Binafsi simuoni Bw Mbowe kama Presidential material. Actually hata ku run Wizara kama waziri pia ni mtihani unless iwe ndani ya mifumo kama ya CCM ambapo uwezo wa mtu hauna maana sana. Ni kujuana kimaslahi zaidi. Mbowe, Mimi kama fan wake, ANAFAA SANA kuwa kiongozi wa chama, Kiongozi wa Upinzani, Mbunge mwenye maarifa na zaidi mwanasiasa mwenye uthubutu wa hali ya juu aliyevaa ujana mwingi japo mzee, kiasi cha kuaminika kwa vijana wengi nchi hii na ndio sababu ya HOFU dhidi yake.
Pia ni mtu akiyekulia maisha yasiyojua njaa , haijui dhiki na ni mtoto wa mjini Dar sehemu nyeti na anajua siri nyingi mno za serikali. Ni sifa hizo Wanaomtesa ambao wao hawana background iliyoshiba kama ya Mbowe, wanamtamani aingie chamani kwao. Hilo ndilo linalofanya Mbowe aogopwe na watawala. Kwamba akiungana na mjanja wa hoja za ki predidential material mwingine kama Lowassa au Lissu ni disaster kubwa na hakika ya kuiondoa CCM iliyokufa madarakani. Ndio maana kesi hazipungui kwao.
Hii kesi ya sasa architect alikuwa mwendazake na kwa sababu hayupo, na Hangaya approach yake zaidi sio kuua, kuteka au kudhulumu itapatwa na natural death. Moyoni mwa Hangaya haitaki lakini iko iliasisiwa akiwepo serikalini na anatambua nguvu kubwa ya kimalengo iliyokuwa nyuma yake ambayo kwa sasa hana uhakika na consequence ya matokeo ya uamuzi wa aina yoyote. Hajui ateme au ameze. Viongozi wakuu wa vyombo vya dola waliosaidia kuliasisi ni walewale waliopo leo wakimlinda yeye Hangaya pia na who knows wanamwambia ukweli kiasi gani.