Jana tarehe 08/03/2020 wanawake wote duniani waliadhimisha kumbukizi kwa ajili Yao ikiwa na lengo la kupaza sauti kupatiwa USAWA na kupinga ukandamizaji wa kijinsia!!
Katika maadhimisho hayo wanawake kwa vikundi ama kwa jumuiya zao walijumuika pamoja kujiwekea mikakati mbalimbali kijamii na kisiasa.
Lakini kituko zaidi kilitokea wakati Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Christian Makonda alipoamua kwenda ili kuwasapoti wanawake wa Chama Cha demokrasia na maendeleo ( Chadema) .
Kilichotokea kulingana na clip zinazogaa katika mitandao ya kijamii Ni kuzuiliwa kuingia huku ikisemekana Mwenyekiti wa Bawacha Taifa Halima James Mdee kuamuru Jambo Hilo.
Well, kwa jicho la kawaida inaonekana Ni sawa kwa kitendo hicho cha kufedhesha alichofanyiwa RC Makonda, Lakini Ni Cha kijinga kufanywa na Baraza Hilo la wanawake Tena ambao wengi wao wanajua protocol za kiuongozi ya kwamba RC anaweza kuhudhuria hafla yeyote ya kitaifa inayofanyika mkoani kwake isipokuwa shughuli binafsi.
Baraza la wanawake Chadema linaongozwa kwa sheria za Nchi na Lina usajili, sio Ngo's Ni taasisi halali inayotambulika na Serikali ikiwa chini ya udhamini wa CHADEMA.
Rai yangu kwao Kuna wakati wa kushirikiana na Serikali ili kufikisha maoni Yao kwa urahisi bila kushupaza shingo, Uzuri waalikwa wao walikuwa Ni moja ya watu waelewa na wanaharakati Kama Fatuma Karume wangeweza kufikisha kero za wanawake kwa RC na yeye akafikisha mahali husika.
Halima Mdee namuona Kama kiongozi mshamba Sana na hii Ni Mara ya pili kufanya vitu vya ajabu Ana chuki, fitina..
Kwa kufanya vile moja kwa moja alimjengea picha RC Makonda kwamba ni moja ya watu wanaokandamiza haki za wanawake.
Kitendo cha hovyo kufanywa na watu waungwana ilitakiwa wamruhusu ili kumsikiliza Halima Mdee asijifanye Bibi Titi Mohamed Hana Kariba hiyo na Wala hatokaa amfikie...
Katika post yangu ya juzi nilivyomuaga Halima James Mdee katika nafasi ya ubunge watu walinishambulia na hoja zao mfu haya semeni na hili ni Sahihi?
1. Kwanza siyo kweli kuwa Bashite a.k.a Makonda ni kiongozi wa kitaifa....
Yeye ni kiongozi mkuu wa mkoa wa DSM na kwa sbb hiyo hana hiyo haki ya kisheria eti kuhudhuria tukio lolote la kitaifa hata bila kukaribishwa/kualikwa....!!
Mamlaka yake yanaishia mipaka ya mkoa wa DSM inapoishia. Nje ya hapo is a no body. Ndiyo maana alienda Dodoma kwenda kufanya uhalifu wa jaribio la kumuua Tundu Lissu mwaka 2017 bila mafanikio....
Sina hakika iwapo hata Rais wa JMT kama ana mamlaka hayo....
Nakumbuka sherehe za wafanyakazi (Mei mosi) mwaka 2010 kama sijakosea, TUCTA waligoma kumwalika Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuwa mgeni rasmi wa sherehe hizo kama ulivyo utamaduni wa miaka yote....
Lakini hakuna kumbukumbu kuonesha kuwa Rais Kikwete aliamua kujipeleka tu kwenye sherehe hiyo kwa kulazimisha hata pasipo kualikwa eti tu kwa sbb yeye ni Rais wa nchi....
2. Turudi kwa Bashite a.k.a Makonda, RC - DSM vs BAWACHA. Hebu tueleze iwapo huyu bwana alikuwa na mwaliko au la. Kama alikuwa nao na waandaaji wa sherehe hizo kumtendea vile, basi ni wazi hawajafanya kitu chema....
Lakini kama RC Bashite a.k.a Makonda hakuwa na mwaliko na akaamua kujipeleka mwenyewe tu kwa ubabe, basi asiwalaumu BAWACHA na badala yake ajilaumu mwenyewe kwa kutofuata utaratibu wa mambo....
3. Ni vyema viongozi hususani waliopewa dhamana ya kiserikali wakatambua kuwa, uongozi ni utumishi tu wa muda fulani na baada ya muda huo kupita, wengine wanaweza kuchukua nafasi yako na wewe kuwa kama walivyo...
Wajiheshimu na RAIA nao watamheshimu tu. Wajifunze kufuata taratibu na sheria za kuwashimu wengine na kazi zao. Makonda hili naona linampiga chenga sana...m