Ni vizuri aliishia kuwa Kanali tu maana angeendelea cheo kingine angeharibu kazini kwa namna fulani. Kuna nchi huwa wanafuatilia unavyoishi na familia na majirani zako na wafanyakazi wenzako. Siku kazini ukimchapa kofi fundi alikuwa anarekebisha mlango, sahau kupanda cheo. Ukigombana na mashabiki kisa mpira hufai napo. Ukipiga watoto wako kiholela na kuwanyanyasa hufai. Ukimpiga mkeo na ikajulikana tena hapo acha kazi kama unataka. Ukitalikiana na mkeo na chanzo ni wewe kumsaliti au makosa unayo wewe chance za kupanda ngazi zinapungua more than 50%.
Sifa mojawapo za kamanda wa jeshi ni kuwa na common sense, good reasoning, risk assessment, morale na anger management. Mfano hapo usiku kuwaamsha mkatafute kuku alitakiwa azingatie usalama wenu (risk assessment) na saikolojia yenu (morale) kwanza kabla ya thamani ya jogoo, alitumia hasira.
Wabongo wengi watakwambia alikuwa anawajenga, wanaamini katika shida na kuteseka. Ndio haohao wanaamini kwenye kula ugali mkubwa ndio kupata nguvu.
Kwa uandishi wako nina hakika huna elimu kubwa na ambavyo aliwakomalia elimu.
Mambo mengine alikuwa strict which is good