Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?


Kipepeo karibu tena JF, "ulipotea" sana mkuu
 
Unajua labda wakati anasoma hakukuwa na Microsoft Office applications kwa hiyo mambo ya single na double spacing yatakuwa magumu kidogo....



Mbona unamjibia mwache Slaa aje mwenyewe kujibu hapa JF. Usimtie maneno yako mdomoni Dk Slaa. jibuni hoja ni kwa nini Chadema wanaweka wagombea wabovubovu na kisha wategemee huruma ya wapiga kura ili kutoka na ushindi kama vile akina Regina Mtema?
 


Kikwete aliposema watoto wa shule waache kihelehele kwa maana kwamba hata kama wanaume wanawatongoza lakini na wao tamaa zinawaponza hivyo bila na wao kuwa mathubutu serikali pekee haiwezi kuondoa kwa urahisi tatizo hilo. kabla ya kauli hiyo Rais alikuwa amechukua hatua kadhaa za kukabiliana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kuwatia ndani wanaume wote wanawapa wanafunzi mimba ikiwemo waalimu na wazazi wanawaoza wanafunzi. Kauli ya kihelehele ilishikiwa bango hapa JF bila kuzingatia kwamba Rais alikuwa anawakanya wanafunzi kwani na wao sehemu ya tatizo hilo.

sasa imekuwa ni zamu ya Dk. Slaa baadhi yetu tunajitokeza na kusema kwamba mambo ya lugha ni madogo katika safari yake ya kuelekea Ikulu. Mbona kwa kikwete hatukufanya hivyo?
 

Kikwete hakusema kihelehele ... alisema kiherehere (kama watu wa musoma).

Wewe ushaanza kuchapia lugha wakati ukijaribu kukosoa watu waliochapia lugha. Mijitu mingine kwa kupenda ligi bana?!
 
Kikwete hakusema kihelehele ... alisema kiherehere (kama watu wa musoma).

Wewe ushaanza kuchapia lugha wakati ukijaribu kukosoa watu waliochapia lugha. Mijitu mingine kwa kupenda ligi bana?!

Mbona Dr. Slaa kashaanza kuvunja ahadi yake ya kujibu maswali hapa? Akipewa urais ataheshimu ahadi zake anazotoa ili kupata urais ?

Aliandika

Nawashukuru wana jamvi wote, na wanajamvi mko huru kudodosa lolote kwa vile kiongozi hana private life, hivyo Dr Slaa anaweza kuulizwa lolote na ufafanuzi unaotakiwa utatolewa

Is Dr. Slaa a man of his word ?
 
Mbona Dr. Slaa kashaanza kuvunja ahadi yake ya kujibu maswali hapa? Akipewa urais ataheshimu ahadi zake anazotoa ili kupata urais ?

Is Dr. Slaa a man of his word ?

Sikukumbuki alikosema kuwa kampeni zikianza ataendelea kukesha hapa masaa 24 akijibu kila swali linaloulizwa na wanachama wa JF. Iwapo alifanya hivyo, basi inabidi arudi hapa ili aendeleze ligi na kina Kiranga (na wapenda ligi wenzake - Taso, Gaijin, kipepeo, tindikali etc).

Wewe unasemaje mkuu?
 


TUMEELEWANA MKUU....
Hivi Kikwete hana Dini? mbona yeye hasemwi kwamba ni Mwislamu?
Huyo anayeandika ameishiwa point.....kwa taarifa tu hata Dk Salim Ahmed Salimu yuko nyuma ya Slaa.....pole wanaoeneza udini, SAS ni Mwislamu saafi, lakini anamkubali Slaa.....
 

Kujibu maswali mawili matatu ya JF huhitaji kushinda na kukesha JF, Dr. Slaa tulitarajia aje kujibu maswala, au kama ana udhuru, aje kujiudhuru hapa.

Lakini hajajibu maswali wala kuja kujiudhuru, hata baada ya kuahidi kujibu.

Hili linanionyesha kwamba Dr. Slaa si mtu wa kuthamini ahadi zake. Anaweza kubadili msimamo wangu huu kwa kuja hapa na kujibu hoja, lakini mpaka hapo atakuwa ametudanganya wana JF.

Kimsingi atakuwa sawa na Kikwete aliyekataa mdahalo.
 
Kujibu maswali mawili matatu ya JF huhitaji kushinda na kukesha JF, Dr. Slaa tulitarajia aje kujibu maswala, au kama ana udhuru, aje kujiudhuru hapa.

Lakini hajajibu maswali wala kuja kujiudhuru, hata baada ya kuahidi kujibu.

Atakakuja tu kama kawaida yake. Dr Slaa ni mgombea pekee wa uraisi Tanzania ambaye anakuja JF. Sidhani kama akipotea siku mbili tatu kuna mtu mwenye akili timamu ataanzisha ligi ya kwa nini Dr Slaa hayuko hapa.

Unless that person anajiona kuwa yeye ni bora kuliko watanzania wooote wanaotaka kumsikiliza Dr Slaa.

Hili linanionyesha kwamba Dr. Slaa si mtu wa kuthamini ahadi zake. Anaweza kubadili msimamo wangu huu kwa kuja hapa na kujibu hoja, lakini mpaka hapo atakuwa ametudanganya wana JF.

Ha ha ha,

Kiranga bana. Kwa chuki zako dhidi ya Dr Slaa, nina hakika kuwa akitembea juu ya maji utaanza ligi kuwa kwa nini hakutembea kinyumenyume.
 

Dk Salim Ahmeid Salim ni muislam safi? kwa ushahidi gani?
 

Mazee hebu tueleze Salim Ahmed Salim kamkubali Slaa wapi?

Au kama ni vitu visivyothibitishika utuambie kabisa kwamba hiki ni kitu kisichothibitishika, kama vile ukituambia nimemuona Julius Kambarage Nyerere viwanja vya jangwani dakika tano zilizopita.
 

Another angle ya kuendeleza ligi (na hii thread). Kazi yenu inatia moyo kweli.
 

Hongera sana Dr. Slaa kwa kujitokeza na kujibu hoja iliyowekwa hapa.

Ni vyema ukajitahidi kujibu hoja hizi bila kucho kadiri unavyoweza kupata nafasi. Naelewa si rahisi sana kufanya hivyo hasa katika kipindi hiki cha kampeni. Ila ni vyema kujibu kila kinachosemwa, hata kama kimewahi kujibiwa mara nyingi siku za nyuma.
 

Kwa kuwataja wachache, Mary Nagu alikuwa kambi ya Fredrick Sumaye na Mark Mwandosya alikuwa mgombea wa Urais pamoja na Kikwete. Je ulitaka wote ambao walikuwa kambi tofauti na kikwete mwaka 2005 waunde serikali ya Kikwete? au ulitaka wangapi ndipo ulidhike?
 

Mkuu, kukubali/kuruhusu wewe kukosea eti kwa sababu hugombei nafasi ya Urais ni kujaribu kupotosha watu bila sababu. Utu wako na wa Dr. Slaa hautofautishwi na nafasi uliyochagua kuitumikia kwenye jamii. Ubora wa maandishi yako unatakiwa kuwa sahihi wakati wote.

Ila ni vyema pia ukajua kuwa wengi wanaoandika hapa hujaribu kutumia muda mfupi iwezekanavyo ili kufikisha mawazo/ujumbe wanaokusudia. Hivyo mara nyingi usahihi wa uwakilishi wa maneno hauzingatiwi sana. Kumbana Dr. Slaa kwa mapungufu ya presentation ya mawazo yake katika forum ni kuwa very low.

Kinachotakiwa ni kuelewa nini kinachowasilishwa. Maandishi yetu hapa hayana reflection yoyote na jinsi tunavyo andika nyaraka za kikazi.

Kwa maoni na imani yangu, Dr. Slaa ni mgombea bora zaidi ya wote waliojitokeza kwa nafasi ya urais. Hiyo haimaanishi kuwa yeye kama mtu binafsi hana mapungufu. Vile vile, mengi kati ya mandiko yake yatafanyiwa kazi na wasaidizi endapo atapata baraka za WaTanzania kuwa Rais. Sitegemei yeye kuwa mwandishi na mhakiki wa maandiko yake yote ya kikazi atakapokuwa Rais. Labda kama unataka kutuambia hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa serikali ijayo.
 
Another angle ya kuendeleza ligi (na hii thread). Kazi yenu inatia moyo kweli.

Kama unaita kuulizana kuendeleza ligi, then point nzima ya JF ni kuendeleza ligi. Kama huna nia ya kuendeleza ligi huhitaji kuwa JF.
 
Kama unaita kuulizana kuendeleza ligi, then point nzima ya JF ni kuendeleza ligi. Kama huna nia ya kuendeleza ligi huhitaji kuwa JF.

Sikusema kama napingana na ligi (trust me... napenda sana ligi za JF). Tatizo ni kuwa, sidhani kama Dr Slaa ana muda wa kuendesha ligi na yeyote hapa JF kwa muda huu. Ligi zinahitaji uwepo JF masaa 24, otherwise kina Kiranga na wenzake watakuita muongo.
 



Sijasema kwamba ubora wa maandishi yangu unatakiwa kuwa sahihi wakati wote, hili nalikubali. Hapa naongelea kitu tofauti.

Naongelea standards na applications zake. Naongelea "Noblesse Oblige". Naongelea "To whom much is given, much is required". Hizi ni basic principles. Huwezi kumpa mtoto wa darasa la pili mtihani wa Chuo Kikuu kuandika research paper, utaonekana unachekesha.

Mimi kwa kazi ninayofanya na dhamana yake kwa maisha ya kila siku kwa wananchi wa Tanzania ni kama mtoto wa darasa la pili. Dr. Slaa kazi anayofanya na hususan anayoiomba ya urais, dhamana yake kwa maendeleo ya taifa ni kama mtihani wa Chuo Kikuu kuandika research paper. Kutupa mimi mtoto wa darasa la pili na Dr. Slaa mtu anayeandika research paper ya chuo kikuu standards zile zile na mtihani ule ule itakuwa ni utovu wa maarifa.

Mimi si Dr, Slaa ni Dr. Mimi siko katika uongozi wa kisiasa wa Tanzania ngazi ya taifa, Slaa yumo, mimi sijaomba dhamana ya kupigiwa kura na wananchi hata ujumbe wa nyumba kumi, Slaa kashaomba na sasa anaomba kura za mamilioni ya Watanzania nchini kote.

Utawezaje kutuweka katika fungu moja?
Hata hao watoza kodi waliosemwa hata kwenye misahafu kwa uroho wao wa fedha huwa na viwango tofauti kwa watu wenye vipato tofauti. Tuweke principles zinazofuata equitability.

Acha hizo.


Wenye kujua mantiki walisema "Anything worth doing is worth doing well, if something is not worth doing well, it is not worth doing at all" kama Dr. Slaa aliona usahihi wa maandishi yake uko matatani angesubiri mpaka hapo ambapo angepata muda wa kuweka kitu kilichotulia, sasa hivi katuonyesha kwamba Dr. Slaa ana mapepe, anakurupuka kujibu vitu haraka bila kutulia na hana umakini.


Kinachotakiwa ni kuelewa nini kinachowasilishwa. Maandishi yetu hapa yana reflection yoyote na jinsi tunavyo andika barua an report za kikazi.

Utaelewa vipi kitu chenye makosa? Chenye makosa hakihakikishi kwamba wasomaji wataelewa, on the contrary kinaongeza uwezekano wa kutoeleweka. Ndiyo maana nasisitiza vitu viandikwe kwa kufuata kanuni zinazojulikana za uandishi ili tunaposoma tusianze kuwa na maswali ya kwamba "hapa Dr. Slaa alipoandika "the onus of proove" alimaanisha nini?" tuwe tunapima hoja alizoleta, sio kuanza kufikiri fikiri kuhusu usahihi wa lugha aliyotumia.


Maoni na imani yako unayo wewe, fact ni kitu kingine. Hata kama yeye si mhakiki wa maandishi, ningetegemea mtu mwenye Ph. D na mwenye hadhi ya urais ajue mambo madogo kama vile ukianza sentensi unaanza na herufi kubwa, huwezi kuchanganya first na third person unapojiongelea mwenyewe, huwezi kuandika bila paragraph etc.

Na huwezi kunihakikishia kwamba matatizo haya yatafanyiwa kazi na Slaa wakati Slaa mwenyewe hata hajayakubali kama ni matatizo, na kuna wafuasi wake lukuki hapa wanataka tusiyaongelee kwa sababu wanadai si ya msingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…