Je, Afrika yenye utajiri mwingi inakuwaje bara maskini zaidi duniani?

Maadui,
Hawa wa Africa ambao ni UJINGA, UMASKINI NA MARADHI.......................

Ndio maadui wakubwa wa Africa
NI uongozi mbovu wala hakuna nini, una akili Kweli unamnunulia V8 DED/DC/DAS anaweza kumsaidia hata Mwalimu kuhama? kwanini usimpe pickup double cabin ambayo itasaidia mambo ya msingi badala ya kubeba mtu mmoja pekee?
 
Is this the afrocentric or eurocentric view toward poverty?

Umaskini ni mtazamo wa jamii fulan

Your basic needs isn't necessary to be someones basic needs. Note that!!
Mkuu unajua basic maana ya neno basic ? Achana na mengine hakuna Binadamu anaweza kuishi bila chakula; Na hakuna binadamu anadamu anaweza kuishi bila kujikinga na extremes za weather be it amevaa magome ya miti au ngozi na anahitaji shelter ya kujikinga kujiziua na hatari zozote zile (iwe ghorofa, pango au nyumba ya nyasi)

kwahio ukiangalia hata mmasai huenda akawa tajiri kwa muktadha huo kuliko hata mtu anayelipwa dollar 500 kwa wiki na anakaa kwenye one rented bedroom flat kule California au London.....; Lakini Basic needs remain basic.... (Hizo needs tatu ni fundamental)
 
Vipi pamoja na utajiri huo wewe binafsi umefanikiwa kuutumia kuufanya ukoo wenu kuwa tajiri?!
Fikra kama hizi ndio fikra za Ubinafsi ambazo ndio zinazolifanya bara la Africa kuwa nyuma kimaendeleo kuliko mabara yote Duniani pengine mpaka na Akhera !!

Ukienda katika Nchi zote zilizoendelea huko Duniani utakuta wananchi wake sio kwamba ni matajiri bali wanaenjoy kwa kupata huduma zote yaani zote muhimu zinapatikana kwa wakati wote na kwa maisha yao yote !!

Afrika kila mtu mmoja mmoja anataka awe tajiri yeye na walio karibu yake tu !!

Wengine potelea mbali !!
 
Utajiri upo kichwani.

Tatizo lenu Waafrika hamuangalii utajiri wa kichwani, mnaangalia mafuta, dhahabu, ardhi na maliasili nyingine kama hizo, ambazo hamjui kuzitumia vizuri.

Huyo John Magufuli mwenyewe alikuwa bogus tu.

Na ndiye mnamuona mtu smart.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…