Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 51,453
- 41,274
Ama kwa hakika, mkataa pema pabaya pana muita.
Mzee huyo baada ya kujilimbikizia fedha na mali za kutosha akiwa kuhani wa kanisa, akaisaliti nadhiri yake ya sakaramenti ya upadre na kuachana na kazi ya uinjilishaji na kutimikia kwenye sakaramenti ya ya ndoa, kwa tamaa za mwili.
Akiwa huko,
akajiingiza kwenye masuala ya uongozi wa kisiasa. Baada ya kujilimbikizia fedha na mali nyingi sana, akapata kiburi na akajiona hana hadhi tena ya kuendelea kua na aina ya familia aliyokua nayo, akatumia ukwasi alionao kufanya unyang'anyi na kupora mke wa wenyewe kibabe, na kuisaliti familia yake ya awali hadharani na kwa udhalilishaji wa kiwango kibaya na cha fedheha sana.
Mzee hakuishia hapo,
akiwa huko huko kwenye siasa na mke mpya alietokana na nguvu ya ukwasi aliokua nao, kwa kunyimwa nafasi ya kugombea nafasi ya urais na chama chake, Mzee huyo aliamua kususa na kudai kuachana na siasa za Tanzania, kumbe ilikua ni unafiki mtupu, na kumbe ule ulikua ndio mwanzo wa mwisho wa anguko lake kisiasa.
Ghafla,
Mzee akatunukiwa nafasi ya uongozi na hayati rais JPM, akawa balozi, na kwa vile alikua mtu mwenye tamaa na uchu wa madaraka, Mzee akatokomea Sweden kwa haraka sana na mke wa wizi, ambae ni wazi anampasua kichwa vilivyo hivi sasa.
Na,
Katika hali isiyo ya kawaida,
Mzee alipopigwa chini kwenye nafasi ya ubalozi, akiwa bado na vihela kidogo, akaanzisha movement iliyoitwa sauti ya wananchi, lakini kutokana na hali mbaya ya kifamilia anayopitia kutoka kwa mke aliepora kwa mwanaume mwenzake, movement hiyo haikudumu sana, na mara ghafla tena Mzee, ikasemekana amerudi chadema, mahali ambapo pamemtokomeza zaidi kisiasa kwa sasa.
In fact,
tangu mwanzo wa andiko hadi mwisho, unaona tabia na hulka ambazo sio za kiungwana, zinavyomtesa na kumsulubisha sana Mzee huyu, asieaminika, kuheshimika wala kutabirika tena kwenye siasa za Tanzania kwa sasa.
Tamaa za fedha, tamaa za kingono, usaliti, majivuno, uporaji, uchu wa vyeo na madaraka ni laana na sababu za mikosi mingi na mabalaa mengi ambayo watu wengi huteseka nayo bila wao kujua.
Sidhani kama kuna miongoni mwa wadau wa JF ambae ana la kujifunza kutoka kwa Mzee huyu useless, ispokua kuepuka aina ya maisha ya anasa na tamaa za mzee huyo.
Lakini pia,
licha ya ya mapungufu hayo ya huyo mzee,
je ni wakati muafaka sasa kwa kanisa na vyama vya siasa alivyowahi kuvitumikia, kumsamehe na kumsitiri kwa fedheha za kijamii, kisiasa na kiuchumi anazopitia kwa sasa?🐒
Mungu Ibariki Tanzania