Je, Alichofanyiwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na BAWACHA ni sahihi?

Unauliza kabla hujapewa majibu,ujijibu mwenyewe.Shule ulienda kusomea ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taasisi bora kabisa barani aftika. Hebu tuambie kwa ufupi tu shughuli ilizofanya zenye manufaa kwa wanawake kiasi cha kuwa taasisi bora afrika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kumkomboa mwanamke wa Tanzania kifikra si kazi ndogo , hili ni jambo kubwa kuliko maelezo , kabla ya BAWACHA kuletwa wanawake wa Tanzania walionekana kama watumwa tu
 
kabla ya yote, si ndo huyu makonda kawasaidia wanawake ambao walikua wana matatizo ya kuwa na wanaume wasiowajibika na malezi ya watoto, ilikuaje tena anazuiliwa pamoja na juhudi kubwa alizofanya juu yao
 
KKwa hiyo hata ubalozi wa Marekani anaweza kuingia wakati wowote? Baadhi ya wanawake mna matatizo
 
Ulichokileta ww ni cha kijinga zaidi....jitu limevaa kihuni bila mwaliko unavamia mkutano wa akina mama.....hili nalo lihitaji elimu kujua kwamba jamaa alichemka?
 

1. Kwanza siyo kweli kuwa Bashite a.k.a Makonda ni kiongozi wa kitaifa....

Yeye ni kiongozi mkuu wa mkoa wa DSM na kwa sbb hiyo hana hiyo haki ya kisheria eti kuhudhuria tukio lolote la kitaifa hata bila kukaribishwa/kualikwa....!!

Mamlaka yake yanaishia mipaka ya mkoa wa DSM inapoishia. Nje ya hapo is a no body. Ndiyo maana alienda Dodoma kwenda kufanya uhalifu wa jaribio la kumuua Tundu Lissu mwaka 2017 bila mafanikio....

Sina hakika iwapo hata Rais wa JMT kama ana mamlaka hayo....

Nakumbuka sherehe za wafanyakazi (Mei mosi) mwaka 2010 kama sijakosea, TUCTA waligoma kumwalika Rais Jakaya Kikwete wakati huo kuwa mgeni rasmi wa sherehe hizo kama ulivyo utamaduni wa miaka yote....

Lakini hakuna kumbukumbu kuonesha kuwa Rais Kikwete aliamua kujipeleka tu kwenye sherehe hiyo kwa kulazimisha hata pasipo kualikwa eti tu kwa sbb yeye ni Rais wa nchi....

2. Turudi kwa Bashite a.k.a Makonda, RC - DSM vs BAWACHA. Hebu tueleze iwapo huyu bwana alikuwa na mwaliko au la. Kama alikuwa nao na waandaaji wa sherehe hizo kumtendea vile, basi ni wazi hawajafanya kitu chema....

Lakini kama RC Bashite a.k.a Makonda hakuwa na mwaliko na akaamua kujipeleka mwenyewe tu kwa ubabe, basi asiwalaumu BAWACHA na badala yake ajilaumu mwenyewe kwa kutofuata utaratibu wa mambo....

3. Ni vyema viongozi hususani waliopewa dhamana ya kiserikali wakatambua kuwa, uongozi ni utumishi tu wa muda fulani na baada ya muda huo kupita, wengine wanaweza kuchukua nafasi yako na wewe kuwa kama walivyo...

Wajiheshimu na RAIA nao watamheshimu tu. Wajifunze kufuata taratibu na sheria za kuwashimu wengine na kazi zao. Makonda hili naona linampiga chenga sana...m
 
hawezi kwenda mahali bili kufuata itifaki. pia mi naona hakwenda kama RC. alikuwa kama makonda. itifaki ikazingatiwa
 
March 8, 2020
Mkuu wa Mkoa katika maadhimisho ya siku ya mwanamke Millennium Tower jijini Dar es Salaam , Tanzania
 
Huyo bwana kuna siku ataangukia mikononi mwa akina "Mwamwindi".

Wewe kuwa Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama wa Mkoa haiwezi kuwa tiketi ya kuingia kwenye shughuli yoyote utavyojisikia hata kama hakuna uvunjifu wa amani na watu wapo pale kwa kibali pengine!

It wasn't necessary kwenda pale kuleta tension isiyo na maana yoyote.

RC Dr Kleruu ni mhanga wa tabia hii ya ku-sneak his nose kwenye mambo yasiyomhusu kwa mwamvuli wa cheo!
 
Ni sahihi kabisa yaani unashauri wangempa kero zao shetani mdogo akaziwasilishe kwa shetani mkuu? Nani asiyemjua makonda na baba yake kuwafanyia hila CHADEMA? Umekula maharagwe ya wapi weye.
 
Huyu mtu wako ana zuio la kimataifa la kukutana na watu wastaarabu, au umejisahaulisha!? Mikono yake ni michafu hawezi kucheza na sisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni sahihi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkitukanwa mnalalamika na kusema jibu kwa hoja, Sasa hapo hoja yako Nini?
Afu wanao watajivunia wewe kuwa baba bora!? Rc's na DC's wote NI makada wa CCM na uwt ni ya CCM.
Kwani hakakwenda huko kunako muhusu?
Hakualikwa,alienda fanya Nini Kama siyo ushamba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…