Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Uchaguzi 2020 Je, Halima Mdee amefanya nini Kawe kwa miaka 10 ya ubunge wake kustahili kuendelea? Sikia ya Askofu Gwajima, 28 Oktoba fanya uamuzi sahihi

Paschal sasahivi hata kuingia jamvini unaona aibu heshima ambayo ulijijengea umekuja kuiharibu sababu ya njaa.
 
Wewe ulikua unagombea kusindikiza wenzio,pambana upate hata viti maalumu.
Naskia team yenu ni mauno tu hakuna jipya
 
Mkuu inawezekana kabisa Bi Halima J. Mdee hajafanya chochote (endapo wabunge wakiwa na ambacho wanaweza kufanya wao kama wao) lakini kumleta Gwajima ni dharau sana kwa wapiga kura...!!
Gwajima haaminiki... Mropokaji... Mtukanaji... Mdhalilishaji...
Kabisa limemshinda atawezana na Ubunge??
 
Anaelezea hayo kwenye kampeni nenda kwenye mikutano yake ili akakubadilishe kabisa umpe nakura
 
Primitive analysis basing on roles of Mbunge vs Gorvement ,in this case both Local and Central Government!
Paschal hii Ni akili yako kweli,kwa hiyo mtu amijitolea tu kuchimba kisima tayari kisha faa kuwa Kiongozi!
 
Gwajima kaifanyia jambo kubwa Kawe la kuwala maboga kondoo wake😜😜😜😜😜😜
Ukweli upo wazi gwaji hana mpinzani , bi kidude hajafanya chochote cha maana jimboni kawe.
 
Kaka
Naona mlioshindwa kura za maoni mnatekeleza agizo la Mwenyekiti wenu kuwapigia debe waliopita!Hapa unajiwekea kafursa ili ukumbukwe kwenye teuzi kwa kutii maagizo ya mwenyekiti!Huwezi kutenganisha ukada wako na mawazo yako,kwa wanaJF utakuwa mnywa maji ya kijani tu!

Kujijengea heshima fulani na kuaminika inachukua muda mrefu,ila kuvivunja vitu hivyo ni ndani ya sekunde moja tu!

Ulishapoteza hilo na huenda mpaka unaingia kaburini,level ya heshima uliyokuwa nayo JF isirudi tena!

Ni bora ukubaliane na hali na uwe kijani kweli kweli,,kuwa kama polepole tu!
Challenge hoja zake sio personality, sasa hapo umejibu hoja gani ya Paschal
 
Paskali, Umeingiaje kwenye tego hili la ukabila?? Hilo swali lako kweli limetoka kwako wewe au mtu kaiiba akaunti yako? Unawezaje kuuliza swali la kitoto kihivyo? Umetunga mtungo mreefu kumbe hakuna kitu?? Yaani unataka Gwaji aje kuchukua sadaka yake aliyoitoa kwa watu wa Kawe? Hii si haki kabisa. Sio kasi ya mbunge kulima barabara wala kutengeneza madaraja. Hiyo ni kodi yetu inafanya hivyo. Mmeondoa vyanzo vyote vya mapato kutoka Halmashauri mkazipeleka hazina kuu. Tusaidie kuuliza; Makusanyo ya kodi zetu yamefanya nini Kawe?? Kama fungu lilitolewa akazibana Halima Mdee leteni data hapa tumbane hadi azikojoe hadharani. Kama mmezibana nyie ili aonekane hajafanya kitu kwa kuwa hakutoa zake mfukoni, Hapo imekula kwenyu na mchungaji wenyu. Paskali. Never again ask such a silly question
 
Kwa jinsi siku zinavyokwenda toka upigwe chini kura za maoni ndivyo nazidi kujiridhisha kuwa sikuwa nimekosea kutokukuchukulia mtu makini toka nijiunge Jamii Forums.

Ni mtu unayejifanyaga impartial lakini kumbe sio kweli. Mnafiki na mganga njaa kama wapuuzi wenzio wengi tu.
Pathetic.

Mithread yako huwa imejaa maneno meeengi...lakini mostly ni upumbavu mtupu.
Misiredi yakufuatana kila baada ya dakika kadhaaa....hana.jipya huyu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom