Mohammed wa 5
JF-Expert Member
- Jun 20, 2022
- 1,215
- 3,035
- Thread starter
- #121
Mkuu sikupingi Yale malezi yamenisaidia Sana kupambana na maisha na kuwa makini na nidhamu kwa kila jamboAliwafundisha kuthamini na kutambua fursa. Mfano kwenye tofali na mchanga sidhani kama atatokea yoyote kati yenu atakayetaka hata kuiona nyumba inaharibika au kuuzwa. Pia aliwaandaa vyema kuyakabili na kiyatekeleza majukumu ya kimaisha. Kwa mfano kwenye kumwagilia miti na bustani; na dunia ya sasa ndivyo ilivyo huwezi pata pale ambapo hujapaandaa/kuwekeza. Na pia dunia haina huruma ndio maana akawa anahakikisha anakula na nyinyi sahani moja kwenye maagizo yake. Aliwandaa vyema na dunia yetu hii. Kongole nyingi kwake. Hata sisi kwetu tulipitia hayo; mwanzoni na kwa fikra za kitoto tuliona manyanyaso lakini baadae tuliona faida kubwa sana haswa tulipoanza kujitegemea au kwenda kuishi ugenini; wanashangaa vijana rika lakini sisi malezi tofauti na utekelezaji wa majukumu upo vizuri tofauti na wenyeji