Unachokifanya hapa ni sawa na kupeleka injili kwenye kilabu cha pombe za kienyeji. Swali ni sahihi, lakini hadhira (Ummah) uliyoipa hili swali siyo sahihi........
Nimesoma majibu machache tu na kutambua kwamba watanzania wengi mno, ni watu wenye fikra zilizochini ya kiwango (Below Average) ilhali tunajikuta wajuaji kupita kiasi......
Tanzania imefika sehemu mbaya mno, kiasi kwamba wale watu wenye akili na wanaofahamu mambo huwezi kuwakuta wanaongea hadharani wala kuchangia chochote kile. Ila wale wasio na ufahamu wanaongea sana.....
Yote tisa Tanzania iko sehemu mbaya mno. Katika ngazi ya kitaifa na kikanda. Siku zijazo watanzania tutatia akili, we subiri........