Hakuna kudumaa mzeeNi umasikini na stress ndio zilizokuwa zinamsumbua mzee wenu.
Mtoto wa darasa la sita hauwezi kumbebesha tofali 100 tena umbali wa mita 250..mzee wenu alikuwa hana pesa ya kuwalipa watu wabebe tofali akaona awatumie nyinyi.
Tambua kazi zinaendana na umri ukimpa mtoto kazi ngumu lazima mtoto atadumaa.
Hata sisi baba yetu alikuwa major general lakini hajawahi kutuendesha kama punda
Utafiti maandaziKuna utafiti unaonesha watoto walioteswa au kuwa mbali na baba zao, hutafuta upendo kwa wanaume baki, au ikitokea mwanaume akamuonesha ukarimu na wema fulani, basi atakuwa karibu naye kwani hakuyapata hayo kwa Baba yake, na ukaribu ukupitiliza, yanatokea haya yanayopigiwa mwayo zama hizi.
Haya mambo mengine ni child abuse, unyanyasaji wa watoto.
Dharau kwahyo umejua kuwa jamaa ajabukuaNi vizuri aliishia kuwa Kanali tu maana angeendelea cheo kingine angeharibu kazini kwa namna fulani. Kuna nchi huwa wanafuatilia unavyoishi na familia na majirani zako na wafanyakazi wenzako. Siku kazini ukimchapa kofi fundi alikuwa anarekebisha mlango, sahau kupanda cheo. Ukigombana na mashabiki kisa mpira hufai napo. Ukipiga watoto wako kiholela na kuwanyanyasa hufai. Ukimpiga mkeo na ikajulikana tena hapo acha kazi kama unataka. Ukitalikiana na mkeo na chanzo ni wewe kumsaliti au makosa unayo wewe chance za kupanda ngazi zinapungua more than 50%.
Sifa mojawapo za kamanda wa jeshi ni kuwa na common sense, good reasoning, risk assessment, morale na anger management. Mfano hapo usiku kuwaamsha mkatafute kuku alitakiwa azingatie usalama wenu (risk assessment) na saikolojia yenu (morale) kwanza kabla ya thamani ya jogoo, alitumia hasira.
Wabongo wengi watakwambia alikuwa anawajenga, wanaamini katika shida na kuteseka. Ndio haohao wanaamini kwenye kula ugali mkubwa ndio kupata nguvu.
Kwa uandishi wako nina hakika huna elimu kubwa na ambavyo aliwakomalia elimu.
Mambo mengine alikuwa strict which is good
Na anayetunga pepa maji ndyo anajua?I couldn't agree more. Wabongo wanapenda sifa za kijinga. Mtu anakwambia yeye kateseka kuliko wewe as though kuna tuzo za mateso.
Unatesa watoto as if wanaenda vitani mwisho wa siku hata ajira wanakosa sasa umewaandaa na nini? Hayo mateso yanawafikisha wapi?
Ni bongo ambapo professor anaona sifa kufelisha wanafunzi kumbe inampa sifa mbaya mwenyewe kwamba hajui kufundisha na kuzalisha failures tu wanaozagaa mtaani.
Kuna kujenga mtu na kutesa mtu. Huyu dingi alikua mtesaji.
Pole sana mkuu...🤣🤣Bwege we, wananishangaa daladalani.
Unaweza kusema hivyo maana ndio jukumu rahisi tunaloliweza. Wenzetu kila tukio hulichunguza na wahusika kuhojiwa. Sisi tunakimbilia kuadhibu!Utafiti maandazi
Hakika Reuben ni nani?Nakupata vilivyo Ndugu HAKIKA REUBEN
Nyie wa we junior wee ndo mnatuharibia taifa sasa napo kuna unyanyasaji ganiHaya mambo mengine ni child abuse, unyanyasaji wa watoto.
Watanzania wengi kama wewe hawana nuance, to them, it's all or nothing.Nyie wa we junior wee ndo mnatuharibia taifa sasa napo kuna unyanyasaji gani
Pitia huu uzi wa mpumbavu utajua kama mzee wenu aliwatesa au la; Ushauri: Lecturer ananitaka kimapenzi, ananitishia yeye ndio mwenye hatma ya matokeo yanguBaba yangu alikuwa kanali wa jeshi la wananchi (jwtz)huko kusini mwa Tanzania mkoa unaozalisha mahindi kwa wingi hapa nchini mzee wetu alikuwa mkali Sana
Nakumbuka mwaka 2008 wakati Mimi nko darasa la sita ,kaka yangu mkubwa first born yupo form one na mdogo angu marehemu kwa Sasa (r.i.p) tulipewa kazi ya kubeba tofali 100 Mimi na Kaka, mdogo wetu abebe tofali 50 na sehemu zilipokuwa tofali ni mbali Sana hakuna gari unabeba kichwani unavuka Kama mitaa 3 mikubwa nakumbuka siku Ile tulibeba tofali mpaka unalia njia nzima unapumzika ukikutana mtu mnaye fahamiana anakupiga tafu kidogo,nakumbuka bimkubwa alikuwa ana toa machozi kutuhurumia na sauti kwa mzee hana ilibidi tupambane tu
Tukio lingine home tulikuwa na eneo kubwa mzee alipanda miti ya matunda na migomba kila mtu alipewa miti yake ole wake mti wako unyauke utachezea fimbo na adhabu zakutosha
Ukirud shuleni baada ya kula unachukua ndoo zako unaenda mtoni kuchota maji tulikuwa tunaisha karibu na mto na usiku ata arudi saa 6 anachukua tochi anapita kugagua kila mti Kama umepata maji ya kutosha ole wako usimwagilie utaenda mtoni usiku kuchota maji umwagilie
Nakumbuka nilikuwa mchezaji mzuri Sana wa mpira nishachaguliwa Sana umintashuta na umisenta kwenda kuwakilisha shule kwenye soka Ila tatizo mzee alikuwa hataki kusikia habari za mpira alichotaka yeye ni kusoma tu na saa 12 jioni uwe ndani kipaji kikapotea...
Tukio lingine nyumbani tulikuwa tunafuga kuku Kuna siku moja kuku mmoja jogoo kumbe hakulala ndani na sisi hatukukagua na tulikuwana na jogoo mmoja tu kwa wakati huo usiku kumbe mzee ajalala anasikilizia saa 9 jogoo awike kimya saa 11 alfrajiri Tena kimya jogoo ajawika akatoka kwenda chumba Cha kuku kuangalia kumbe yule jogoo hayupo nakumbuka tuliamsha wote nyumba nzima tukatafute kuku Hadi tumpate ilikuwa kasheshe kila pori tunatafuta hatuna ata tochi tulifanikiwa kumpata asubuhi kesi ikaisha
Ni matukio mengi Sana yalitokea home mzee alikuwa mafia afu acheki ovyo majirani walikuwa wanamuogopa Sana
Nw kastaafu yupo nyumbani tu Japo ukali umepungua wajukuu na ndugu wanaoishi pale wananienjoy tu
Ndio chiefKunyauka kisa ugonjwa au cio
50% alitufundisha maishaNatumai ushakuwa mtu mzima sasa. We unaonaje, mliteswa ama mlifundishwa maisha?
Sahihi mkuu mshua saiz yupo piece Sana Yani wajukuu wanamchezea Hadi bsKuna kaumri washua wakifika huwa na ukali ukali sometimes hata usio na maana ila wakizeeka wajukuu wanawachezea sana
Poker mkuuMdingi hawezi kukutesa ulimtafsiri vibaya shukuru Mungu umebahatika kuishi na mshua mpaka anazeeka
Miss you Dad
Sikupingi mkuu nimekulewa SanaKama malezi uliyopitia yalikuwa sahihi basi ungejua jibu la hili swali lako bila kuja kuuliza hapa ila inaonekana malezi aliyowalea baba yenu hayajaleta matokeo chanya au aliyoyadhania kwa asilimia 100%. Maana yake kuna sehemu mzee wako alikosea. Mfano unatumia jibu alilotoa member numbisa kujibu members wengine.
Malezi kama haya mara nyingi yanafanya baba na mtoto wasipatane ukubwani kitu ambacho sio kizuri kwa mzazi lakini hasa mtoto. Mimi sitaki hata kufikiria malezi yangu lakini ndio yamenifanya niwe jasiri na katili, real fighter lakini sio hapo tu bali kwenye akili pia. Tatizo mahusiano ya baba na mtoto ndio hayapo, kitu muhimu zaidi kwenye maisha.
Malezi kama haya yana uzuri na ubaya wake, ukipatia mtoto atakuwa jasiri, fighter na anayetumia akili kufanya maamuzi binafsi na ukikosea sehemu mtoto atakuwa muoga, asiyejiamini na asiyetumia akili yake kufanya maamuzi binafsi bali ataendeshwa kwa hisia na mitazamo ya watu.
Bila shaka umepata jibu lako hapo.
NB: Mzee alikuwa mjeshi vilevile.
Ni kweri kabisa mtoto lazima ajue na haweze kufanya Kaz ndogo ndog za homeKuna muda home kuwa jeshi inasaidia
Watoto wanatakiwa kuwa na majukumu sio mlendamlenda tu unakuta watoto wapo hata kufyeka nyasi hawawez