La WIZA
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 221
- 497
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijui Solomon yu hali gani huko aliko!!
Na inaleta rahaTamu lkn fupi
RIWAYA: MPANGO WA CONGO
SEHEMU YA 19
Remi alipotoka kituo cha polisi alihitaji sana kuonana na Mwasu lakini pia alihitaji kupumzika walau saa kadhaa baada ya kuwa kwenye heka heka kwa siku kadhaa.
Akajipekua kwenye sidiria aliokuwa amevaa na kutoa kikaratasi kilichokuwa na namba za simu za Malima mtu aliesemekana kuwa na mahusiano na Mwasu.
Kwa msaada wa vijana waliokuwa wamesimama karibu yake,walifanikiwa kupata simu ambayo walimpa Remi.
Remi akampigia Malima.
****
Malima alikuwa ndani kwake akiwa ameshika kiuno huku akitikisa kichwa kushoto kwenda kulia na kulia kwenda kushoto.
Alichanganyikiwa!!
Alikuwa ametumia zaidi ya saa tatu akitafuta nyaraka fulani zilikokuwa kwenye mkoba wake wa kazini bila mafanikio.
Alipekuwa kila pahali bila kupata jawabu la wapi alipoziweka.
Mwanzo alidhani aliziacha ofisini lakini kumbukumbu zake zilimwambia hajawahi kuacha hizo nyaraka kila alipokwenda.
Na alikumbuka vyema kabisa ya kuwa hata wakati yupo msibani,nyaraka zile zilikuwa ndani ya gari hadi wakati aliporuhusu gari limpeleke Mwasu mgahawani kwake Igoma.
Kila alipofikiria ni nani hasa anaeza kuwa amezichukua kati ya dereva na Mwasu; hakupata jibu.
Hakuona kama Mwasu anaeza kuwa amezichukua nyaraka zile muhimu wakati ule ama dereva wake ambae amemwamini zaidi ya miaka mitatu.
Zipo wapi? Hakujua.
Alirudi tena kwenye mkoba na kutazama,alikuta nyaraka zingine zipo kama kawaida isipokuwa zile nyaraka tu.
Akaingiwa na wasiwasi.
Akatamani kumpigia mkubwa wake wa kazi ambae ndie aliempa kazi ya kuzimilisha nyaraka zile baada ya zile za mwanzo kuonekana zinahitaji marekebisho kadhaa.
Mbali ya yote ni kuwa mkubwa wake wa kusanifu majengo alikuwa amemwambia kazi ile ina pesa nyingi sana na pia ni sifa kwa kampuni yao kupata kazi ile ya serikali.
Alichanganyikiwa zaidi baada ya kugundua umuhimu wa kazi ile.
Wakati akiwa amekata tamaa ya kuzipata nyaraka zile ni wakati aliposikia simu yake ikiita kwa fujo.
Akasonya huku akienda kuipokea.
Alikutana na namba ngeni!!
Akapokea!!
"Habari!!" Ikasabahi sauti kavu ya kike.
Malima akasita kujibu huku akijaribu kubahatisha sauti itakuwa ya nani bila kupata majibu.
"Nzuri" akajibu Malima kwa sauti ya kukwaruza.
"Naongea na Malima!!" ikahoji sauti upande wa pili.
"Ndio,nawe nani?" akahoji Malima.
"Naitwa Remi!!" ikajibu sauti upande wa pili.
"Nikusaidie nini usiku huu" akauliza Malima.
"Naomba nielekeze au nipe namba za Mwasu tafadhali!!" akasema Remi.
"Mwasu!!" akashangaa Malima.
Ukapita ukimya wa nusu dakika.
"umepata vipi namba yangu!!" akauliza Malima baada ya kutilia mashaka mtu aliempigia.
"Samahani ndugu mi ni mdogo wake Mwasu; kupata namba nitakweleza siku nyingine ndugu!" akaeleza Remi.
Malima akakaa kimya kidogo kisha akauliza.
"Upo wapi!!?"
"Nipo hapa Soko la Mwendesha!!" akajibu Remi huku akimtizama kijana aliempa simu ambae alitikisa kichwa kuafiki ni sahihi alipotaja.
"Subiri kidogo!!" Malima akasema na kukata simu kisha akampigia Mwasu.
"Nambie mpenzi!!" ilisema sauti ya Mwasu baada ya kupokea simu.
"Samahani kwa kukusumbua usiku!!" alijitetea Malima.
"usiwe na shaka upo huru kunipigia muda wowote ule unaojisikia mpenzi." Mwasu alimtoa wasiwasi Malima.
"Ok! Nimepigiwa simu hapa na binti anaitwa Remi...!" hakumaliza alichotaka kusema akasikia mshituko alioupata Mwasu.
"Wewe unasema nani vile!!" aliuliza Mwasu huku akinyanyuka kitandani alipokuwa amejilaza huku kanga ikimdondoka na kubaki uchi.
Hakujali wala!!
"Remi!!" alijibu Malima na kuzisikia pumzi za Mwasu alizopandisha na kuzishusha kwa mkupuo.
"Kasema yuko wapi saivi!!" aliuliza Mwasu.
"Soko la Mwendesha" alijibu.
"Naomba umwambie anisubiri hapo hapo asitoke lakini pia mwambie namna ya kunipata!" alisema Mwasu huku akikita simu.
Malima akabaki akiitazama simu yake bila kufanya lolote.
Yalimchanganya mambo.
Akabinua mabega yake kuashiria hayamhusu.
Akampigia tena Remi.
Simu ikapokelewa.
"Kanambia umsubiri hapo hapo atakuja kukufuata ila akikawia shuka chini kutoka hapo ulipo ulizia kanisa la wokovu, na ukifika hapo ulizia kwa Bibi Tuku. Sawa!!" akaelekeza Malima.
"sawa" akajibu Remi na Malima akakata Simu.
Malima akakaa kwenye sofa huku akirudi kuwaza zilipo nyaraka za ofisi.
Hakupata usingizi.
*****
Ilikuwa saa, ikatimia hadi lisaa la pili bila kumuona Mwasu ama dalili ya kutokea Mwasu na kutoka pale alipokuwa tayari watu walianza kupungua baada ya usiku kuanza kuwa mkubwa.
Remi alitamani kuondoka pale alipokuwa ili aelekee huko kanisani kumtafuta Mwasu ila akajionya huenda kufanya hivyo kungempelekea Mwasu kumkosa.
Akavuta zaidi subira.
Kwake subira haikuwa heri,muda ulienda bila Mwasu kutokea.
Remi alikuwa amekaa kwenye kibalaza cha duka la kuuza filamu na mbele yake pia kulikuwa na duka lingine la kuuza filamu kifupi eneo lile lilizungukwa na maduka mengi ya kurudufu filamu na muziki.
Duka la tatu kutoka alipokuwa Remi kulikuwa na vijana wawili waliokuwa wamesimama kama hawafahamiani huku mara kwa mara wakimtizima kwa kuibia.
Remi hakutaka kuwatilia mashaka na aina ya utazamaji wao ila wasiwasi wake ulizidi pale ambapo mwenye duka alifunga na wale vijana wakabaki wakiwa wamesimama bila kuonesha jitihada zozote za kuondoka.
Remi aliishi kwa mashaka siku zote hivyo hakutaka kuendelea kukaa pale wakati roho yake haitaki.
Akanyanyuka huku akiwatizama vijana wale ambao nao walinyanyuka na kuanza kumfuata.
Remi aliongeza hatua za miguu yake,vijana nao wakaongeza hatua.
Remi akaingia katikati ya soko pweke lililogubikwa na kiza kizito.
Alipokelewa na kelele za mapaka shume yaliokuwa yanagombania mabaki ya chakula sokoni pale.
Akapiga hatua akiwa na lengo la kupotelea gizani ili kuwapoteza vijana wao ambao alijua dhamira yao.
Hakufika mbali akasikia sauti ikiamuru nyuma yake.
"Simama hivyohivyo!" ilikuwa sauti ya watu iliojaa mamlaka.
Remi akasimama na akageuka na akashuhudia vijana wale wakija mkukumkuku wakiwa wamewasha taa za simu zao.
Lakini hakumuona alieamrisha asimame.
Remi matatani tena!!