TheDreamer Thebeliever
JF-Expert Member
- Feb 26, 2018
- 2,490
- 3,584
- Thread starter
- #21
πππππππBinafsi Nimechana sana hizo CV Uchwara za watafuta kazi.
Ukinikuta nalinda ukaacha barua yako, mwisho ni Dustbin.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
πππππππBinafsi Nimechana sana hizo CV Uchwara za watafuta kazi.
Ukinikuta nalinda ukaacha barua yako, mwisho ni Dustbin.
Umeeongea ukweli lakini kila mwanadam anapita changamoto ,hata Mo Dewji na hela zote zile some time anapitia changamoto km kutekwa,kutukanwa mitandaoni n.k .Kiukweli naweza nikasema graduate sio rahisi kupitia changamoto sanaaa kama inavoelezwa, ukiwa umesoma hadi elimu ya juu maisha ya kula, kuendesha maisha hayawezi yaka kusumbua. Kwakua elimu ya juu ni elimu kubwa sana ambayo kwa namna yeyote lazima tu ikuweke pahala pazuri. Mimi nilimaliza masomo ya uhandisi mara moja nilienda ERB nikaomba SEAP nikapata moja ya taasisi kubwa hapa nchini ya kihandisi (serikali) na nikawa nalipwa ukijumlisha na kazi za kati kati ya mwezi kwa kila mwezi nikawa napata si chini ya laki 6 na nusu. Baadae nikaona haitoshi kabisa. Ndipo nilipoanza tafuta sehemu nyingine tena private companies, na kama mjuavyo Hata vitabu vya dini vimeandika ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona. Baada ya kuweka nia, nilifanikiwa kupata kazi nzuri na inalipa vizuri sana. Na baada ya hapo nimeendelea kufanikiwa kupata nafasi mbalimbali katika kampuni nyingine nyingi.
Hebu niwaambieni kitu kimoja, graduate lazima uwe na janja janja lazima uwe muongeaji hata kama vitu una idea navyo basi zungumza as if unavielewa hakuna atakaye lala njaa.
Hizo ndio changamoto baada ya ku graduate unajikuta hauna hata demu wa kupanga naye mipango baada ya yule wa chuo kukupiga kibutiπππHuwa nakupenda tu sijui kwann mkuu...nimekuja pm chek
Huyu ni mpuuzi.Bibie anasema kama hujatuma barua 100 na kupeleka proposal 100, ujue hupitii changamoto bali ni Uzembe tu unakusumbua.
So kabla hujawasilisha malalamiko zingatia vigezo na masharti.
Mjumbe hauwawi.
View attachment 1651033
Hiyo noma sanaπππChangamoto ni nyingi sana, imagine unaambiwa uache CV kwenye kampuni Fulani kumbe wanazichoma moto zote kama takataka,
Changamoto nyingine ni connection ajira za sasa hivi especially private sector ni connection zaidi
Ukiwa na demu mpenda hela ndiyo taabu zaidiHiyo noma sanaπππ
Mkuu habari za siku?Ni miaka 4 sasa tangu nilipomaliza chuo, sikuwahi kufikifiria kama hata ningekaa mwaka mzima bila kupata kazi nikiwa kama Banker by profession,na vimini vyangu nilijipa matumaini bank zote hizi zaidi ya 50 pamoja na microfinances kweli ntakosa kazi? No no,
Uhalisia sasa baada ya kumaliza na kurudi mtaani mmh life halieleweki sambaza sana CVs kwenye Banks/microcredit aisee zingine wanaishia kupokea walinzi tu getini sidhani kama zinafika, zingine secretaries huku wakikuangalia kwa dharau, tuma kwa posta/Ems dah pesa yenyewe ya mawazo hamna kitu.nikapata kwa huyo Baba ana company yake binafsi dah naona alitaka kunipa kazi pamoja na kuwa mke tena dah. Nikajiondokea tu.
Kuna siku nilikaa ndani nikafikiria hivi nikiweka uzi jf wa kuomba kazi yoyote siwezi pata kweli, nikaona ngoja nijaribu nashukuru niliweka nikapata response za kutosha za matumaini ,nikatuma CVs nikafanya interviews, nikapata sehemu nikafanya for a year huku nikiendelea kucheki sehemu nyingine,nikapata pia kwa kutumia experience niliyoipata huko,Japo mambo hayajakaa sawa bado ila[emoji120]
Watu tusikate tamaa tuendelee kujaribu njia mbalimbali naamini ipo siku mambo yatakua poa tu.
Salama mkuu, za huko ulipo!Mkuu habari za siku?
Hongera kwa hatua ulofikia sasa,binafsi nimefuta kabisa hili wazo la kusaka ajira kwa sasa,nishauzoea mtaa. Niko chimbo nazisaka pesa bila aibu wala wenge.
Kumbe changamoto zake anataka kunihamishia na mimi piaππHizo ndio changamoto baada ya ku graduate unajikuta hauna hata demu wa kupanga naye mipango baada ya yule wa chuo kukupiga kibutiπππ
Mimi wakati nipo mwaka wa tatu enzi za kikwete vuguvugu la kuadimika kwa ajira mtaani lilikuwa limeanza wala sikutaka kupasuka kichwa nikatunza hela yangu ya boom jumlisha na hela za field nikaanza bana matumizi nakula wali maharage aisee mpka masela zangu wakina Mudy wakaanza kunipa jina la Wali ndondo.Nilikomaa mpaka tunamaliza chuo.Ile narudi town nikawa bank nina kama nina mil 1.4 aisee wazo la kutafuta aina ya biashara likaja.Nikaona kama vip hela haitoshi maana niliwaza ninunue Sanlg nimpe mtu ili izae but wakati huo Sanlg ilikuwa inauzwa mil 2.15 plus usajili.Daa kilichonitokea huko mbeleni natamani nisimulie ila sorry jamani naanza safari nadrive(ila kwa sasa nina kazi plus shughuli zangu binafsi maisha yanasonga.Kumbe changamoto zake anataka kunihamishia na mimi pia[emoji3][emoji3]
Asante pia, huku nilipo hali si mbaya sana wala si nzuri sana.Salama mkuu, za huko ulipo!
Aisee ahsante hongera pia maana kuuzoea mtaa bila aibu si kitu kidogo, na popote kambi either mtaani ama ajira ili mradi kipatikane chochote kitu. Ila ni kwanini hutaki tena kutafuta ajira? Umesumbuka sana kama sisi ? Au maamuzi tu mkuu?
Nini kilikukuta mkuu??Asante pia, huku nilipo hali si mbaya sana wala si nzuri sana.
Nakumbuka kipindi cha mwanzo naanza tu kutuma maombi kati ya sehemu 5 nilizotuma niliitwa 2, na hizo 2 nilikutana na mambo ya ajabu yalosababisha nisithubutu kutuma tena maombi sehemu yoyote bila kuwa na mtu ninae mjua pale.
Hakika umenena my dearJamani ahsante mkuu , kama ni pesa zinatafutwa muhimu upendo na amani ya moyo tu, kuna walioolewa na wenye uwezo ila hata hawaenjoy kutwa baba anawaza miradi na kusafiri tu hana time, ila waliooana na kiuwezo cha kawaida maisha simple kutwa wapo pamoja wanakula zao tembele kwa amanii[emoji7], ila tupige kazi tutafute dough mkuu.
On paper mambo ni mepesi, ila ground ni tofauti sana.Aisee acha tu, unakua unajipa matumaini ukiangalia field yako mbona kazi zipo tu kibao,kumbe ingia ground ujionee unavoishia getini kwa walinzi na CV yako[emoji849][emoji849]
Huyo na yeye hana akili anazingua.Bibie anasema kama hujatuma barua 100 na kupeleka proposal 100, ujue hupitii changamoto bali ni Uzembe tu unakusumbua.
So kabla hujawasilisha malalamiko zingatia vigezo na masharti.
Mjumbe hauwawi.
View attachment 1651033
Theory yako haiwezi kufit kila mahali.Kiukweli naweza nikasema graduate sio rahisi kupitia changamoto sanaaa kama inavoelezwa, ukiwa umesoma hadi elimu ya juu maisha ya kula, kuendesha maisha hayawezi yaka kusumbua. Kwakua elimu ya juu ni elimu kubwa sana ambayo kwa namna yeyote lazima tu ikuweke pahala pazuri. Mimi nilimaliza masomo ya uhandisi mara moja nilienda ERB nikaomba SEAP nikapata moja ya taasisi kubwa hapa nchini ya kihandisi (serikali) na nikawa nalipwa ukijumlisha na kazi za kati kati ya mwezi kwa kila mwezi nikawa napata si chini ya laki 6 na nusu. Baadae nikaona haitoshi kabisa. Ndipo nilipoanza tafuta sehemu nyingine tena private companies, na kama mjuavyo Hata vitabu vya dini vimeandika ombeni nanyi mtapewa, tafuteni nanyi mtaona. Baada ya kuweka nia, nilifanikiwa kupata kazi nzuri na inalipa vizuri sana. Na baada ya hapo nimeendelea kufanikiwa kupata nafasi mbalimbali katika kampuni nyingine nyingi.
Hebu niwaambieni kitu kimoja, graduate lazima uwe na janja janja lazima uwe muongeaji hata kama vitu una idea navyo basi zungumza as if unavielewa hakuna atakaye lala njaa.