Je, Baba askofu wa Kanisa Katoliki anaweza kugombea Ubunge?

Je, Baba askofu wa Kanisa Katoliki anaweza kugombea Ubunge?

Nauliza tu wadau kama baba askofu wa Kanisa Katoliki anaweza kugombea ubunge.

Kwa mfano baba askofu Ruwaich anaweza kugombea ubunge jimbo la Ilala?

Maendeleo hayana vyama!
Ungemwuliza Padre wenu yuko sweden atakuwa na jibu zuri
 
Kwanza neno Askofu kwa sasa, linatumika sawa na neno Rais.

Tuna Rais wa nchi lakini pia kuna watu wanajiita ni rais wa wacheza bao Mbagala.

Askofu wa Kanisa mwenye wakfu hawezi kugombea Ubunge lakini maaskofu wanaojitangaza baada ya kuwapata watu wachache wajinga wa kuwafuata, wanaweza kugombea nafasi yoyote, na wanaweza kufanya chochote, hata kucheza picha za ngono au kubugia konyagi mpaka kuwa chakari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Labda kama kuna kanuni/sheria mpya za kanisa Katoliki, Nakumbuka marehemu Padri Severino Supa wa kanisa la Katoliki jimbo la Dodoma, alikuwa mbunge machachari wa TANU mwaka 1975 - 1980, lakini dhahama ilimkuta katika uchaguzi wa mwaka 1980 ambapo aliangushwa na Mchungaji Simon Chiwanga wa kanisa la Anglican, lakini alipambana vilivyo mahakamani akitetewa na wakili marehemu Chambakali, na mwaka 1982 Hukumu ya Judge Marehemu Rukagikingira ikamvua ubunge Chiwanga aliyekuwa akitetewa na wakili Marehemu Mbezi, na uchaguzi uliporudiwa mwaka 1983, Padre Severino Supa akarejea kwenye ubunge wake. Kumbukumbu zangu zinaonyesha kipindi chote Padre Supa alikuwa akiendelea na upadre.
Hakuna Padre hapa Tanzania ambaye alikuwa mbunge halafu aliendelea kutoa huduma kama Padre japo anaendelea kuwa Padre, kwa sababu tu Upadre ni sakramenti isiyofutika. Upadre unaweza kufutika ebdapo tu kama kurakywa na nullification.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom