Jasmine Razack: Feitoto amekwisha fungua kesi CAS dhidi ya TFF na sio Yanga!

Jasmine Razack: Feitoto amekwisha fungua kesi CAS dhidi ya TFF na sio Yanga!

Tuanzie hapa boss. Hazina mashiko kwa mchezaji au mwajiri?
Watakuumiza kichwa hao hapo washameza dawa zao hawaelewi labda uwavizie jua likizama kidooooogo maana zinaishaga nguvu muda huo,usiku wanapewa dozi nyingine usije ukajaribu...

Huwaambii kitu na yanga yao
images%20(7).jpg
 
Wajibu ni mchezaji kwenda kuzungumza na club yake kuhusu mkataba, wao wanahusika nini?
ila TFF wana mandate ya kuamua mchezaji acheze timu x baada ya kusaini timu mbili [emoji23][emoji23] rejea kesi ya ngasa, yule dogo wa mbao aliyesaini Simba na yanga
 
Wewe mkuu usiwe mgumu kuelewa . Kwenye sakata hili kinacholalamikiwa si mkataba . Kinacholalamikiwa ni kutokufuata hatua za kuvunja mkataba huo.
Dogo alitoweka kambini . Akaja kuibuka akiwaaga mashabiki na wapenzi wa yanga mitandaoni . Ikaripotiwa amevunja mkataba Kwa kuweka kiasi Cha pesa kilichopo kwenye mkataba wake . Club yake ikamshitaki TFF Kwa kuvunja mkataba bila ya upande wa pili kuhusishwa (yanga). Dogo akaitwa kwenye kamati ya TFF . Akashindwa kesi Kwa kutokufuata hatua za kuvunja mkataba na club yake. Akaambiwa wewe Bado ni mchezaji wa yanga Rudi mkamalizane. Dogo akagoma kurudi . Akafungua shauri la kutaka TFF auvunje mkataba wa yeye na club yake. TFF wakamwambia hawana mamlaka ya kuvunja mkataba aludi Kwa MWAJILI WAKE wauvunje . Wakati huo club yake ikamwita njoo tufike mwafaka dogo kakataa . Ulitaka TFF na yanga wafanyaje ?[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Masaa 6 kati ya hersi na Fei, na akapewa options 3, ilikua nn?? Hivi mnajua mnacho kizungumza???
 
Hakuna uthibitisho kuwa hawakuzungumza. Tunajadili kwa maelezo ya Eng Hersi na Fei. Inaonekana ndani ya Club mchezaji hana utaratibu maalum ambao utamuwezesha kutoa uthibitisho kwamba walikuwa na kikao official ili hichi anachosema amekaa na Hersi kwa saa 6 kiwe batili.

Huu ni ushahidi kuwa walizungumza ndio maana Fei akarudi TFF baada ya kuona kuwa wamekaa masaa 6 bila kuelewana.

Aliyekimbilia TFF ni Yanga, Fei alianzia Yanga kisha Yanga ikaenda TFF. TFF wakamwabia Fei arudi Yanga, wakakaa masaa 6 wakashindwana Fei akarudi TFF akarudishwa tena Yanga, akakata rufaa akarudishwa tena Yanga. Akaenda CAS.


Ni suala zito kwa mchezaji, ndio maana hataki mshahara wa mzuri ambao club ipo tayari kumpatia. Kama ni suala jepesi lingeshatatulika.


Kurudi siyo option ya Fei, ni option ya Hersi. According to Fei, Mezani wameshakaa masaa 6 wakashindwana ndio maana akaenda TFF twice.

Na hapa ndipo kichaka kilipo. Inaonekana tafsiri ya neno kukaa mezani inatumika kwa janja janja kama jinsi ilivyotumika janja janja ya kusaini miaka 3. Fei anasema wamekaa, Hersi anasema aje wakae.
Kumtetea Feisal unahitaji kua na roho ngumu sana , TFF walimwambia arudi kwenye club yake kitu cha kwanza angetii then akafatilia madai yake akiwa kituo cha kazi fikilia endapo akishindwa huko CAS itakuaje,?
 
fikilia endapo akishindwa huko CAS itakuaje,?
Atarudi zanzibar na ww na mnaotamani hilo litokee mtafanya sherehe maisha yataendea mpaka mauti itakapogonga hodi.
 
ila TFF wana mandate ya kuamua mchezaji acheze timu x baada ya kusaini timu mbili [emoji23][emoji23] rejea kesi ya ngasa, yule dogo wa mbao aliyesaini Simba na yanga
Mkuu wanaingilia kati kama kwenye mkataba kuna utata kama hio double signing sio kuvunja au kuandika
 
Nilikuwa natafakuri hapa:Hivi kutokuwa na furaha ktk timu flani inaweza ikawa Sababu ya kuvunja mkataba? Kama ndivyo basi nadhani mchezaji hawezi kukosa Sababu ya kuvunja mkataba,rejea kwa Chama na Kisinda.why not Tanzania?
 
Nilikuwa natafakuri hapa:Hivi kutokuwa na furaha ktk timu flani inaweza ikawa Sababu ya kuvunja mkataba? Kama ndivyo basi nadhani mchezaji hawezi kukosa Sababu ya kuvunja mkataba,rejea kwa Chama na Kisinda.why not Tanzania?
Ebu fafanua iyo kutokuwa na furaha ktk timu ni kitu gani!?
 
Mkataba unaisha bila kuutumikia, kumbuka hii ni case nyingine.....!!!

Watu watalala nae ulalo ulalo......nasema atalipia gharama za ujinga wake kwa Uchungu Mkubwa...

Ajiandae kisaikolojia...
Ngoja nikufahamishe kitu, moja ya Sheria za Cas ni kwamba mchezaji halazimishwi kucheza timu asiyo itaka na mchezaji anaweza akavunja mkataba muda wowote iwe kwa halali au isivyo halali, kama akivunja mkataba isivyo halali basi atatakiwa kulipa fidia ya mkataba kulingana walivyo kubaliana katika kipengele cha kuvunja mkataba, na hicho kitu wangeweza kukiamua Tff lakini walishindwa kumchukulia hatua fei Toto kwa sababu zao binafsi wanazo jua wao
 
Ni sahihi kabisa. Nilishawahi kusema TFF hawajatimiza wajibu wao.
Sijui uwa mnawaza kwa kutumia viungo gani vya mwili? Tuwekee kifungu kinachoilazimisha Tff kuvunja mkataba halali baina ya mchezaji na klabu yake,
 
Back
Top Bottom