. Athari za Kijamii: Ukosefu wa ulinzi kwa wafanyakazi (mfano, hakuna bima ya afya au msaada wa kisheria endapo mfanyakazi atapata shida za zinazohitaji msaada wa kisheria). Pia uwekezaji mdogo katika miundombinu na huduma za umma kutokana na kupoteza mapato ya kodi.
View attachment 3348936
Tanzania inashika nafasi ya 7 Duniani kwa kuwa na Uchumi Haramu au Uchumi Kivuli, ikiwa na zaidi ya asilimia 44.7% ya uchumi haramu au uchumi kivuli unaopotea kutoka kwenye Pato la Taifa (GDP). Ambapo ni karibia nusu ya Pato la Taifa linapotea kwenye Biashara Haramu au Uchumi Kivuli (Shadow Economy)
Sierra Leone inaongoza, ikiwa na uchumi wa kivuli unaofikia asilimia 64.5 ya GDP. Nchi hiyo ni mfano wa mwenendo mpana zaidi katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, ambako ajira isiyo rasmi—ambayo mara nyingi hupatikana katika kilimo, biashara za mtaani, na biashara ndogo ndogo—hutumika kama sekta ya ajira ya kawaida kutokana na upatikanaji mdogo wa kazi za rasmi.
Marekani ina uchumi wa kivuli wa wastani wa asilimia 5% ya GDP. Kutokana na ukubwa wa uchumi wa Marekani, takwimu hiyo inawakilisha wastani wa dola trilioni 1.4, na kuiweka kati ya nchi zenye uchumi wa kivuli mkubwa zaidi duniani kwa viwango vya jumla. @WorldVisualized
Chanzo: Ripoti ya Uchumi wa Kivuli Duniani ya Ernst & Young 2025
Sasa kwani Rwanda wanakwepa Kodi? Au wana biashara zisizosajiliwa, au wana magendo, au madawa ya kulevya kuliko Tanzania.... kila nchi ina Shadow Economy, kipengele ni kwa kiwango gani? Wezi kila nchi wapo, je ni nchi gani yenye wahujumu uchumi wengi?Kama Rwanda haipo huo utafiti ni wa kupuuzwa.
Kabisa yani, tuna maziwa makubwa Afrika, tuna mbuga, tuna madini, tuna kila rasilimali kuliko hata Kenya, ila uchumi yani pato la taifa tunazidiwa na wakenya, huku sisi tukiongoza Kwenye Shadow Economy (Uchumi Haramu), yani wahujumu uchumi na wakwepa kodi ni wengi, ikiwemo biashara za magendoHili kwetu wazi kabisa, tena hapo tulipo nafikiri warudie utafti huenda tukawa top 3.
Fikiria tu sisi kuwa na madini tena mengine yapatikana hapa kwetu tu lakini hali ni tofauti kabisa.
Uenda wanamiliki madawa ila hawakwepi kodi na wanafuata sheria za nchi ambazo mwisho wa siku zinaficha udhaifu wa uchumi na pesa inabaki nchini au kwenye mzunguko wa serikali yani serikali inakuwa na pesa... hizo nchi ulizotaja kama Brazili ni nchi Tajiri kwenye Pato la Nchi na Pato la mtu mmoja, na hazipo kwenye orodha ya nchi masikiniHuu ni ubaguzi yaa ni nchi za AFRIKA tu!!!...mbona hawaitaji ,HAITI,BRAZILI,VENEZUELA?nchi zilizobobea kwa madawa ya kulevya?
Rwanda inayopora huko DRC inatakiwa iwe ya kwanza hapoSasa kwani Rwanda wanakwepa Kodi? Au wana biashara zisizosajiliwa, au wana magendo, au madawa ya kulevya kuliko Tanzania.... kila nchi ina Shadow Economy, kipengele ni kwa kiwango gani? Wezi kila nchi wapo, je ni nchi gani yenye wahujumu uchumi wengi?
Kabisa yani, tuna maziwa makubwa Afrika, tuna mbuga, tuna madini, tuna kila rasilimali kuliko hata Kenya, ila uchumi yani pato la taifa tunazidiwa na wakenya, huku sisi tukiongoza Kwenye Shadow Economy (Uchumi Haramu), yani wahujumu uchumi na wakwepa kodi ni wengi, ikiwemo biashara za magendo
Kabisa yaniWatu wetu wamejaa ubinafsi sana na siyo utaifa, ndiyo maana hata wale wanaopewa nafasi za kusimamia rasilimali zetu ndiyo hao hao hushiriki kufanya uharamia.
Huu ni mwaka wa uchaguzi, wengi wanatafuta nafasi za uongozi kwa ajili ya kutatua matatizo yao binafsi wala siyo kwa ajili ya taifa/wengi.
Waadilifu hukimbia mifumo yetu ya uongozi lakini wezi/mafisadi/wenye uchu na tamaa nk hukimbilia na kuikumbatia kwa ajili ya matumbo yao.
Rwanda inayopora huko DRC inatakiwa iwe ya kwanza hapo
Kutoa Nje na kuleta ndani ni kuongeza pato la nchi au uchumi wa Nchi... Rwanda haiwezi kuongoza kwa sababu haifanyi Magendo kupeleka pesa nje ya nchi, Pesa ya Rwanda inabaki ndani ya nchi kwenye mzunguko wa serikali....Rwanda inayopora huko DRC inatakiwa iwe ya kwanza hapo