Elections 2010 Je, Dr. Willibrod Slaa atatufaa?

Kama lengo lenu lilikuwa kupima uwezo wake katika matumizi ya lugha na mpangilio wa maneo basi Dr. Slaa amefeli, ila kama ulitaka ajibu hoja iliyotolewa jaribu kuwa mvumilivu na upate maana ya anachokisema. Hivyo, mnapotezea muda wa kuandaa mengine ya muhimu.

Na hao wagombea wengine mbona nao hamwapimi kama wanajiweza au vipi?
 
Dr. Slaa mwenyewe kakaribisha maswali yote tu, ingawa naona anagwaya kujibu.

Sidhani kama amegwaya kuyajibu. Inawezekana hata hayupo kwenye mtandao sasa hivi. Kwa hiyo vuta subira kidogo kabla hujaanza kuhukumu.
 

Now why should he worry you? Vuta subira kidogo, usiwe na papara! Tulia! tulia! tulia!
 
HAPANA.

Kuandika 'vizuri' hakuna mafungamano na fikra au umakini. Kuna maprofesa wanachemka hata wanapoandikia kwenye fields zao itakuwa huyu mwanasiasa Slaa?

Uprofesa si kipimo cha umakini. Ukiandika vizuri kwa kufuata kanuni za uandishi unanionyesha unaweza kufuata taratibu, ukiandika bila paragraph wala capitalization, unachanganya first person na third person kujielezea mwenyewe, unanionyesha kwamba mawazo yako hayako organized.

Na hii sio article ya specialization kwenye gazeti au kitabu, ni post tu ya kwenye forum tu..Sisemi kwamba aandike hovyohovyo kwa kusudi la, ila lazima tuangalie bigger picture hapa, ambayo ni kuangalia hoja iliyopo mezani.

Huwzi kusema nachafua pixels zote halafu ukategemea kuona bigger picture. Halafu hata kwenye bigger picture mbona tume question strategy ya CHADEMA na udhaifu wa ugombezi wake bila kupewa jibu ?

Walau tumshukuru Slaa kwa kuja humu kuonesha anachangamana na wanamijadala na walau anajua kutumia kompyuta na internet. Wengine huko hata kuumba hati ni 'wito'.

Mbona hili nimeshalisema? Siyo kwamba najisifia, kwenye credit natoa na wala sina upande, nimemsema vizuri Dr. Slaa kwamba angalau yeye tunamuona.

And just for the records, I did endorse Dr. Slaa hapa, even though I said he will not win. I still want to see the gap gradually narrowed and the opposition grow, increasing parliamentary seats and presidential votes percentage until we have a realistic chance of regime change.

Although how much change even that farfetched fate will institute is still debatable.
 
Kwa mwanazuoni kuandika kwenye junol sio umakini ila kwa mwanasiasa
kuandika kwenye forum ni kipimo cha umakini. THIS IS NONSENSE.

Huwzi kusema nachafua pixels zote halafu ukategemea kuona bigger picture. Halafu hata kwenye bigger picture mbona tume question strategy ya CHADEMA na udhaifu wa ugombezi wake bila kupewa jibu ?
Kama angekuwa amechafua pixels zote ungeambulia chochote?
BTW, wewe mwenyewe mbona unachapia na kuchemka hapo? au utajitetea wewe hugiombei 'urahisi'?
 
Kwa mwanazuoni kuandika kwenye junol sio umakini ila kwa mwanasiasa
kuandika kwenye forum ni kipimo cha umakini. THIS IS NONSENSE.

Sijasema hivyo, unachanganya madawa labda.

Kama angekuwa amechafua pixels zote ungeambulia chochote?
BTW, wewe mwenyewe mbona unachapia na kuchemka hapo? au utajitetea wewe hugiombei 'urahisi'?

Sikusema kwamba amechafua pixels zote. Nime employ an extreme example to drive a point home.

Tofautisha typo, ambayo nilishasema mwanzo kwamba hata mimi niko prone nayo (soma posts) na mtu kuchapia kitu kama "onus of proove".

Halafu hata kama ningechapia kama yeye, which I didn't, mimi sijachukua mzigo wa kutaka kuendesha nchi, kwa hiyo naweza kukuambia mimi mzugaji tu hapa wala usitake kuniwekea standards kama za Dr. anayetaka kurun nchi, it won't be fair.
 
Hoja ya antibayotiki ingekuwa valid kama asingezingatia kutoa maelezo zaidi kwenye sababu/point namba 1, 7, 8.

Nawaogopa sana wale wanaowaweka ant Slaa kuwa ni wasaliti. Binafsi I am not either Pro Slaa nor Pro Kikwete. Hawawote hawawezi. Nitacast my vote atakaposimama mgombea binafsi. Vyama vyote vya siasa, and especially vya upinzani ni hopeless.
 
Hii makala inaonekana kuandikwa na kada wa CCM. Mambo ya udini na ukampuni wa familia ya Mtei wa CHADEMA ni propaganda ambazo CCM wangependa zipandikizwe kwenye fikra za wapiga kura. No wonder mwandishi hakuthubutu hata kuweka jina lake.

Nasema na nitarudia kusema: Wadanganyika hatupendi kuambiwa ukweli, na ndiyo maana tumefikia hapa tulipo. Tukianza kuukataa ukweli na kuanza kumshambulia Jenerali Ulimwengu, basi hatutendi haki. NANUKUU; "......Mtu asiyeweza kuisimia nyumba yake atawezaje kulisimamia Kanisa la Mungu........" Kwani matatizo yote haya tunayoyaona chanzo chake ni nini? Jibu ni kwamba viongozi wanashindwa kuwakemea maswahiba wao. Dr. Slaa kashindwa kabisa kukemea uozo ndani ya CHADEMA. Tukimpa nchi mambo ni yale yale yale ya kufumbia macho maovu ya ndani ya CHADEMA na viongozi wake. Mahali panapomfaa Dr. Slaa ni bungeni na siyo ikulu. Lazima tuwe waelewa na kumpima mtu. ALIKUWEPO MREMA NA MABOMU YAKE!!! Sasa yuko wapi !!!!! Hizi kelele zote za kulipua mabomu lengo ni kupata umaarufu wa kukimbilia IKULU. [PERIOD]. Nasema na narudia kusema, Slaa mahali pake ni bungeni. MOSACHA SACHA NGAMBIRE AMAHENE, BASACHI...
 
Groupthink ni pamoja na kukubali kufikiri kwamba kuna watu wako above criticism, kwa mkumbo wa JF. Habari za kuchamba - ashakum si matusi- nilishakujibu hapo juu, huja address counter yangu.
Nimekuelewa... but once again, you are not overcritical to anyone, i just find it amusing that you are looking to satisfying yourself through ideal scenarios while we live in a real world



1. Nimeongea zaidi ya maswala ya lugha, na nilishakuambia hili katika post ya juu, nikakushauri usome hiyo post uone nilichoongea zaidi ya lugha, sasa naona hujasoma, na huna kipya unarudia rudia. Rudi kusoma post.

Nimeshasoma


once again, excellence ya mtu haitegemei lugha pekee na vilevile sijui kama tuna aliye 100% hapa duniani... i hope Taso will educate me on this one




again, i dont need to go to the extreme ends... waweza pia kuchamba kiasi tu yatosha... na pia nazi waweza tu kuchagua kiasi



I am cut from a different cloth, what? You don't like it ?

ah Kiranga... you know that you have my vote of confidence, but that doesn't mean we have to agree on everything, nothign but love bro

Kirangaaaaaaaaa.... aka......

haya bana
 
Sijasema hivyo, unachanganya madawa labda.
Awali nimesema kuna wanazuoni kwene fani zao wanakosea na kutupiwa usoni kazi seuze mwanasiasa Dr. Slaa anayeandika JF? Wewe ukajibu ati uanazuoni sio kipimo cha umakini..sasa nikitumia huo mzani kujenga hoja unasema hujasema!
Wacha nafasi kwa nuetrals waone nani anachanganya madawa hapa.
Sikusema kwamba amechafua pixels zote. Nime employ an extreme example to drive a point home.Tofautisha typo, ambayo nilishasema mwanzo kwamba hata mimi niko prone nayo (soma posts) na mtu kuchapia kitu kama "onus of proove".
Nimesema sijasema..back and forth zaanza..
Huwzi kusema nachafua pixels zote halafu ukategemea kuona bigger picture.
Halafu hata kama ningechapia kama yeye, which I didn't, mimi sijachukua mzigo wa kutaka kuendesha nchi, kwa hiyo naweza kukuambia mimi mzugaji tu hapa wala usitake kuniwekea standards kama za Dr. anayetaka kurun nchi, it won't be fair.
Readability ndio criterion kuu ya JF. Na hatuezi kusema ati mtu anayechapia JF ati hafai urais, huo utakuwa ujuha. Kama unatafuta secretary tafuta secretary..thats it.

Halafu unasema hujachemsha na 'HUWZI' ndio lugha gani..Halafu mbona unatumia plural kujirefer wewe mwenyewe..mko wangapi?
 
Sina wasiwasi kusema wewe hujakatishwa tamaa, ila hujui unatoka wapi na unaelekea wapi.

Kwa kifupi hujitambui. Sijui tuanzishe mashindano ya mimi si kisura sijitambui ili na wewe ugombee na ushinde? Kwanza ni mwongo, halafu hujui kudadavua mada, mbona huelezei, mfano eti hakubaliki, hauziki,
Kama ni kumkubali ni wale wanaojua mwelekeo wa nchi na siyo watu wa aina hii. Kuuzika ndugu yangu ni kwamba kuna watu wanauzika kinoma lakini mambo yao ndo hivi kuongeza matumizi ya serikali, kuwahusudu wageni na bidhaa zao hadi mfumko unaongezeka kihivi>

Mzee wanauzika lakini chamoto wengi wanakiona.
Unasema anaishi kuhuni, hayo ndo maamuzi ya mtu wa kada ile. huwezi kuishi na mke anayekwenda kinyume na wewe na ambaye atahatarisha maisha yako na ya taifa zima. hiyo haipo.
Kuhusu uchumi huyo aliyepo anajua uchumi wako tu yawezekana kama una bibi yako yawezekana umemsahau kama yupo mbali nenda kamwone anaumia sana. Uliza wazee wa zamani watakwambia wametoak wapi na sasa mambo yapoje. Utawaonea huruma na kura yako utampigia slaa. THE PRESIDENT FOR NATIONAL CHANGE
 
Kwangu mimi nadhani Dr. Slaa anafaa kuwa rais kwa sababu urais ni taasisi.

Ni mtu ambaye anathubutu ya kusema na kusimamia jambo hata kama wengi mwanzoni hawalijui au kuliafiki kama lina maslahi kwa taifa. We need people who dare to talk against evils and Dr. Slaa he has that capability.

This country will not be led by angels but human and human has their own shortcomings and I dare to say there is none who is 100% saint in this world. All have made mistakes and sinned but many have also repented once they knew their mistakes or have sinned. We need a new direction, we need a new regime, we need new minds, we need new executions, we need new political willingness, we need changes.

Nyerere came to know this after 23 years of being in power that people need changes regardless that they loved him or they may not loved him but are afraid of him b/se of informative systems he put in place....etc.

You cannot know how much you have lost if you are still following the old routes and mentality, you can only see and know it if you have a change.

There are times we must accept changes!!!!!!!
 
Join date.......august 2010 no wonder akaongea hayo,bila shaka after election utakimbia tuu
Hana mbinu wala mikakati ya kushinda
2. Anaonekana ana kaugonjwa ka ulevi na anataka kuwaambukiza watanzania wote ugonjwa huo-BE SPECIFIC
3. Hajui uchumi unakwendaje (labla kwa vile ni mtheolojia)-KUWA RAISI SI LAZIMA KUWA MCHUMI,MKAPA ALIKUWA MCHUMI NA ALIKUWA BETTER KULIKO HUYU MTAALAMU WA POLITICAL ECONOMY JK
4. Hauziki-WHAT IS YOUR BASIS
5. Hana ndoa-ANY PROOF?
6. Jema pekee alilofanya (ingawa hajafanikiwa na hatafanikiwa) ni kuwataja wevi pale mwembe yanga
7. Mnafiki. Analialia eti posho za wabunge ni kuwa huku anazipokea-KUMBUKA THAT WAS SUBJECT TO BEING PASSED BY THE BUNGE AMBALO MAJORITY NI CCM
8. Hodari wa kulalamika lalamika-NILIDHANI UNASEMA KUONGEA UKWELI
9. Anataka kuzalisha jamii yta wavuta sigara (huende na bangi pia) pamoja na walevi-THAT IS SO PERSONAL
10. Hakubaliki-WHAT IS UA BASIS
 

Narudia, kipimo cha umakini ni umakini, hakiwezi kuwa mwanazuoni.Unapojaribu kutenganisha mwanazuoni na mwanasiasa nakushangaa, kwa sababu kuna watu ni wanazuoni wanasiasa. Woodrow Wilson alikuwa Profesa Princeton halafu akawa rais wa US, sasa huyu utamuita mwanazuoni au mwanasiasa ?

Nimesema sijasema..back and forth zaanza..

Nimesema sijasema kwamba nimesema sijasema, don't misquote me.

Readability ndio criterion kuu ya JF.

The doctor was hardly readable na kuna watu hata hawajasoma kwa kuona hakuna mtu anayeweza kuandika kwa format mbaya vile akawa na mchango wa maana. At least hawakupata kutaka kutapika kwa kukutana na "onus of proove" na mambo ya sentensi kuanza bila capitalization. Readability gani unayoongelea wewe hiyo ambayo haijali paragraphs wala consistency ?

Na hatuezi kusema ati mtu anayechapia JF ati hafai urais, huo utakuwa ujuha. Kama unatafuta secretary tafuta secretary..thats it.

Wengine tutaona sio tu huwezi urais, tutaona hata shule hujaenda . Swala hapa si kuandika tu, kuna swala zima la presentation. Slaa kachemka kujipresent, huwezi kubisha. Na hizi kazi za circus show presentation ni muhimu kweli, you should know. Some would even go as far as saying the whole circus is nothing but presentation, sasa kama Slaa anashindwa presentation hapa JF utamtegemea aweze viwanja vikubwa ?

Halafu unasema hujachemsha na 'HUWZI' ndio lugha gani..Halafu mbona unatumia plural kujirefer wewe mwenyewe..mko wangapi?

Nishakwambia hiyo ni typo, nishakwambia mimi niko prone kufanya makosa, nishakwambia standard ya kumwekea kafuku kama mie nisietaka hata ofisi ya katibu kata ni tofauti na ya Dr. Slaa.

Lakini sikukosea kusema "onus of proove". Na hiyo ya kujirefer kwa wingi nakuonyesha kwamba mimi niko kama army, nakuonyesha umuhimu wangu.

Hata ukisoma Quran ilivyoanza kuandikwa mungu ana ji refer in the plural. I represent that level of importance.

But I guess it is like Japanese Haiku to you.
 
HIGHER EDUCATION:
1979-1981 Pontifical Urba University,Rome,JCD(summa cum laude)
1980-1980 ADV.Diploma-Socio-Political Studies,Koln,Germany(KAF)
1981-1981 St.Thomas Aquinas University,Rome,AD.Diploma Rural Development
1985-1985 London COR.College, Principles and Practice of Management Certificate.
Hii naona itakusaidia kujua kuwa sio mtaalamu wa Theology peke yake
 

Dr. kasepa !
 
Dr. kasepa !
Don't flatter urself..yaani ulitaka Slaa aache mambo yake nyeti ajibu hoja zako kuhusu 'ufanisi wa viingereza na punctuation' ambavyo wewe mwenyewe umeshindwa kudemonstrate? Hata ningekuwa mimi ningekupuuza tu ningekuona unanipotezea muda tu.

BTW, sio lazima ajibu, maana yeye ni individual tu na hawezi kujibu maswali yote ya CHADEMA as chama..ndio maana kuna PR departments kwene organisations.
 
Kwa hiyo tumnyime Kikwete kura kwa kuwa ni Ustaadhi? Tukifanya kupiga kura kwa hivyo sisi M bye bye
 

Kipimo cha umakini ni umakini, fine enough, umakini ambao wewe mwenyewe umeshindwa na
umekiri kushindwa kuu-demonstrate.
Mwanasiasa na mwanazuoni ipo tofauti KUBWa.Sababu kwamba mtu alikuwa mwanazuoni
kisha kuwa mwanasiasa haina maana ana wajibu na majukumu yaleyale, maana kule
kwene uanazuoni inabidi a-demonstrate vitu fulani mbele ya wenziwe ili kuendeleza
libeneke la uanazuoni wake.Kila moja lina requirements zake. Kwanza nimeweka scenario
2 hapa, moja kwamba mwanazuoni anawasilisha kazi yake inakataliwa na pili mwanasiasa Slaa
anajibu hoja ya say,Malaria Sugu JF. Wewe ukadismiss scenario ya kwanza kwamba sio KIPIMO ila ya pili ni kipimo..narejea tena kusema huu ni upuuzi.

Hoja ya kwanza hapa ni kwamba kama kuandika JF ni kipimo cha umakini,
kwanini mwanazuoni kuandikia kazi na kuipeleka kwenye chapisho linalohaririwa isiwe kipimo.

pili, furthermore nimesema hapa JF sio mahala pa kusema kwamba Slaa alitakiwa aandike
kwa standards za article ya gazeti au kitabu..this is a damn forums..ni sawa kuandika
vyovyote ili mradi kinasomeka na kueleweka. Ukitaka kumpima kwenye maandishi JF sio mahali pake.

Nimesema sijasema kwamba nimesema sijasema, don't misquote me.

It doesn't matter, utasema tu.


Kungekuwa hakuna readability ni wazi hakuna mtu angeuliza content, watu wangeuliza awasilishe upya post yake. Suala kwamba umeweza kuona hiyo 'onus of proove', ni wazi u were able to read the msg. Imeumiza macho lakini it was readable.

Kama nilivosema, JF sio sehemu ya kupimia umahiri wa makatibu muhtasi ..wewe unatafuta secretary wakati wenzio wanasaka Rais, sasa how do u explain wale ambao hawapo JF kama criterion ni ukatibu muhtasi JF? its getting really funny.

Nishakwambia hiyo ni typo, nishakwambia mimi niko prone kufanya makosa, nishakwambia standard ya kumwekea kafuku kama mie nisietaka hata ofisi ya katibu kata ni tofauti na ya Dr. Slaa. Lakini sikukosea kusema "onus of proove".
Kusaka urais manake unatakiwa kuwa malaika asiyeandika 'onus of proove', ila wengine ni ruksa sivo?

Might be flawed self-importance or grandeur. Sadly i don't know how many jayefers really cares.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…