Je, Aga Khan Sea View, ni kwa wahindi, wabunge, mawaziri na viongozi wa juu wa Serikali tu?

Je, Aga Khan Sea View, ni kwa wahindi, wabunge, mawaziri na viongozi wa juu wa Serikali tu?

Nitake nisitake,utake usitake,kiumbe hai chochote lazima kife.Anyway kwa swali lako huoni kabisa umuhimu wa vituo vya kutolea huduma za afya,yaani ungekua kiongozi ungeona ni muhimu huduma nyingine ziwepo,ila huduma za afya ungeachana nazo,nikimaanisha usingehangaika nazo kwa kuwasogea wananchi wako?
Tulia mkuu
 
Na wana mfumo wa paperless ukienda hospital mpk unarudi hakuna kartac yyte unayoona form ya doctor dawa wala vipimo yani unapewa tu file number ww unazunguka na kikartac kwahio wizi wa bima za afya umeongezeka
Wanashirikiana kuiba na watawala
 
Tulia mkuu
Nimeshangaa sana mkuu,nimeeleza alikutwa ini na figo vimeharibika,we unadhani angekua anafanya check up,yasingegundulika mapema na yawezekana hadi sasa angekuwepo?
Aisee wewe yawezekana ukikuta mgonjwa anafanyiwa CPR unaweza ukafanya jitihada za kuzuia watoa huduma,wasiendelee kutoa huduma husika,kisa LAZIMA TUFE.
 
Nimeshangaa sana mkuu,nimeeleza alikutwa ini na figo vimeharibika,we unadhani angekua anafanya check up,yasingegundulika mapema na yawezekana hadi sasa angekuwepo?
Aisee wewe yawezekana ukikuta mgonjwa anafanyiwa CPR unaweza ukafanya jitihada za kuzuia watoa huduma,wasiendelee kutoa huduma husika,kisa LAZIMA TUFE.
Mkuu vipimo ni gharama kubwa sn, siyo kwamba alikuwa hataki kufanya checkup isipokuwa ni urasimu wa wizara ya afya ndiyo tatizo
 
WAHINDI SI WATANZANIA WENZETU, HO NI MABEBERU TU, HAO VIJIBWA NA MAJUHA WA KITANZANIA(VIONGOZI) NDIYO WANAO LEA UPUUZI HUU
Muhindi na muarabu anakuwa mtanzania tu anapokuwa fukara ila akipata pesa huyo anageuka kuwa beberu na fisadi wa nchi yetu, na uraia wake unakuwa mguu mmoja ndani na mwingine nje

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
Mhindi( gabacholi) mmoja alikuwa ananieleza;
Wale Aga Khan Hospital vipi? Nilifanyiwa operation pale ilinigharimu 15,000,000ts(milioni kumi na tano):nikaenda India kufanyiwa operation hiyo hiyo,ilinigharimu 1.5 million Tanzanian shillings.(shilingi milioni moja na nusu)."
Hatutaki kuwakashifu Aga Khan Hospital,lakini wanasemwa vibaya na Mhindi mwenzao.( Na huyu Mhindi ninayemzungumzia ameshafariki)
 
Charges zao pale sea view ni kubwa na NHIF hawako tayari kulipia na kuepusha migogoro hawapokei NHIF sio hao tu hata Saifee pale karibu na namanga nao hawataki NHIF na ishu ni swala la malipo hao jamaa ni wagumu kulipa
 
Hivi vijijiji wanaishi vipi? mbona wana afya njema na hakuna hizo Aga khan?
Dawa za kizungu ni package ya dawa za vijijini. Mmea wa Artemisia (omushunshu) tumeutumia mara nyingi kijijini kutibu majeraha na majipu.

Pia gugu aina ya bidens pilosa au mashona nguo tunayatumia kijijini kwa ajili ya kutibu majeraha. Wengine huchemsha kwa ajili ya kuongeza damu.

Hivi unajua kwamba uking'atwa na nyoka unaweza kujitibu porini kwa kusaga mkaa na kufungia kwenye jeraha au ukanywa mkorogo wa mkaa kutibu sumu uliyokunywa au kunyweshea?

Mkumbushe Dr.Mollel ule mzuka wa kutengeneza dawa zetu wenyewe kipindi cha JPM uliishia wapi?
 
Mtoa mada ambacho haujui ni kuwa Aga Khan ni jina moja lakin bei zinatofautiana bei ya pale mjin ni kubwa sana kuliko za uswazi hivyo Bima yako haina huo uwezo usikariri jina la Aga Khan ukajua ukienda yoyote bei ni sawa. Pia mbona madokta wengi na na manesi ni waafrika kama wewe tu ondoa hofu ya ubaguzi tutafute PESA
 
P
Katikati ya mwaka huu yaani 2023 mwezi wa sita nilikwenda hospitali ya Aga Khan iliyopo Sea View Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu, kama taratibu zilivyo niliwasilisha kadi yangu ya bima ya afya ilipokelewa na nikapewa jibu kuwa siwezi kutibiwa kwenye hospitali hiyo!

Haikuwa shida kwangu, nikaenda hospitali ya Shree Hindu Mandal iliyopo Upanga na nikapata tiba kwa kutumia kadi hiyohiyo.

Mwezi huu wa kumi nilienda kwenye tawi la hospitali ya Aga Khan lililopo uswahilini na nikisema uswahilini ni uswahilini kweli kwani madakitari, manesi na wafanyakazi wengine ni waswahili wenyewe wanakili wahindi wa uzao wa Aga Khan hawakanyagi huku uswazi!

Baada ya kupata tiba kwenye hilo tawi letu la hospitali ya Aga Khan nikamuuliza dakitari kuhusu hospitali mama ya Sea View, naye hakusita kuniambia kuwa kule ni kwa wahindi, wabunge, mawaziri na viongozi wa juu wa serikali, nikajua kuwa ukiwapendelea hawa basi jambo lako litakwenda vizuri bila kuhojiwa.

Miaka iliyopita tulikuwa tukitibiwa bila tatizo kwenye hospitali hiyo ya Aga Khan Sea View licha ya tatizo la hawa wazalendo watanzania wenzetu kutokujua kiswahili vizuri, lakini walipoona tunawabana wakatufungulia matawi uswazi na madakitari wetu wakiswazi tumaliziane huku huku.
Pesa yako ndiyo inaamua utibiwe wapi uishi wapi, mwanao asome shule gani, utembee na mwanamke gani. Hospitali ya Agha Khan haimbagui mtu kutibiwa pale. Hiyo bima yako haina sifa ya kukubalika pale lakini ziko bima zingine zinakubalika kwa sababu ya package ya hizo bima. Bima uliyonayo gharama inazolipa ni za chini kuliko viwango vinavyochajiwa na hiyo hospitali.

Acha kuingiza siasa kila mahali.
 
Bima yako ndogo masta ungeenda na cash ungefurahia huduma pembeni ya bahari pia bill yako ingekufanya uombe wakurudishie ugonjwa wako
 
Iyo hospital ni hatari mimi niliumwa malaria ghafla nilipotoka safarini nikalazwa pale before ujatibiwa nikaambiwa ni deposit mamilioni 6 ndio matibabu ya anze bahati nzuri bima yangu ika cover cost zote mpaka natoka pale nilikaa kama siku6 cost ikaja miloni 5 na laki 8..ile hospital ni special kwa watu wenye vipato vikubwa kama unajua kipato chako ni cha kubangaiza usithubutu kukanyaga pale.
 
Mkuu Hismastersvoice , Aga Khan main hapo, hawatubagui kabisa sisi akina REGULAR JOE/JUMA. Ila wana operate kutokana na makubaliano yao na NHIF.

NHIF bima zao zina category nyingi. Wana bima za mashirika kama BOT, TPA, TANESCO n.k halafu kuna bima zile za walimu, wahudumu wa afya nk (standard). Hizi ndizo zinaamua huduma zipi upate na zipi usipate.

So Aga Khan wamekubaliana na serikali yetu, watanzania watakaotibiwa hapo ni wenye bima za mashirika tuu. Hizi standard ( za walimu, ma-dr sumbawanga, manesi mwananyamala, n.k zitapokelewa Aga Khan za mitaani huku.

Kingine tunachotakiwa kujua ndugu wananchi, hata hizi hospital na polyclinic za pembeni, dawa tunazopata wakati mwingine zinatofautiana kutokana na aina ya bima yako.

Mfano mimi ni mwalimu, nimeenda polyclinic X na mfanyakazi wa TPA ameenda hapo hapo X. Wote tuna kikohozi, na wote tumeandikiwa cough sysrup. Tukienda kuchukua dawa, mimi nitapewa Zecuf yangu ya 3,000. Lakini mwenzangu atapewa Benyln ambayo inauzwa mpaka 20,000
 
Back
Top Bottom