Mkuu, kukubali/kuruhusu wewe kukosea eti kwa sababu hugombei nafasi ya Urais ni kujaribu kupotosha watu bila sababu. Utu wako na wa Dr. Slaa hautofautishwi na nafasi uliyochagua kuitumikia kwenye jamii. Ubora wa maandishi yako unatakiwa kuwa sahihi wakati wote.
Sijasema kwamba ubora wa maandishi yangu unatakiwa kuwa sahihi wakati wote, hili nalikubali. Hapa naongelea kitu tofauti.
Naongelea standards na applications zake. Naongelea "Noblesse Oblige". Naongelea "To whom much is given, much is required". Hizi ni basic principles. Huwezi kumpa mtoto wa darasa la pili mtihani wa Chuo Kikuu kuandika research paper, utaonekana unachekesha.
Mimi kwa kazi ninayofanya na dhamana yake kwa maisha ya kila siku kwa wananchi wa Tanzania ni kama mtoto wa darasa la pili. Dr. Slaa kazi anayofanya na hususan anayoiomba ya urais, dhamana yake kwa maendeleo ya taifa ni kama mtihani wa Chuo Kikuu kuandika research paper. Kutupa mimi mtoto wa darasa la pili na Dr. Slaa mtu anayeandika research paper ya chuo kikuu standards zile zile na mtihani ule ule itakuwa ni utovu wa maarifa.
Mimi si Dr, Slaa ni Dr. Mimi siko katika uongozi wa kisiasa wa Tanzania ngazi ya taifa, Slaa yumo, mimi sijaomba dhamana ya kupigiwa kura na wananchi hata ujumbe wa nyumba kumi, Slaa kashaomba na sasa anaomba kura za mamilioni ya Watanzania nchini kote.
Utawezaje kutuweka katika fungu moja?
Hata hao watoza kodi waliosemwa hata kwenye misahafu kwa uroho wao wa fedha huwa na viwango tofauti kwa watu wenye vipato tofauti. Tuweke principles zinazofuata equitability.
Acha hizo.
Ila ni vyema pia ukajua kuwa wengi wanaoandika hapa hujaribu kutumia muda mfupi iwezekanavyo ili kufikisha mawazo/ujumbe wanaokusudia. Hivyo mara nyingi usahihi wa uwakilishi wa maneno hauzingatiwi sana. Kumbana Dr. Slaa kwa mapungufu ya presentation ya mawazo yake katika forum ni kuwa very low.
Wenye kujua mantiki walisema "Anything worth doing is worth doing well, if something is not worth doing well, it is not worth doing at all" kama Dr. Slaa aliona usahihi wa maandishi yake uko matatani angesubiri mpaka hapo ambapo angepata muda wa kuweka kitu kilichotulia, sasa hivi katuonyesha kwamba Dr. Slaa ana mapepe, anakurupuka kujibu vitu haraka bila kutulia na hana umakini.
Kinachotakiwa ni kuelewa nini kinachowasilishwa. Maandishi yetu hapa yana reflection yoyote na jinsi tunavyo andika barua an report za kikazi.
Utaelewa vipi kitu chenye makosa? Chenye makosa hakihakikishi kwamba wasomaji wataelewa, on the contrary kinaongeza uwezekano wa kutoeleweka. Ndiyo maana nasisitiza vitu viandikwe kwa kufuata kanuni zinazojulikana za uandishi ili tunaposoma tusianze kuwa na maswali ya kwamba "hapa Dr. Slaa alipoandika "the onus of proove" alimaanisha nini?" tuwe tunapima hoja alizoleta, sio kuanza kufikiri fikiri kuhusu usahihi wa lugha aliyotumia.
Kwa maoni na imani yangu, Dr. Slaa ni mgombea bora zaidi ya wote waliojitokeza hadi sasa kwa nafasi ya urais. Hiyo haimaanishi kuwa yeye kama mtu binafsi hana mapungufu. Vile vile, mengi kati ya mandiko yake yatafanyiwa kazi na wasaidizi endapo atapata baraka za WaTanzania kuwa Rais. Sitegemei yeye kuwa mwandishi na mhakiki wa maandiko yake yote ya kikazi atakapokuwa Rais. Labda kama unataka kutuambia hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa serikali ijayo.
Maoni na imani yako unayo wewe, fact ni kitu kingine. Hata kama yeye si mhakiki wa maandishi, ningetegemea mtu mwenye Ph. D na mwenye hadhi ya urais ajue mambo madogo kama vile ukianza sentensi unaanza na herufi kubwa, huwezi kuchanganya first na third person unapojiongelea mwenyewe, huwezi kuandika bila paragraph etc.
Na huwezi kunihakikishia kwamba matatizo haya yatafanyiwa kazi na Slaa wakati Slaa mwenyewe hata hajayakubali kama ni matatizo, na kuna wafuasi wake lukuki hapa wanataka tusiyaongelee kwa sababu wanadai si ya msingi.