Je, Avatar yako hapa JamiiForums ina maana gani?

Je, Avatar yako hapa JamiiForums ina maana gani?

Ah! hata picha mwauza sasa???? duh! haya jaribuni kingine kwani mlima unajulikana upo kenya! kwani siri???

acha masihara wewe, mlima upo TZ bana, anyway tuishie hapa maana amani isije kutoweka bure, kenya nyie hamjatulia kabisa.
 
Mpwa ID 2 za nini mimi? pia style yangu ya kuandika ungekuwa umeijua.

aaah, yuu neva noo, kuja jamaa ana ID 6 humu!.
yaaa ila nadhani watu wangekustukia tuu, si unajua mjasiri haachi asili?
 
attachment.php


Superman Avatar - ina maana I can (fly) be there when u need me to help and support you with problems.

This happens only in real life, not at JF.
 

Attachments

  • Superman.jpg
    Superman.jpg
    30.9 KB · Views: 96
umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu!
 
Wananchi kama mnavyoona avatar yangu ni kito aina ya RUBY.....hiyo kitu imejaa sana kwetu Nawenge,Mahenge kule kwetu Upogoroni.Licha ya kwamba najivunia utajiri mkubwa ambao nchi hii inayo lakini nasikitia umasikini ambao unaendelea kuikumba hii nchi hasa Upogoroni kwetu.

Hatari zaidi ni polisi walipoamua kuua ndugu zangu wakina Jongo....nji hii bwana!
 
Sina,lakini baada ya kuona maana ya avatar nyingi tu,tena maana za kufurahisha,kujenga na kufundisha.nitakuwa nayo sana tu...
 
Avata yangu...Nadhani inajieleza tosha kuwa sipendezwi na terrorists wanaoua binadamu wasio na hatia kwa visingizio mbalimbali visivyokua na kichwa wala mkia.
Wananiudhi sana hawa viumbe wenye tabia hizi za kinyama.
 
Huyu Ni "Mchungaji Mwema" anapeleka kondoo kwenye malisho.
Mchungaji huyu ametangulia kondoo akiwaonyesha njia ya kuendea malisho.

Vivyo hivyo kiongozi anatakiwa awe kama huyu mchungaji mwema awaonyeshe njia njema wananchi wake ili siku ya siku nchi yetu iwe ni ya asali na maziwa. Wananchi wawe wananeemeka na kuendelea kuijenga nchi yao na siku moja iwe kama Nchi ya Uholanzi.

Jamani, mchungaji mbele kondoo nyuma?? atakigeuka atakuta wote wamepotea.
 
Red, black, green and gold is my identity, I'm proud African and this is my flag, a blackman flag.
Avatar yangu ni bendera isio rasmi ya waafrika na wanugu kule Marekani ikiambatanishwa na alama ya Peace "amani" ya rangi ya manjano, hizi ndio rangi zinazoelezea uafrika, kwa takriban bendera zote za waafrika zina rangi hizi. Yellow peace means gold (minerals)
We want peace and control of our own minerals, they robbed us, enslaved us and devided us for the sake of golds and diamonds, Africans want peace and stability and not handouts, Africa is rich , fertile and Africans demands the right to decide their own destiny. Let's Africans have the control of our matters and destiny if we really want peace and prosperity to the world.
 
Mm avater nayotumia ni ya bilionea kutoa SA, anatwa Nicky oppenhermer ni former chairman wa kampuni ya alimasi huko SA inaitwa De Beers Ltd, ana utajiri wa Usd $7.7b
mm nilichangua hii picha 'avater' kuwakilisha profile yangu kwa sababu nilipata kusoma kuhusu mafanikio yake anaamini kwenye kujitua na kujitoa ili kufanikiwa haijalisi upo kwenye hali gani.. Kila mara nikiangalii picha inanifanya nikumbuke maneno yoke na pia nifanye juhudi kutimaza malengo yangu.
Kwa mnaotumia Avater kama mm hiyo avater yako ni ya nani?? Au ndo wewe.?? Pia kwa nini umechangua hiyo avater tupe japo ka story behind
 
Huyo kwa avatar yangu ni Shaaban Robert, Baba wa kiswahili. Napenda kiswahili lugha poa sana ndio lugha yangu ya kwanza kuijua(fikra halisi huja kwa lugha asili), sipendi zile " xawa, tantee, jomoni, vepe, na zingine kama izo" Hua namuona fala sana anae andika au kuongea ivo
 
Hiyo Avatar yangu ni picha ya empty profile tu, lakini hilo neno Polymath' kwenye iyo Avatar ndo imebeba uhalisia wa Avatar nzima, "POLYMATH" ni nini.'? Polymath' linaeleza mtu ambaye ni Expert kwenye more than one category
I am'_ _ _ _ _
-Dreamer
-business man
-inventor
-investor
-futurist
-artist
-mathematician,
-Programmer
Siku najiunga jf nilipata shida kati ya kuchangua kati CYBERGATES AU POLYMATH kama Id: sema cybergates nalipenda zaid.
Write your reply...
 
Back
Top Bottom