Je, CCM ilisajiliwa UPYA ulipoasisiwa mfumo wa Vyama vingi Julai 1992?

Salaam, Shalom!

Swali hili nimekuwa nikujiuliza kitambo sasa kuwa, Ulipoasisiwa mfumo wa Vyama vingi July 1, mwaka 1992, CCM iliyokuwa chama pekee katika mfumo wa chama kimoja, ilipata usajili UPYA na kujitenga na kujishikamanisha na system?

Maana ukikiangalia chama hiki Kwa nje ni kama chama Cha siasa, lakini Kwa ndani, nionavyo ni zaidi ya hapo.

Wajuzi wa mambo watujuze ikiwa CCM ilipata usajili mpya Ili kuwa sawa na vyama vingine vya siasa, au walifanya Yale mambo ya KINYONGA kujibadili RANGI ilhali ni kinyonga yule yule?

Waonaji katika Ulimwengu Ule, Kila wakikitafuta, kinasoma kitu kingine, tuambieni mlifanyaje fanyaje? Pascal Mayalla

Karibuni🙏
Unayo report ya Tume ya Jaji Francis Nyalali? Hebu pitia kama rejea hizi hoja zako Za msingi sana
 
Siyo hewa ni haramu

Akitokea Mwanasheria ahoji mahakamani orodha ya vyama vyenye usajili sijui kama jamaa watavuka

Labda walijisajili bila utaratibu. Yaani hawakufuata sheria ya usajili wa vyama
🤣kwahiyo hayupo mwanasheria huyo hata kwa wpinzani wasomi?
 
Mfumo wa vyama vipya ilipoanzishwa mwaka 1992, na kuundwa kwa ofisi ya msajilli wa vyama vya siasa. Vyama vyote viliwasilisha nyaraka za usajili kwa msajili wa vyama vya siasa, na kupokea maelekezo ya kupata usajili na kukabidhiwa kanuni, vigezo, masharti na taratibu za kufuata ili hatimae kupata usajili wa kudumu.

Vyama vyote, ikiwa ni pamoya na CCM vilifuata utaratibu na kupata usajili wa kudumu.
Kwahiyo unamaanisha Msajili anayo hati ya usajili wa CCM ya 1992?

Makao makuu ya CCM cheti hicho Cha usajili kipo utuwekee hapa?
 
Mkuu, pitia vifungu hivi vya Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act) ili upate jibu. Ni vifungu vya 8 (1) na 7 (2)

.8–(1) Every political party other than the political party registrable pursuant to subsection (2) of section 7, shall apply and be registered in two stages, after fulfilling all the conditions prescribed for each stage.

7 (2) Notwithstanding the provisions of subsection (1) of this section Chama cha Mapinduzi, also known by the acronym CCM, which was, immediately before this Act, the sole political party for the whole of the United Republic shall, on the coming into effect of this Act, and without further requirement, be deemed to have been fully registered as a political party and shall be issued with a certificate of registration in accordance with this Act.
 
Tuendelew kusubiri mkombozi mkuu wanhi😅

Mindset za wabongo wengi ni kuwa ATALUJA MTU KUTUKWAMUA. Sisi wenyewe hatuwezi😆
Tutafika,
twendeni pole pole kwa mipango mahiri na mikakati ya kuleta umoja na mshikamano.
 
Mkuu, pitia vifungu hivi vya Sheria ya Vyama vya Siasa (Political Parties Act) ili upate jibu. Ni vifungu vya 8 (1) na 7 (2)

.8–(1) Every political party other than the political party registrable pursuant to subsection (2) of section 7, shall apply and be registered in two stages, after fulfilling all the conditions prescribed for each stage.

7 (2) Notwithstanding the provisions of subsection (1) of this section Chama cha Mapinduzi, also known by the acronym CCM, which was, immediately before this Act, the sole political party for the whole of the United Republic shall, on the coming into effect of this Act, and without further requirement, be deemed to have been fully registered as a political party and shall be issued with a certificate of registration in accordance with this Act.
Fafanua Kwa lugha ya Nyerere hata st kayumba waelewe.
 
Salaam, Shalom!

Swali hili nimekuwa nikujiuliza kitambo sasa kuwa, Ulipoasisiwa mfumo wa Vyama vingi July 1, mwaka 1992, CCM iliyokuwa chama pekee katika mfumo wa chama kimoja, ilipata usajili UPYA na kujitenga na kujishikamanisha na system?

Maana ukikiangalia chama hiki Kwa nje ni kama chama Cha siasa, lakini Kwa ndani, nionavyo ni zaidi ya hapo.

Wajuzi wa mambo watujuze ikiwa CCM ilipata usajili mpya Ili kuwa sawa na vyama vingine vya siasa, au walifanya Yale mambo ya KINYONGA kujibadili RANGI ilhali ni kinyonga yule yule?

Waonaji katika Ulimwengu Ule, Kila wakikitafuta, kinasoma kitu kingine, tuambieni mlifanyaje fanyaje? Pascal Mayalla

Karibuni🙏
Haikusajiliwa. Ni hivi: tungekuwa na mahakama huru CCM ingeshafutika siku nyingi. Ngoja nikuulize swali la kutafakarisha. Majaliwa ni waziri mkuu wa nchi gani? Si wanasema ni Tanzania ambayo ni Tanzania bara + Zanzibar? Zanzibar ana sauti au anajulikana? Tukisema ni waziri mkuu wa Tanzania bara tutakuwa tumekosea?
 
Unazidi kuongeza maswali tata!!

Yaani Zanzibar na Tanganyika ziungane, mchanga uchanganywe, Tanganyika ikapotea.

Cha kushangaza Zanzibar Bado IPO?

Ni aina Gani ya Muungano hii? Labda Nguruvi3 atufafanulie.
 
Back
Top Bottom