Je, dakika yake ya mwisho duniani alisemaje? Ilikuwaje?

Je, dakika yake ya mwisho duniani alisemaje? Ilikuwaje?

Uzi huu tusaidiane kutambua last moments za wapendwa wetu huwa zinakuwaje au watu tunaowafahamu. Hususan pale anapokata roho. Nitaelezea kiss kimoja nilichoshuhudia.

Nilikuwa namuuguza ndugu yangu hospitali moja ya mkoa enzi hizo tunalala na wagonjwa mahospitalini. Kitanda opposite na mimi alikuwako mzee mmoja anamuuguza kijana mmoja wa miaka kama 17 hivi au zaidi kidogo.

Yule mzee akamuona yule kijana anahangaika anatapatapa akajua huyu anakata roho. Alichofanya yule mzee akakaa nyuma ya mabega ya yule kijana hivyo kijana akawa amemlalia mzee mapajani. Yule mzee akaanza kummassage macho yule kijana kwa kuyafumba. Taratibu yule kijana akakata roho na kufariki. Sitaisahau siku hii ilikuwa mwaka 1993/4.
Eloi eloi sabalakitani
 
Let me share this one….ni kama mwezi umepita tokea my half brother amefariki..aliumwa sana kwa muda wa miaka miwili alikuwa akisumbuliwa na saratani ya utumbo mpana na mimi ndo nilikuwa namuuguza kwa muda wote aliokuwa anaumwa alikuwa anapitia maumivu makali sana nilikuwa naona.To cut off the story siku 3 kabla ya kifo chake nilipata safari ya kwenda mkoani wakati huo yeye alikuwa anaugulia nyumbani(alikuwa anafanya radition so ilikuwa ni hosp to home) siku nnayoondoka huku nyuma alizidiwa sana wakampeleka hosp nikawasiliana nao kwa simu wakasema alikuwa na hali mbaya sana hivyo niwahi kurudi. Na kweli nikarudi baada ya siku mbili na kwenda moja kwa moja hosp kumuona. Kama mungu siku hiyo mtu aliekuwa analala nae nikwambia aende nyumbani na kusisitiza kwamba kwa usiku huo ntalala mimi na mgonjwa na ni baada kuona amebadirika kabisa alikuwa sio yeye kabisa. Alikuwa haongei anafanya ishara tu na akiongea anaongea vitu ambavyo huvielewi kabisa ila kwa usiku ule alihangaika sana na kuongea mambo mengi ambayo sikuelewa but kufikia saa 9 alikata roho mbele yangu nikiwa nimekaa kwenye kiti namuangalia. And He was only 29.
Pole Sana mkuu
 
Wakati mgumu mno ni ule wakati uhai unatoka - usiombe kitu hicho kikukute. Ukitaka kujua namna utakavyohangaika jaribu kuziba pumzi yako wa dakika kama 3 hivi... au jaribu kujinyonga na kisha ukijitundika mwambie nduguyo awepo hapo ili kabla hujakata roho aikate kamba - then uje utushuhudie uchungu wake.

Kwa kweli kifo ni kitu kichungu mno, na kibaya zaidi ukishazaliwa tu lazima ushuhudie maumivu hayo na baada ya kukata roho hutajua upo wapi, kama ulizaliwa duniani ama laah.

Kifo ni fumbo.
Kifo ni process mtu anayekuwa kwenye hiyo process inafika kipindi hasikii kitu anakuwa hana concentration anapotea taratibu ni kama mtu anayepoteza fahamu hasikii maumivu sasa mwili au organs zinaanza kuacha kufanya kazi ile inakuondolea maumivu kuna wako wanakata kauli kama hayupo ndio maana utasikia utasema amelala tu. Kuna vifo vya ghafla kama heart attack au ajali anapoteza nguzu tu na kuanguka. Mungu atupe mwisho mwema tuseme amiin
 
Tukiwa kwenye harakati za kumuuguza mke wangu mpendwa,Mama alikuwa msaada mkubwa kwangu na kwa mke wangu,siku hiyo nimetoka hospitali kumuona mke wangu,nafika nyumbani nikaambiwa mama ananiita kwake,nikaenda na kumkuta ana huzuni sana,akaniuliza tu mgonjwa anaendeleaje?nikamwambia anaendelea vizuri sana,akaniambia "moyo wangu unaniuma sana nimeshindwa kwenda kumuona,miguu yangu haifanyi kazi kabisa,ila naamini tu Mungu ATANIKUTANISHA naye siku moja" niliondooka kwake saa tano usiku,tukaagana,akaenda kulala na mimi nikaenda kwangu,siyo mbali sana! Usiku wa kama saa nane nikapigiwa simu na mtu aliyekuwa hospitali alipokuwa amelazwa mke wangu!akaniambia hali ya mke wangu imekuwa mbaya ghafla,hivyo kama nitaweza niende asubuhi,hospitali yenyewe ilikuwa mkoa mwingine, nikakosa amani kabisa! Kufika saa kumi hivi usiku nikapigiwa simu tena! Roho ikapasuka paah!! Kuicheki ni mdogo wangu anayeishi na mama,nikapokea,akawa analia huku akiniambia "njoo nyumbani haraka" nikatoka mbio,nikafika na kumkuta mdogo wangu nje ana haha na kulia,nika muuliza kuna nini?akanikumbatia huku akilia na kuniambia niingie ndani,nikaingia mbio,nikaenda haraka chumbani kwa mama! Nikamkuta amelala huku anakoroma kwa sauti ya chini kabisa nikajaribu kkumwamsha kwa kumtikisa! Hakujibu,wala hakuamka,Akaondoka hivyo!! Tukaandaa mazishi na kumzika hapo hapo nyumbani huku mke wangu akiwa bado hospitali na akiwa na hali mbaya,siku tumezika mmke wangu ni kama alipata nafuu ghafla na kuongea na dokta aniambie nimpe mama simu aongee naye,nikamwambia mama ametoka kidoogo,akasisitiza sana,maana siku mama yangu anazikwa mimi nilienda hospitali asubuhi na mke wangu akawa anaongea kwa tabu akinilaumu kwa kumnyima kuongea na mama,akasema kuna kitu anataka amwambie mama ili mmama aniambie mimi,akasema "mimi nakufa,ila kuna jambo nataka nimwambie mama kwa ajili yako, basi tukamzika mama!! Mke wangu hakujua kuwa mama amefariki hadi siku moja alipoambiwa na mgonjwa mwingine aliyefika hospitalini akkitokea huku tunakoishi siku hiyo mke wangu alilia sana,akaniita,nikaenda,akalalamika kwa nini Mungu amemchukua Mama aliyekuwa mzima na mwenye aliyempenda sana na kumuacha yeye akiteseka kitandani kwa miaka!! Nimekuwa na wakati mgumu toka hapo ndugu zangu! Wiki mbili baada ya kumzika mama mke wangu mpenzi naye akafariki!! Lile neno alillotaka kumwambia mama aliniambia mimi mwishoni,nikamzika nyumbani pembeni ya mama aliyependa na waliopendana sana!! Mimi bado nipo kwenye msiba mzito!! Ni wiki tatu tu zimepita tangu nimzike mke wangu,mke wangu aliugua saratani ya ziwa(breast cancer) naandika huku machozi yananimwagika.
Duuh so sad mkuu Pole sana
 
Mzee alitaka kuongea namimi mambo mengi ,Mimi na ndugu tukawa tunamzuia mana alikuwa anapata maumivu sana wakati wakuongea.Ila nakumbuka maneno baadhi”NIWAJALI NDUGU ZANGU NA KUWAHESHIMU WATU”
RIP mzee!!!Corona ilimuondoa
Huu ugonjwa wa kishetani sana.
Rip Mzee.
 
Tukiwa kwenye harakati za kumuuguza mke wangu mpendwa,Mama alikuwa msaada mkubwa kwangu na kwa mke wangu,siku hiyo nimetoka hospitali kumuona mke wangu,nafika nyumbani nikaambiwa mama ananiita kwake,nikaenda na kumkuta ana huzuni sana,akaniuliza tu mgonjwa anaendeleaje?nikamwambia anaendelea vizuri sana,akaniambia "moyo wangu unaniuma sana nimeshindwa kwenda kumuona,miguu yangu haifanyi kazi kabisa,ila naamini tu Mungu ATANIKUTANISHA naye siku moja" niliondooka kwake saa tano usiku,tukaagana,akaenda kulala na mimi nikaenda kwangu,siyo mbali sana! Usiku wa kama saa nane nikapigiwa simu na mtu aliyekuwa hospitali alipokuwa amelazwa mke wangu!akaniambia hali ya mke wangu imekuwa mbaya ghafla,hivyo kama nitaweza niende asubuhi,hospitali yenyewe ilikuwa mkoa mwingine, nikakosa amani kabisa! Kufika saa kumi hivi usiku nikapigiwa simu tena! Roho ikapasuka paah!! Kuicheki ni mdogo wangu anayeishi na mama,nikapokea,akawa analia huku akiniambia "njoo nyumbani haraka" nikatoka mbio,nikafika na kumkuta mdogo wangu nje ana haha na kulia,nika muuliza kuna nini?akanikumbatia huku akilia na kuniambia niingie ndani,nikaingia mbio,nikaenda haraka chumbani kwa mama! Nikamkuta amelala huku anakoroma kwa sauti ya chini kabisa nikajaribu kkumwamsha kwa kumtikisa! Hakujibu,wala hakuamka,Akaondoka hivyo!! Tukaandaa mazishi na kumzika hapo hapo nyumbani huku mke wangu akiwa bado hospitali na akiwa na hali mbaya,siku tumezika mmke wangu ni kama alipata nafuu ghafla na kuongea na dokta aniambie nimpe mama simu aongee naye,nikamwambia mama ametoka kidoogo,akasisitiza sana,maana siku mama yangu anazikwa mimi nilienda hospitali asubuhi na mke wangu akawa anaongea kwa tabu akinilaumu kwa kumnyima kuongea na mama,akasema kuna kitu anataka amwambie mama ili mmama aniambie mimi,akasema "mimi nakufa,ila kuna jambo nataka nimwambie mama kwa ajili yako, basi tukamzika mama!! Mke wangu hakujua kuwa mama amefariki hadi siku moja alipoambiwa na mgonjwa mwingine aliyefika hospitalini akkitokea huku tunakoishi siku hiyo mke wangu alilia sana,akaniita,nikaenda,akalalamika kwa nini Mungu amemchukua Mama aliyekuwa mzima na mwenye aliyempenda sana na kumuacha yeye akiteseka kitandani kwa miaka!! Nimekuwa na wakati mgumu toka hapo ndugu zangu! Wiki mbili baada ya kumzika mama mke wangu mpenzi naye akafariki!! Lile neno alillotaka kumwambia mama aliniambia mimi mwishoni,nikamzika nyumbani pembeni ya mama aliyependa na waliopendana sana!! Mimi bado nipo kwenye msiba mzito!! Ni wiki tatu tu zimepita tangu nimzike mke wangu,mke wangu aliugua saratani ya ziwa(breast cancer) naandika huku machozi yananimwagika.
Pole sana ndugu,unaweza kutugusia neno alilokwambia?
 
Mimi ni Mtu wa Afya Nimeshuhudia Mara nyingi mtu akikata Roho mbele yangu.

1..Nikiwa wodi ya wanawake mwaka 2018 kuna Client aliugua Sana Kwa Muda mrefu na Kiutaaramu Tukiweza kujua Huyu ni ngumu kutoboa Labda Mungu Tu..siku nimeingia Night nakuta client ana Furaha Tofauti na Siku zote aisee kufika saa nane Usiku Tayari Nimeshapeleka mwochwali.

2.Huyu alikuwa mwanafunzi wa Kidato cha sita ameanguka kwenye Chumba cha mtihani wa Taifa kaja Kituo cha Afya chetu tukaanza Huduma za Kwanza Faster Sana ..Ila Hapa Napo kutoboa Tulihisi ngumu Kwa watu wa Afya wanaelewa hii Baada ya Kuhakikisha fluid kama sita za IV fluconazole nimezitembeza nikasema ngoja nikanywe chai kurudi client ananiambia naomba tuombe alikata Moto mbele yangu huyu Nilimfumba macho na mdomo mwenyewe Ila niliumia Sana Hasa dogo Amepotea ndoto zake mapema hawa mabinti wanaua Sana wadogo zetu japo kuanzia form five aligoma Kutumia dawa kijana wa watu na Sijui Nani alimpa.

Aisee matukio ni MENGI WATU wa Afya tunakutana na mengi na ndio maana Tunakuwa na Roho Fulani tunazijua Wenyewe
Ngoma nini
 
Dahhhh, ilikuwa jumamisi ya 13/11/2018 Mzee wangu alianguka tu ghafla baada ya kumaliza kusali Jumuia nyumbani kwake. Alimwambia Mama "Mke wangu, usisumbuke kunipeleka hospitali kwani nimeshakufa, nimeuona Yesu na kaniambia nimeshakufa. Kisha akasema, Mungu wangu unisamehe kwa yote niliyotenda nikiwa duniani" Akafunga Macho na mdomo ndio moja kwa moja.
Mzee wako yupo sehemu salama,na kafa vizuri Sana,huwa ninaomba siku yangu ikifika nife taratibu tena nikijua sehemu ninapoenda kufikia huku ninatabasam,nikaonane na Mungu wangu,baba yangu na wapendwa wangu wote
 
Amina brother. Mungu akutane na haja ya moyo wako
 
Watu mmeelewa ila wagumu kuelewa. Sio kwamba hujui,unajua huyo ni MUNGU MWANA. Hapo alikuwa anamaanisha mkuu,ambaye ni babaake pia.
Kumbe kuna Mungu mtoto na Mungu baba! hapo Imebaki kuongezewa Mungu mama.
Mungu ni mmoja hafaninishwi na yeyote.
 
I was not there lakini last few days nilienda kumuona, alikua na Hali Fulani ngumu, alipata second stroke, hakuweza kuongea LAKINI alinishika mkono wangu kwa nguvu sana Kisha nikatokwa na machozi, alikua ananihakikishia kuwa nisiwe na mashaka atapona! Man, that's still the worst scenerio ninayoikumbuka. Naandika hivi huku machozi yananitoka. She was among the best Mom ever.....then tarehe 13/04/2017 asubuhi as I was getting out kwenye meeting I received a call.....nililia kama Mtoto. Niliondoka Dar jioni ya siku Ile 13/04/2017 kama Jana then 15/04/2017 tukampunzisha. Sitaki kukumbuka hiki kitu kabisa.

Siku mbili hizi zimekua ngumu sana kwangu Kila mwaka nakumbuka hili tukio napata shida mnooooo.

Pole sana dahhhhh
 
Uko emotional sana pole, me wangu anatimiza miaka 10 mwaka huu mwezi julai.
 
wataalam wanasema kifo kizuri kuliko vyote ni kulipukiwa na bom la nyuklia ukiwa ndani ya mzunguko wa 100 m

kabla haujahisi chochote unakua umeshafutika duniani..

Note: sio kufa, bali kufutika kabisa
 
Back
Top Bottom