Je, baraka za Mungu ni mafanikio ya kimwili kama utajiri au zipo nyingine tofauti na utajiri?

Mynd177

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2022
Posts
2,817
Reaction score
5,141
Wakuu, habari za leo, natumai Jumapili iko poa kwenu,

Kama kichwa kinavyosema, je, baraka za Mungu tuzihesabu kupitia mafanikio yetu ya kimwili kama pesa, majumba, magari ya kifahari, mke mrembo, simu kali na mengine mengi au kuna namna nyingine anaweza kuwa anatubariki ila sisi hatujui?

Kwa nini nasema hivi? Nimeona mara nyingi watu tukipitia changamoto tunahisi labda tumemkwaza Mungu kwa namna fulani na tunaanza kuhisi wale ambao mambo yanawaendea vema basi Mungu anawapa favour, sijui ninyi mnaonaje?

Karibuni tujadili hili.
 
Wakuu, habari za leo! Natumai jumapili iko poa kwenu..
Kama kichwa kinavyosema.. je baraka za Mungu tuzihesabu kupitia mafanikio yetu ya kimwili kama pesa, majumba, magari ya kifahari, mke mrembo,simu kali na mengne mengi... Au kuna namna nyingine anaweza kuwa anatubariki ila sisi hatujui.?
Kwa nn nasema hivi??
Nimeona mara nyingi watu tukipitia changamoto tunahisi labda tumemkwaza Mungu kwa namna fulani...Na tunaanza kuhc wale ambao mambo yanawaendea vema basi Mungu anawapa favour...SIJUI ninyi mnaonaje..
KARIBUNI TULIJADILI HILI.
Baraka zipo lakini tusisahau ile laana ya asili pale Eden
Baraka zipo lakini kwenye mikanganyiko ya maisha watu huchuma laana
Baraka zipo lakini kwenye harakati za maisha watu hujaribu kumsahihisha Mungu
Baraka zipo lakini watu wanapofinywa kidogo tu hukimbilia upande wa giza
Baraka zipo lakini kila mmoja wetu ana kipimo chake[emoji1545]
 
Mkuu umenena vema, lakini je unamaanisha kuwa Mungu ana upendeleo?? na hapo pa kumsahhsha Mungu, je yeye anataka nini kutoka kwetu...
 
Wakuu, habari za leo! Natumai jumapili iko poa kwenu..
Kama kichwa kinavyosema.. je baraka za Mungu tuzihesabu kupitia mafanikio yetu ya kimwili kama pesa, majumba, magari ya kifahari, mke mrembo,simu kali na mengne mengi... Au kuna namna nyingine anaweza kuwa anatubariki ila sisi hatujui.?
Kwa nn nasema hivi??
Nimeona mara nyingi watu tukipitia changamoto tunahisi labda tumemkwaza Mungu kwa namna fulani...Na tunaanza kuhc wale ambao mambo yanawaendea vema basi Mungu anawapa favour...SIJUI ninyi mnaonaje..
KARIBUNI TULIJADILI HILI.
Kumbukumbu La Torati 8:18.
 
Nimesoma hapo! lakini wapo wenye mafanikio ya kimwili yaani pesa af wanafanya uovu tena sometimes wa kutisha je Mungu anakubaliana nao???!
Matajiri hufanya kwa matakwa yao wenyewe lakini Mungu huwa hapendezwi kamwe na hizo tabia zao.

Umesahau Mfalme Nebuchadnezzar alivyoshushwa toka juu hadi kupelekwa kule kondeni?

MITHALI 28:6
Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,
Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.
 
MUNGU hakubaliani nao kamwe, pia si kila Tajiri hutokana na baraka za Mungu, wapo wengine wenye utajiri wa masharti ya nguvu za giza.

ZABURI 75:7-8.

7. Bali Mungu ndiye ahukumuye;
Humdhili huyu na kumwinua huyu.

8. Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe,
Na mvinyo yake inatoka povu;
Kumejaa machanganyiko;
Naye huyamimina.
Na sira zake wasio haki wa dunia
Watazifyonza na kuzinywa.
 
Matajiri hufanya kwa matakwa yao wenyewe lakini Mungu huwa hapendezwi kamwe na hizo tabia zao.

Umesahau Mfalme Nebuchadnezzar alivyoshushwa toka juu hadi kupelekwa kule kondeni?

MITHALI 28:6
Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,
Kuliko mpotofu wa njia angawa ni tajiri.
Mkuu ahsante kwa jbu hili! kumbe kuwa tajir au maskin sio kesi kwa Mungu!! jambo la msingi ni kufuata njia zake. sio?! sasa hii feeling ya kuhc Mungu katuacha na anatuadhibu tukipata changamoto za kiuchumi au kiafya na nyngne nyng huwa inatoka wap?....
 
Jibu utalipata katika Biblia , Yesu alipopandishwa mlimani na shetani na kuahidiwa Mali ya Dunia kama atamsujudi. Kwa ufupi ni jinsi unavyocheza mchezo wa maisha.
 
Mkuu umeniacha njia panda, tafadhal nieleweshe hapo kwenye namna ya kuucheza mchezo wa maisha!.. af kumbe na Shetani nae anatoa mali! s Mungu tu.?
 
Baraka kubwa kuliko zote ni afya.. hakuna kitu cha thaman kama afya duniani

Matajiri wengi wamechuma mali kwa njia haramu ni wachache sana wenye mafanikio ya halali. Maskini wengi hawajatoboa kisa kukosa uthubutu 🙌

Mwisho wa siku , tajiri na maskini wote wanaenda chooni, wote wanakufa... kila mmoja ana masaa 24 katika siku!
 
Baraka kubwa kuliko zote ni afya.. hakuna kitu cha thaman kama afya duniani

Matajiri wengi wamechuma mali kwa njia haramu ni wachache sana wenye mafanikio ya halali. Maskini wengi hawajatoboa kisa kukosa uthubutu
 
Mkuu umenena vema, lakini je unamaanisha kuwa Mungu ana upendeleo?? na hapo pa kumsahhsha Mungu, je yeye anataka nini kutoka kwetu...
Mungu hana upendeleo ndio maana hutoa vyote kwa wote bila upendeleo
Hutoa pumzi, jua, na hali zote za hewa kulingana na jiografia ya mahali bila kumbagua huyu na kumpa yule

Wanaotaka kumsahihisha Mungu ni wanadamu wasioridhika na kipimo chao
 
nimekuelewa mkuu.
 
Back
Top Bottom