Labda kama kuna kanuni/sheria mpya za kanisa Katoliki, Nakumbuka marehemu Padri Severino Supa wa kanisa la Katoliki jimbo la Dodoma, alikuwa mbunge machachari wa TANU mwaka 1975 - 1980, lakini dhahama ilimkuta katika uchaguzi wa mwaka 1980 ambapo aliangushwa na Mchungaji Simon Chiwanga wa kanisa la Anglican, lakini alipambana vilivyo mahakamani akitetewa na wakili marehemu Chambakali, na mwaka 1982 Hukumu ya Judge Marehemu Rukagikingira ikamvua ubunge Chiwanga aliyekuwa akitetewa na wakili Marehemu Mbezi, na uchaguzi uliporudiwa mwaka 1983, Padre Severino Supa akarejea kwenye ubunge wake. Kumbukumbu zangu zinaonyesha kipindi chote Padre Supa alikuwa akiendelea na upadre.