Angalia maisha yako ya sasa, yameathiriwa vibaya au vizuri na namna mzee alivyowalea.
Nikupe stori kuhusu (sisi)
Baba yetu alikuwa mdemokrasia sana. Nyumbani tulikuwa watoto wengi sana, mimi nilkuwa mdogo sana. Kaka zangu waliwekeana zamu ya kwenda kuchunga ng'ombe, lakini ilikuwa ikitokea mwenye zamu hajaenda baba alikuwa anaenda mwenyewe kuwachunga. Yeye ilikuwa ukiwa na shida na kitu ukimfuata atakwambia nenda kaombe ulikoshinda siku ambayo hukuenda kuchunga ng'ombe.
Tabia ya baba ya kuwa mdemokrasia sana ilifanya kaka zangu wengi waachie shule njiani. Maana ilikuwa kama hawajaenda shule atauliza "vipi mbona hujaenda shule ukijibu naumwa.. atakwambia tu, shauri yako utaumwa mpka uzeeni"
Yeye alikuwa mchapakazi sana, na alikuwa na mafanikio makubwa sana, ameacha mali nyingi sana ambazo sasa watoto wake wanagombaniana [emoji23]
Alipenda kufundisha kwa mifano sana, kwa mfano kipindi wakija watu wazima kuomba kazi ya kupalilia migomba au mahindi atakutuma ukamuoneshe shamba, ukirudi atakwambia "umeona yule mtu, alivyokuwa kama wewe alikuwa anacheza, usipokuwa makini utakuja nawe kuomba vibarua ukiwa mzee".
Na utu uzima huu, nimegundua maneno pekee hayatoshi kuleo mtoto, muda mwingine misimamo kama ya baba yako ndo inafanya mtoto awe kwenye njia flani nzuri, hata si ukatili. Malezi ya kubembelezana si maadili yetu, tumeiga tu ndo maana jamii sasa imepotoka maana hata mtoto akikosea eti inabidi uongee naye, umbembeleze (nani kasema) ujinga na upumbavu upo kwenye akili ya mtoto, anatakiwa anyooshwe hata kwa viboko.
Tumechukua tamaduni za watu, sasa hata namna ya kulea watoto wetu tunaita ukatili. Katili atanyima msosi, atakunyima pa kulala. Lakini adhabu ya kubeba tofali ukizingua ilikuwa si ukatili, alikuwa anakuandaa kukabili nyakati ngumu katika maisha, pia alikuwa anakuandaa kusimamia msimamo, ndo maana ilikuwa usipomwigilia miti hata saa nane ya usiku utaenda mwagilia. Hiyo ilikuwa na maana kuwa unakiwa kufanya wajibu wako kwa wakati sahihi.
Kwa upande wangu baba yako alikuwa sawa sana.