Je, dakika yake ya mwisho duniani alisemaje? Ilikuwaje?

Wengine hufa kwa Amani kabisa, wakiwa usingizini. Kwamba ni viungo muhimu kama ini, figo na hatimaye moyo, huacha kufanya kazi, mhusika anajihisi kuchoka au usingizi. Hivyo hapati shida ya kusema siwezi kupumua n.k. hana maumivu kwani kupooza kunakuwa kumempata, na inaishia hivyo.
 
Jinsi nzuri ya kufa!
 
more milk more milk...
maneno ya mwisho ya wacko jacko
Hakumaanisha maziwa, bali madawa ya kumfanya alale, hapo alikuja akimwambia daktari wake maalum aliyeshitakiwa kwa kumuua kwa madawa.
 
Hakumaanisha maziwa, bali madawa ya kumfanya alale, hapo alikuja akimwambia daktari wake maalum aliyeshitakiwa kwa kumuua kwa madawa.
sahihi kabisa
 
Tukiwa kwenye harakati za kumuuguza mke wangu mpendwa,Mama alikuwa msaada mkubwa kwangu na kwa mke wangu,siku hiyo nimetoka hospitali kumuona mke wangu,nafika nyumbani nikaambiwa mama ananiita kwake,nikaenda na kumkuta ana huzuni sana,akaniuliza tu mgonjwa anaendeleaje?nikamwambia anaendelea vizuri sana,akaniambia "moyo wangu unaniuma sana nimeshindwa kwenda kumuona,miguu yangu haifanyi kazi kabisa,ila naamini tu Mungu ATANIKUTANISHA naye siku moja" niliondooka kwake saa tano usiku,tukaagana,akaenda kulala na mimi nikaenda kwangu,siyo mbali sana! Usiku wa kama saa nane nikapigiwa simu na mtu aliyekuwa hospitali alipokuwa amelazwa mke wangu!akaniambia hali ya mke wangu imekuwa mbaya ghafla,hivyo kama nitaweza niende asubuhi,hospitali yenyewe ilikuwa mkoa mwingine, nikakosa amani kabisa! Kufika saa kumi hivi usiku nikapigiwa simu tena! Roho ikapasuka paah!! Kuicheki ni mdogo wangu anayeishi na mama,nikapokea,akawa analia huku akiniambia "njoo nyumbani haraka" nikatoka mbio,nikafika na kumkuta mdogo wangu nje ana haha na kulia,nika muuliza kuna nini?akanikumbatia huku akilia na kuniambia niingie ndani,nikaingia mbio,nikaenda haraka chumbani kwa mama! Nikamkuta amelala huku anakoroma kwa sauti ya chini kabisa nikajaribu kkumwamsha kwa kumtikisa! Hakujibu,wala hakuamka,Akaondoka hivyo!! Tukaandaa mazishi na kumzika hapo hapo nyumbani huku mke wangu akiwa bado hospitali na akiwa na hali mbaya,siku tumezika mmke wangu ni kama alipata nafuu ghafla na kuongea na dokta aniambie nimpe mama simu aongee naye,nikamwambia mama ametoka kidoogo,akasisitiza sana,maana siku mama yangu anazikwa mimi nilienda hospitali asubuhi na mke wangu akawa anaongea kwa tabu akinilaumu kwa kumnyima kuongea na mama,akasema kuna kitu anataka amwambie mama ili mmama aniambie mimi,akasema "mimi nakufa,ila kuna jambo nataka nimwambie mama kwa ajili yako, basi tukamzika mama!! Mke wangu hakujua kuwa mama amefariki hadi siku moja alipoambiwa na mgonjwa mwingine aliyefika hospitalini akkitokea huku tunakoishi siku hiyo mke wangu alilia sana,akaniita,nikaenda,akalalamika kwa nini Mungu amemchukua Mama aliyekuwa mzima na mwenye aliyempenda sana na kumuacha yeye akiteseka kitandani kwa miaka!! Nimekuwa na wakati mgumu toka hapo ndugu zangu! Wiki mbili baada ya kumzika mama mke wangu mpenzi naye akafariki!! Lile neno alillotaka kumwambia mama aliniambia mimi mwishoni,nikamzika nyumbani pembeni ya mama aliyependa na waliopendana sana!! Mimi bado nipo kwenye msiba mzito!! Ni wiki tatu tu zimepita tangu nimzike mke wangu,mke wangu aliugua saratani ya ziwa(breast cancer) naandika huku machozi yananimwagika.
 
Poleni sana mkuu
 
Pole sana
 
Pole sana makilo,hao waliodhulumu hizo mali lazima ni makapuku mali ya dhuluma inawatesa
 
Ok,Km mngemuuliza akawajibu tungeweza kujua kuwa ni Malaika au lah!!!.
Mpaka leo najiuliza ni malaika watoa roho au ni ndugu zake waliotangulia walikuja kumkaribisha kwenye makazi mapya. Ajabu walivyoondoka wakamuacha alikuwa kama anasikitika kwanini wameondoka bila yeye..inanifikirishaga sana
 
Kaka pole sana,mungu akufanyie wepesi
 
Mtu kama huyu nitafurahi kifo chake badala ya kulia, ni maisha ya ushuhuda sana sana
Bro hata mimi kwa jinsi ya kimwili niliumia sababu alikuwa ananishauri na kuniongoza ila kwa jinsi ya Roho nilikuwa na furaha. Ameshinda na kumaliza vizuri. Mimi natumika kanisani, siku aliyokufa niliota ndoto naenda nyumbani ila nikarudi kwangu bila mchele. Hii ni kwa sababu mara nyingi nilipokuwa naenda nyumbani na watoto wangu, mzee alikuwa ananikobolea gunia 1 la mpunga then narudi nao kwangu. Sasa siku hiyo nikaota narudi bila kitu. Huwa naamka saa 9 au 10 kwa ajili ya maombi. Nikaamka nikasali ila sikuwa najua maana ya ndoto hiyo. Saa 12 alfajiri nikarudi kitandani ikaja kwa namna nyingine. Nikaamka na kuingia kusali ila kuna Wimbo ukawa unatembea kichwani mwangu "Kwa Mji wa Mwangaza" baadae wananipigia simu he is no longer. Msiba ule wimbo mkubwa uliokuwa kichwani mwangu ni huo. Nikilala, nikiamka mchana na usiku moyo na mawazo yangu yana wimbo huo. Binafsi nikawa namuomba na kumsihi Mungu nijue mzee kaendaje. Sikupata maono wala ndoto kuhusu yeye ila baada ya maiba kuisha nami kurudi kwangu ndipo nilipata ndoto moja na ya mwisho kuhusu yeye. Akaniambia" Ndetefyose kwanini unanililia? Mimi nimeshamaliza mwendo, ililie nafsi yako. Sina deni na mtu na fulani unayezani namchukia simchukii ila sikuwa nataka nimuachie mji wangu.

Hakika tutaonana baadae mzee, hakika tutakutana patakatifu pale katika ibada ile ya harusi ya mwanakondoo tukiimba hossana hossana huku tukizunguka kiti cha enzi.
 
Nakosa la kuandika!
Kuna watu wana mapito...tamar pole sana
 
Pole sana kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…