Je, awamu ya sita ipo kwaajili tu ya kurekebisha makosa ya Awamu ya Tano?

Badilisha chama acha kukariri
 
Hahaaa
Kumbe tanzania hakuna Corona afu bi mkubwa anasema ipo ..aisee bi mkubwa siyo mzalendo hata kidogo ila magufuli alikiwa jembe kwerikweri ....au nasema uongo ndugu yangu ..msema kweri ni mpenzi wa mungu na razima ukweri usemwe
 
Aliongoza nchi katika uhalisia kwa vitendo na maneno hakuwa muumini wa polifix hio ndo shida muulize mwanao raisi wa Tanzania ni nani atamtaja mwamba wa africa alijaa kwenye mioyo ya watu amekufa kwa heshima hayupo lakini anaishi pamoja nasi
Kama alikua anazindua mpka choo cha stand na kuwa covered na media zote kwa nn hata vichaa mtaan wasimjue?
 
Aliongoza nchi katika uhalisia kwa vitendo na maneno hakuwa muumini wa polifix hio ndo shida muulize mwanao raisi wa Tanzania ni nani atamtaja mwamba wa africa alijaa kwenye mioyo ya watu amekufa kwa heshima hayupo lakini anaishi pamoja nasi
Mkuu 'beny jr', haya unayoyaandika hapa ni kweli yanatoka moyoni mwako?
Hukuona ubaya wowote aliofanya Magufuli?

Magufuli "angejaa sana mioyoni mwa watu" kama tabia zake zisingekuwa mbaya. Alikuwa ni mtu mwenye tabia mbaya, pamoja na kwamba yalikuwepo mazuri ambayo yangemjaza ndani ya mioyo ya watu hao kama si kwa tabia zake mbaya..

Ukisema Magufuli "...amekufa kwa heshima"; sielewi una maana gani na neno 'heshima'. Kifo kinachosababishwa na kiburi chake tu kutotambua hatari ya ugonjwa uliomsababishia kifo, wewe unaita hali hiyo kuwa ya heshima?

Mimi, kama wewe, ningempenda sana Magufuli kwa baadhi ya mambo ya msingi sana aliyokuwa akiyasimamia kwa ajili ya manufaa ya nchi hii; lakini heshima yangu kwake ilitoweka kwa matendo yake mengi mabaya.
 
Shujaa hufa ili kuokoa maelfu hata kama ni covid imemuua sawa tu cha msingi hakuruhusu hali ya panic na hofu ambayo ingeua wananchi wengi zaidi! Huo ni ushujaa!
 
Usimtishe mama mlivyokuwa mnauwa watu kuwateka kuwapoteza kuwapiga risasi kuiba kura kupokonya Mali za wafanyabiashara mliona sawa?
 
Huwezi amini yule ibilisi kawa skeleton mungu fundi
 
Duh.. Kilaza wa standadi geji
[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwamba anakosea anavyowaondolea watu waliobambikiwa kesi?
 
Hilo la kusahihisha makovu ya Awamu ya Mwendazake halikwepeki. Miaka 5 iliyopita Tanzania ilikuwa inapita kwenye BONDE LA MAUTI. Niliyaona haya kwenye uzi wangu huu hapa:

 
Shujaa hufa ili kuokoa maelfu hata kama ni covid imemuua sawa tu cha msingi hakuruhusu hali ya panic na hofu ambayo ingeua wananchi wengi zaidi! Huo ni ushujaa!
Unaonyesha kiasi cha ujinga uliokughubika, kama alivyokuwa nao huyo unayemuongelea hapa.

Hapa ni karne ya ishirini na moja, bado tuna watu wajinga kama nyinyi, ni aibu kubwa sana kwa taifa letu. Yaani maendeleo yote ya sayansi yamewapita pembeni kabisa, ni kama mnaishi kwenye pango lenu kusikofikiwa na taarifa kabisa?
 
Awamu ya sita ipo kurekebisha makosa na mapungufu ya magufuli na kuendeleza mazuri na kuanzisha mapya.
 

Yes. Ndio hivyo. Mnapokuwa na mfumo wa chama kimoja cha siasa (de facto); yaani chama dola - CCM, ndivyo inavyokuwa.

Hiyo ndiyo namna pekee utawala unaokuwa madarakani unavyoweza kujipambanua na utawala uliopita na kuthibitisha ubora/weledi wake (value-added).

Baada ya kujihakikishia CCM kutawala milele, mchezo siku zote utakuwa CCM vs CCM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…