Hapo ndio naposhindwa kuelewa sababu ya kutaka kuuliwa huyo Lissu, kama mnasema Magufuli alitaka kumuuwa Lissu kwa sababu ya kumkosoa tu sasa Magufuli hayupo na hao watu waliyobaki hawajashika madaraka kama mwanzo, sasa hapo hao watu watake kumuuwa Lissu ili iweje na hata wakifanya hivyo wana uhakika gani wa kutofuatiliwa na kukamatwa?Bado traces za Umagufuli (kuua, kuteka, kubambikia kesi, kupoteza watu and the like ) bado vipo. Huwezi kujiaminisha kurudi now! Samia haaminiki kama mnavyotaka mtu aliyepigwa risasi 40 aamini!
Kwani alitakiwa kufanya nini kinyume na hayo?Wewe sijui ni kipofu?
Yote aliyofanya mama huyaoni?
Karudisha uhuru wa vyombo vya habari.
Miradi yote ya kimkati inaendelea kujengwa Kwa Kasi kubwa
Elimu Bure mpka F6.
Ajira mpya.
Kupandisha madaraja watumishi
Makusanyo ya TRA kupaa bila uporaji wa kutumia task force
Ujenzi wamadarasa katika shule za msingi na sekondari na shule mpya bila kuchangisha wananchi.
Ujenzi wa zahanati,vituo vya afya na hospitali pamoja na ununuzi was vifaa tiba.
Kuongezeka kwa Bei ya mazao yote ya wakulika na masoko ya uhakika.
Orodha ni ndefu mno! Nimechoka kuandika.....
Mtu kama Retired unategemea akili atoe wapi?Unachokifanya hapa ni sawa na kupeleka injili kwenye kilabu cha pombe za kienyeji. Swali ni sahihi, lakini hadhira (Ummah) uliyoipa hili swali siyo sahihi........
Nimesoma majibu machache tu na kutambua kwamba watanzania wengi mno, ni watu wenye fikra zilizochini ya kiwango (Below Average) ilhali tunajikuta wajuaji kupita kiasi......
Tanzania imefika sehemu mbaya mno, kiasi kwamba wale watu wenye akili na wanaofahamu mambo huwezi kuwakuta wanaongea hadharani wala kuchangia chochote kile. Ila wale wasio na ufahamu wanaongea sana.....
Yote tisa Tanzania iko sehemu mbaya mno. Katika ngazi ya kitaifa na kikanda. Siku zijazo watanzania tutatia akili, we subiri........