Hakuna mtu anayeandaliwa kuwa Askofu bali anaandaliwa kuwa Padre. Na Padre yeyote anaweza kuwa Askofu. Kitu msichokijua ni kwamba hata Pope Francis hana tofauti na padre yeyote bali kile ni cheo kilichowekwa na kanisa. Kuna siku vijana waliobadili dini kutoka uislamu kwenda Ukatoliki walimuuliza padre mmoja anaitwa Padre Peter Morgan, ni paroko wa parokia mmoja Liverpool, kwamba nini tofauti ya yeye na Francis Papa. Akawaambia kwanza wote ni mapadre ila mmoja ni kiongozi wa ngazi ya juu. Hivyo hilo swala la kwamba wanaandaliwa wakiwa wadogo kuwa maaskofu ni uongo wa hali ya juu na uliotukuka.
Maaskofu wanapendekezwa na kwa tabia zao, majina matatu yanapelekwa kwa Pope yeye analichagua moja na kurudisha kwa waliolipeleka na hivyo kuwa Askofu Mteule kabla hajawekwa wakfu. Askofu Filbert Mhasi kwa mfano wa jimbo la Masasi, nilikua naye Seminarini kabla sijaacha na alikua nyuma yangu madarasa manne na nilikua kiranja wake na mpaka anateuliwa hakujua kabisa kama angekuwa Askofu. Hata alipopigiwa simu na mjumbe wa Baba mtakatifu hakujua kwanini alipigiwa simu.
Jaribuni kuandika vitu mnavyovijua ama fanyeni utafiti kabla hamujawadanganya watu hapa kwenye Forums