Mkuu
Hismastersvoice , Aga Khan main hapo, hawatubagui kabisa sisi akina REGULAR JOE/JUMA. Ila wana operate kutokana na makubaliano yao na NHIF.
NHIF bima zao zina category nyingi. Wana bima za mashirika kama BOT, TPA, TANESCO n.k halafu kuna bima zile za walimu, wahudumu wa afya nk (standard). Hizi ndizo zinaamua huduma zipi upate na zipi usipate.
So Aga Khan wamekubaliana na serikali yetu, watanzania watakaotibiwa hapo ni wenye bima za mashirika tuu. Hizi standard ( za walimu, ma-dr sumbawanga, manesi mwananyamala, n.k zitapokelewa Aga Khan za mitaani huku.
Kingine tunachotakiwa kujua ndugu wananchi, hata hizi hospital na polyclinic za pembeni, dawa tunazopata wakati mwingine zinatofautiana kutokana na aina ya bima yako.
Mfano mimi ni mwalimu, nimeenda polyclinic X na mfanyakazi wa TPA ameenda hapo hapo X. Wote tuna kikohozi, na wote tumeandikiwa cough sysrup. Tukienda kuchukua dawa, mimi nitapewa Zecuf yangu ya 3,000. Lakini mwenzangu atapewa Benyln ambayo inauzwa mpaka 20,000