Nikiwa kama muislam ambae nachukizwa na izo itikadi za kigaidi kuuwa watoto na watu wote kiujumla niseme kwamba ayo mambo ni nje na mafundisho na Dini ya uislam na unaweza fuatilia ni namna gani mtume aliishi na Jews pamoja na christian kwa uzuri na kwa wema na watu weusi kutoka Africa na namna gani aliwatoa watu kwenye utumwa na kuzifuta taratibu fikra za kitumwa ambazo zilikua ni asili ya watu wa mashariki ya kati, na mabara ya ulaya
Nikwambie kwamba binadamu anapenda kwenda against na mambo anaelekezwa afanye iyo ni nature
Kwaiyo mambo mengi yanayoleta madhara yanayofanyika na baadhi ya vikundi vya waislam ukifuatilia utagundua mtume aliyakataza
Mfano tukifungua huo mlango wa vita za jihadi zilikua ni vita za kujitetea zina maelezo mapana ila kuna mambo yalikatazwa na mtume yasifanyike katika vita:-
-kuuwa watoto wazee na wanawake
- kujiua mwenyewe (muhanga) wazee wa kamikaze
- kuadhibu kwa moto
- kuuwa maadui waliosalimu amri na mengine mengi
Kwaiyo ukiona jitu limejilipua ujue haliko sawa, ukiona jitu limeua binadam mwenzake ujue halipo sawa na mfano wa hayo
Marekebisho, ni shirki kumuabudu muarabu au binadam au malaika katika uislam na ni dhambi kubwa
Na mtume aliwasihi watu wake ya kwamba mbora wenu katika hii dunia ni yule mwenye kufanya ibada kwa wingi na kufanya mambo mema sio muarabu wala mzungu wala muafrica, kwaiyo hakuna anaemuabudu muarabu
Naamini una mambo mengi yakujifunza kabla yakuendelea kuukosoa uislam ili usiingie kwenye kundi la wajinga, dalili moja wapo ya mtu mjinga katika mabishano au huwa anatabia yakushikilia point moja na hawezi kuiachia mpaka pale atakapojiona ameshinda jichunguze apo ni sababu ya watu wengi wanakupuuza